Tanzania tunaelekea wapi? Kama maji na umeme bado ni shida?

Tanzania tunaelekea wapi? Kama maji na umeme bado ni shida?

Cash Generating Unit

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2019
Posts
13,284
Reaction score
39,513
Ndugu habari zenu,

Unajua sometimes unawaza jinsi nchi yetu ilivyobarikiwa kuwa na bahari, maziwa, mabwawa na mito lakini suala la umeme na maji bado ni shida.

Tuna viongozi ambao hawana uchungu na maisha ya Watanzania wanajali matumbo yao, tuna viongozi ambao wanashindwa kubuni vyanzo vya maji na umeme miaka 60 ya uhuru lakini maji ni shida. Viongozi wameshindwa jenga matank ya kuhifadhia maji kumbuka tunakatwa tozo zinakwenda wapi??.

Kiongozi anakwambia maji yamekauka simple tu zingekua nchi za wenzetu angebondwa na mawe. Maana wameshindwa kabisa hata kutumia akili kujenga matank ya akiba hasa kipind cha kiangazi. Pita mwenge pale kuna nuka mikojo hatari, vyooni hakuna maji hali ni mbaya Dar es salaam. Kwa hali hii ya umeme na maji tutapata wawekezaji?

Tanzania tumebarikiwa tuna maziwa mikoa mbalimbali kama ziwa Victoria, Tanganyika, Nyasa, Rukwa, Eyasi, Natron, Manyara, Burigi, Balangida, Jipe, Babati, Ambussel na Chala nknknk. Tuna vyanzo hivo vyote lakini bado tunategemea maji kutoka Ruvu ni AIBU kwa viongozi wetu kwamba imeshindikana kutoa maji kwenye hivo vyanzo??? Serikali inashindwa kujenga matank kwa ajili ya kuweka reserve ya maji?

Tuna Natural gas bado tunagangaika na mabwawa kwanini tusitumie gas yetu kuzalishia umeme?? Sometimes tumshukuru mwendazake aliyekumbuka kujenga bwawa la nyerere. Nchi za uarabuni ni jangwa lakini hazina shida ya maji wanatoa wapi maji?.

Kweli Tanzania ya kuhangaika na maji wakati tuna vyanzo vya maji kila kona? Mungu atusaidie kwa hali hii wawekezaji tutawasikia tu GAME supermarket washatangaza wanafunga biashara.
 
Iko wazi kwamba hawa wazee wameshindwa kutatua changamoto za maji na umeme...miaka 60 bado shida ni zile zile tu.

Kuna nchi nahisi ni netherlands (wadachi) wanatengeneza mvua jamani.
Sisi bongo tumekalia siasa tu
 
Iko wazi kwamba hawa wazee wameshindwa kutatua changamoto za maji na umeme...miaka 60 bado shida ni zile zile tu.

Kuna nchi nahisi ni netherlands (wadachi) wanatengeneza mvua jamani.
Sisi bongo tumekalia siasa tu

Wanawaza teuzi na uchawa
 
Uzuzu mwingi, je wananchi wa Dodoma wanahitaji maji Safi na salama au kuwa na international Airport?,route hii ambayo mashirika mengi ya ndege yanatumia yanapokwenda kusini mwa Africa, kuna airports nyingi tu incase kunatokea emergency, Dodoma ipo less than 500km from Dar,ya nini kuwa na Airport?,fedha zile bora zitumike kwenye service delivers including safe water
 
Uzuzu mwingi, je wananchi wa Dodoma wanahitaji maji Safi na salama au kuwa na international Airport?,route hii ambayo mashirika mengi ya ndege yanatumia yanapokwenda kusini mwa Africa, kuna airports nyingi tu incase kunatokea emergency, Dodoma ipo less than 500km from Dar,ya nini kuwa na Airport?,fedha zile bora zitumike kwenye service delivers including safe water

Sion umuhimu wa international airport pale dodoma kwa sasa. Watengeneze miundo mbinu ya maji maana hata dodoma maji ni shida
 
Hii ilikuwa 8 September 2015 kipindi cha uchaguzi mkuu
Screenshot_2022-10-30-21-43-51-041_com.google.android.apps.photos.jpeg
 
Chini ya utawala wa CCM utatuzi wa suala la maji nchini utabaki kuwa ni ndoto.
 
Tuchukue maji ziwani tupeleke kwenye miji yote yenye changamoto ya maji.

Kandarasi apewe mchina atandaze mabomba ya maji katika miji yetu,makampuni ya wazawa yanazengua na yanachelewesha kukamilisha kazi.
 
Miaka yote iliyopita mlikuwa mnamsubiria Samia?

Haya tunaelkea huku 👇
 

Attachments

  • Screenshot_20221030-082814.png
    Screenshot_20221030-082814.png
    45.2 KB · Views: 13
  • Screenshot_20221030-082935.png
    Screenshot_20221030-082935.png
    206.2 KB · Views: 15
  • Screenshot_20221030-083019.png
    Screenshot_20221030-083019.png
    125.5 KB · Views: 15
Kuhusu umeme tunaelekea huku 👇
 

Attachments

  • Screenshot_20221030-080052.png
    Screenshot_20221030-080052.png
    172.7 KB · Views: 15
  • Screenshot_20221030-080038.png
    Screenshot_20221030-080038.png
    166.4 KB · Views: 15
  • Screenshot_20221030-080017.png
    Screenshot_20221030-080017.png
    105.8 KB · Views: 14
Mimi siwalaumu viongozi ata kidogo.wananchii ni mizigoo tumebaki tunawaangalia kwa nini nguvu ya umma tusiwatoe madarakani??
 
Hii nchi ni kwamba ukipata nafasi kula na familia yako...suala la uwajibikaji hiyo kwetu ni stori tu
mungu ibariki Tanzania
 
Back
Top Bottom