Tanzania, tuko salama?

Tanzania, tuko salama?

Eistein

JF-Expert Member
Joined
Nov 24, 2011
Posts
1,107
Reaction score
482
Wadau salaamuu, kichwa cha habari cha husika.

Tumeona matukio mengi sana ambayo kwayo haikuwa desturi sana kuyasikia miaka takribani 15-20 iliyopita, miaka ya 2012-2014 tulishuhudia mapadri na mashekhe wakimwagiwa tindikali na kuuwa (zanzibar, na arusha).

Tunakumbuka kutekwa na kuteswa kwa dr. Ulimboka, kumwagiwa kwa tindikali kwa mmliki wa home shoping centre, mwandishi kubenea etc.

Tukashuhudia milipuko yaa mabomu katika mikutano ya kisiasa pamoja na kanisa la olasiti hapo arusha. Katika matukio haya yote mimi binafsi sijaona juhudi harisi za usalama zikichukuliwa, naweza sema ni kama zima moto yanapotokea hayo ndio tunaona tume zikiundwa na zikitumia fedha nyingi sana, lakini hatma ya hayo matukio/ripoti hubaki katika makabati watanzania tunasahau na kusubiri tena tukio lingine litokeee ndio kamati ziundwe.

Wahusika wa matukio hayao ni nadra sana kusikia wamekamatwa au huo mtandao kweli umethibitiwa, maana ungekuwa umedhibitiwa hayo matukio bila shaka yangekoma.

Enzi za nyerere ilikuwa ikihisiwa kuwa ukisema neno lolote baya juu ya serikali au ukitaka kufanya uhalifu basi muda si mrefu utakamatwa, lakini leo hali ni tofauti kabisa, je kama taifa wapi tumekosea??. Kama taifa sioni mkakati mathubuti wa usalama, polisi na vyombo vya usalama.

Binafsi naona vyombom vyetu vya ulizni na usalama vipo kimatukio zaidi lakini si watu wa kuweza kutrace jambo kabla halijatokea na kulidhibiti. Sasa juzi tumeona kijana mtanzania amekamatwa hapo kenya katika tukio la garrisa university , alikuwa mwanafunzi wa bihawana dodoma tena kijana mdogo tu form 5 (pcb), kwa melezo yake anakili kuwa alikuwa member wa alshababu.

Sasa ni vijana wangapi kama hawa tuko nao uraiani,ni wangapi wamesharubuniwa na magaidi.

Je kwa hali hii tunakoelekea je taifa liko salama??? Wapi tumekosea?? Nini kifanyike??;
 
Kutokana na tishio la mambo ya uhalifu ilivyo sasa naomba watu wote wenye mapenzi mema na nchi hii tuchukue hatua za kumwomba mkuu wa nchi afumue mfumo wa kiusalama katika jamii unaotusimia kwa sasa!

Nashauri tuunde uongozi tambuzi wa familia badala ya vitongoji au mitaa ilivyo sasa.

Tukiwa na kiongozi mwenye mipaka isiyozidi nyumba kumi itasaidia sana utambuzi wa jamii na shughuli zake, na kupitia kiongozi huyu itakuwa rahisi kwa serikali kubaini nini kinachofanyika wapi, kiuchumi, uzembe, majanga, uhifadhi wa maovu nk.

Mpaka sasa viongozi wa mitaa ni wakujitolea lkn mitaa ni eneo kubwa, na usalama wetu hauwezi kuletwa na polisi, tukianza kufahamiana itakuwa rahisi kuwatumia polisi kuja maeneo yetu.

Rai yangu kingozi wa nyumba kumi atasaidia zaidi usalama wa raia.
 
Usalama unaanza na mimi na wewe. Kilakitu mkulu ndo afanye!
 
Ni wazo zuri kwa usalama wa Taifa letu. Mabalozi wa nyumba kumi kumi wapewe meno maana ulinzi sio jambo la vyombo husika tu. Kupitia Balozi hizo kila mtanzania atakuwa mlinzi wa mwingine maana Mabalozi ni rahisi sana kufikika.
 
