Tanzania tuko awamu ya ngapi ya uongozi?

Utotole

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
6,604
4,259
Nimekuwa nikifuatilia kwa muda mrefu sasa na kuzidi kuchanganywa na jinsi tunavyozipambanua awamu za uongozi, hasa urais katika nchi yetu.

Mfano Baba wa Taifa Mwalimu JK Nyerere tunamwita Rais wa awamu ya kwanza (na awamu ile inaitwa ya kwanza). Ali Hassan Mwinyi watu wanamwita rais wa awamu ya pili, Benjamin William Mkapa anaitwa rais wa awamu ya tatu na Jakaya Mrisho Kikwete anaitwa rais wa awamu ya nne.

Kwa mchanganuo huo inaelekea hadi sasa Tanzania tuko katika awamu ya nne! Mimi nina fikra tofauti na nina hakika si mimi peke yangu mwenye fikra kama hizo. Kama ni sahihi au si sahihi naomba tueleweshane maana ni suala la uelewa na kwa kuwa vyombo vya habari hutumia awamu kama nilivyozichanganua, ni dhahiri wananchi walio wengi wataelewa hivyo kwa kuwa wanasikia hivyo kila wakati.

Mawazo yangu ni kama ifuatavyo:

Mwalimu JK Nyerere alikuwa wa awamu ya kwanza, hilo halina mjadala maana ninaamini hatukuwahi kufanya uchaguzi wa kitaifa wakati wa uongozi wake, uchaguzi ambao ungeweza kumwondoa madarakani na kumweka mwingine. Yeye anabaki kuwa rais wa kwanza, na rais wa awamu ya kwanza.

Ali Hassan Mwinnyi alikuwa rais wa awamu ya pili, na ya tatu! Kwa kuwa katiba ilisema kuwa urais ni miaka mitano kwa awamu moja, Mwinyi alipigiwa kura ya Ndiyo/hapana mwaka 1990 (haijalishi ilipigwaje). Kwa maana hiyo, kama watanzania wangempigia kura nyingi za hapana, angeongoza awamu moja tu (1985-1990). Kwa kuwa alipita tena hadi 1995, mimi naona hizo ni awamu mbili. Kwa mtazamo wangu basi, Mwinyi ni rais wa pili, na rais wa awamu ya pili na ya tatu!

BW Mkapa ameingia madarakani wakati wa vyama vingi, 1995-2000. Kisha akagombea tena na kushinda 2000-2005. Hizo ni awamu mbili. Kwa sababu mwaka 2000 kama angeshindwa kwenye kura za maoni ndani ya CCM au kushindwa uchaguzi mkuu mwaka huo (say na mgombea wa NCCR-Mageuzi) angekuwa ameongoza awamu moja tu ya miaka mitano. Kwa kuwa alishinda tena 2000-2005, hiyo ilikuwa awamu ya pili kwake. kw mtatzamo wangu basi, Mkapa ni rais wa tatu, na rais wa awamu ya nne na ya tano!

JK Kikwete aliingia 2005 hadi 2010 akamaliza awamu yake ya kwanza ambayo mimi naiita awamu ya sita kwa jumla Tanzania. Kama angepata mpinzani CCM, au hata kuangushwa na upinzani (say Dk. Slaa) angeishia awamu ile tu.

Kutokana na hayo, mimi naamini kwa sasa Kikwete japo ni rais wetu wa nne bado hatuwezi kumwita kwa usahihi rais wa awamu ya nne, wakati anaongoza awamu 2! Mimi ningemwita rais wa nne, ila kuhusu awamu ningemwita rais wa awamu ya sita na ya saba, (1 ya Mwl Nyerere, 2 za Mwinyi, 2 za Mkapa na 2 za Kikwete) Katiba inatafsiri awamu kuwa miaka mitano. Ninaviomba vyombo vya habari viwaeleza wananchi kwa usahihi kuhusu mambo kama haya ambayo yanaonekana madogo lakini katika nchi changa kidemokrasia, haya ni ya muhimu. Sitashangaa kusikia kuna mahali watu walimpigia kura Kikwete kwa kuwa wanachojua ni kwamba bado hajamaliza muda wake!!

Mwenye mtizamo tofauti naomba anieleweshe, na awaeleweshe na watanzania wote juu ya suala hili ambalo limekuwa likiendelea miaka yote.

Naomba kuwasilisha.:thinking:
 
Back
Top Bottom