Mkuu hoja yako ni nzuri,na nakupongeza kwa kuliona hilo
Naomba niongeze kuwa,ulinzi uwe ni jukumu letu sote
kama unaona jambo lisilo la kawaida chukua hatua au kumjulisha mjumbe
wakati mwingine toa taarifa polisi kabisa.

Kama huyo jirani yako mna mahusiano mazuri,unaweza kumwuliza
juu ya jambo unaloliona kwake lisilo la kawaida,kuna mambo mengine unaweza kuta na mjumbe yumo kwenye dili,
Ndo maana sehemu nyingine raia tujifunze kuchukua hatua wenyewe.
 
Ni swali tu,

Salaamu wanaJF,
pili salamu ziwaendee wanausalama wa Taifa letu, awali niwapongeze na kuwapa pole kwa kazi nyingi na nzuri, lkn niseme tu nzuri zile tu mlizofanya kwa uaminifu kulinda usalama wa taifa letu, bila kutanguliza maslahi binafsi kwa gharama ya uhai wa Tanzanzia.

Sote tunakumbuka hivi karibuni tulikutwa na matukio mbalimbali ya kugusa kustua usalama wa watanzania.
Lakini bila kurefusha linalonigusa zaidi ni tukio lile la watu wasiofahamika kuwaua na kuwanyang'anya silaha polisi katika matukio mbali mbali, ambayo nadhani hadi leo hayana jibu.

Tumesikia matamko mbalimbali kuwa waliohusika na uhalifu huo wangekamatwa mara. Lakini hadi leo ni zaidi ya miezi, tangu tukio la kwanza hakuna hata silaha moja iliyokamatwa, hakuna hata mtu mmoja wa wahusika aliyesemekana kukamatwa, hatujui wahusika.

Hatujui serikali pamoja na wanausalama, au kupitia kwa wanausalama wanafanya mikakati gani kutuhakikishia usalama wetu. Hatujui wahusika wa uhalifu watafanya tukio lingine lini la mauaji wa polisi na kunyang'anya silaha tena. Mungu aliepushe hiyo mbali.

Lakini najiuliza tu, tupo salama kweli? Wanausalama wa Taifa mmeridhika na hali hiyo?

Siamini kama uwezo na ujuzi wenu unazidiwa na vibaka. Siamini kama mnashindwa kutumia mbinu zenu zote za ujuzi na uzoefu kuwakamata wauaji wa polisi, na zaidi waliopora silaha, kwani watatumia kwa uhalifu unaofuata wa raia wengine. Sipendi kuendelea lakini niseme wazi kuwa inaniuma.

Sitaki nigusie haya matukie mengine kuwa wamekamatwa sijui morogoro, mara matukio ya Amboni, maana haya hata bado ni kitendaliwili, na kama ni ya kweli? Usalama wa watanzania upo wapi ikiwa Alshabaaba wanafika hadi kilombero na silaha kali za kivita?

Inaniuma zaidi pale ambapo maslahi binafsi yanaingizwa kwa gharama ya maisha ya m/watanzania.
 
Kwa system mbovu na siasa chafu tulizonazo katika nchi hii,usalama wa Wanzania ni Mungu tu anausimaia!
 
Tanzania kuna wanausalama au jeshi la watunisha misuli kwa wapinzani?
 
JKT wale ni wanajeshi kwa asilimia kubwa, sema tunawachukulia Poa.
Tunaweka usalama wetu rehani ndo maana hata sisi katika siasa tuna red brigade, green guard, blue guard sisi nao kule ACT tutaanzisha white guard na kule mtaani tutaanzisha kitaa guard na hata ofisini tutakuwa na kiiivu guard kwa kuwa system wenyewe imeruhusu kuwa na makundi ya kupinda usalama Zaidi ya usalama wa taifa na jeshi la polisi..... Ngoja niwahi mazoezi kule katika blue bahari guard kikosi cha ulinzi kule nakocheza mpira
 
Back
Top Bottom