TANZANIA TAJIRI MASKINI
TATHMINI YA KUDORORA KWA MAEMDELEO LICHA YA RASILIMALI LUKUKI
Mwandishi: Bakran Awadh Ali
Tarehe 23 juni 2025
UTANGULIZI
Tanzania ni miongoni mwa mataifa yenye utajiri mkubwa wa rasilimali barani Afrika. Tangu kupata uhuru mwaka 1961, taifa hili limekuwa na matarajio makubwa ya kujitegemea kiuchumi, kuboresha maisha ya wananchi wake, na kufanikisha maendeleo ya kijamii na kisiasa.
Hata hivyo, zaidi ya miongo sita baadaye, hali halisi ni tofauti kabisa kiwango cha umasikini kimeendelea kuwa juu, miundombinu mingi ni duni, na mamilioni ya Watanzania wanaishi chini ya kiwango cha maisha ya binaadamu
Ripoti hii inachambua sababu kuu za kudorora kwa maendeleo ya Tanzania, licha ya kuwa na rasilimali nyingi. Pia, inatoa mapendekezo ya mwelekeo sahihi wa kiutawala na kiuchumi, kwa kuzingatia mifano kutoka nchi ambazo zimepiga hatua kubwa katika mazingira yanayofanana na yetu.
TANZANIA NA RASILIMALI ZAKE
Dhahabu
Reserves za dhahabu zimekadiriwa kufikia 45 milioni (~1 270 tonnes).
Uzalishaji unazunguka 39–50 tonnes kwa mwaka; mwaka 2020 ilikuwa takribani 47 tonnes.
Diamonds
Migodi ya almasi ni kishap (Williamson) yenye zaidi ya 38.1 milioni carats.
Uzalishaji wa almasi ulikuwa 399,615 carats mwaka 2019; 298,130 carats mwaka 2020.
Tanzanite
Tanzania pekee ina rezerves za takribani 109 milioni carats; eneo la Block C lina takriban 87.1 milioni carats.
Zaidi ya 2.4 milioni carats zimetoka mwaka 2011; rekodi kubwa ilijumuisha mawe ya zaidi ya 15 kg (33,000 carats).
Makaa ya Mawe (Coal)
Rezerves zilizothibitishwa 0.4–1.9 bilioni tonnes kuna makadirio hadi 5 bilioni tonnes.
Uzalishaji mwaka 2019 ulikuwa 712,136 tonnes; kama ilivyo 2015 ilikuwa 250,000 tonnes.
Iron Ore
Migodi kama Liganga ina rezerves zisizopungua 126 milioni tonnes.
Nickel / Copper / Cobalt
Kabanga Nickel sulphide deposit ni moja ya kubwa duniani, ingawa haijachimbwa kwa wingi.
Makadirio ya mauzo: 500,000 tonnes nickel, 45,000 tonnes cobalt, 75,000 tonnes copper.
Uranium
Rezerves makubwa katika maeneo ya Namtumbo (Mkuju), Bahi, Manyoni, n.k.
Mradi wa Mkuju River una 182.1 milioni tonnes za rezerves.
Gesi Asilia
Makadirio ya gesi: 57.5 Tcf (trillion cubic feet) mwaka 2020.
Songo Songo inakadiriwa kuwa na 20 milioini tonnes (gas) kwenye visiwa vya Songosongo.
Helium
Eneo moja la bonde la U rift lina angalau 54 bilioni feet³ za helium.
Madini ya Kichumvi / Industrial Minerals
Kaolin, bentonite, soda ash, gypsum, phosphate…
Kaolin pekee kwenye Pugu Hills ni kubwa.
Marble, limestones: miongoni mwa Tanga Cement huzalisha 500,000 tonnes cement/year.
Mbuga za Wanyama na Utalii wa Asili (Wildlife Parks & Tourism)
Tanzania ni miongoni mwa nchi chache duniani zilizo na hifadhi kubwa za wanyama pori, na utalii unachangia zaidi ya 17% ya pato la taifa.
Mbuga za Taifa (National Parks – TANAPA) Jumla: 22 mbuga
Serengeti National Park – Eneo: 14,763 km² (UNESCO Heritage Site)
Ruaha National Park – 20,226 km² ya pili kwa ukubwa Afrika
Jumla ya ardhi ya hifadhi: asilimia 38 ya uso wa nchi (365,000 km²) ni eneo la hifadhi za wanyamapori (hifadhi za taifa, misitu, game reserves, n.k.)
Bahari ya Hindi na Mwambao (Blue Economy)
Tanzania ina mwambao wa takriban 1,424 km (kati ya bara na Zanzibar) wenye rasilimali nyingi
Rasilimali za Bahari:
Samaki wa bahari ya kina kirefu – tuna, prawn, octopus, sardines, n.k
Mwani (Seaweed) – hasa Zanzibar, hutumika kutengeneza bidhaa za urembo na dawa.
Maeneo ya matumbawe (Coral Reefs) – takriban 3,500 km²
Mangrove Forests – zaidi ya 115,500 ha (hususani Rufiji, Pangani, Lindi)
Bandari na Usafirishaji wa Kimkakati
Tanzania ni lango kuu kwa Afrika Mashariki na Kati.
Bandari Kuu:
1. Bandari ya Dar es Salaam
Inahudumia zaidi ya 90% ya shehena ya Tanzania
Ina uwezo wa kupokea meli zaidi ya 3,000 kwa mwaka
2. Bandari ya Tanga
Inahudumia kaskazini, pia bomba la mafuta kutoka Uganda linapita hapo.
3. Bandari ya Mtwara
Eneo la maendeleo ya LNG (Liquefied Natural Gas).
4. Bandari za Zanzibar (Malindi na Mkoani)
Malindi inahudumia biashara ya visiwani na baharini kwa kiasi kikubwa.
Maeneo ya Kimkakati:
Bandari Kavu (Dry Ports): Isaka (Shinyanga), Kigoma, Mwanza – kusaidia nchi zisizo na bandari kama Zambia, Rwanda, Burundi, DRC.
Ardhi
Zaidi ya asilimia 44 ya ardhi ya Tanzania inafaa kwa kilimo. Mazao kama kahawa, chai, korosho, pamba na mazao ya chakula yanatoa ajira kwa zaidi ya asilimia 65 ya Watanzania.
Nguvu kazi: Takribani asilimia 60 ya Watanzania ni vijana walio chini ya miaka 25 — kundi lenye nguvu na uwezo mkubwa wa kuzalisha.
Pamoja na haya yote, maendeleo bado ni ya kusuasua.
3. SABABU ZA KUDORORA KWA MAENDELEO
A. Uongozi Mbovu na Ukosefu wa Dira ya Maendeleo
Tanzania haijawahi kuwa na mpango wa maendeleo wa muda mrefu uliofuatiliwa kwa ufanisi mfululizo kati ya tawala tofauti. Uongozi umejikita zaidi katika miradi ya kutangaza jina la mtu au chama, badala ya mahitaji halisi ya wananchi.
B. Rushwa na Ubadhirifu wa Mali za Umma
Takwimu kutoka Taasisi ya Transparency International zinaonyesha Tanzania imekuwa ikishika nafasi za juu kwa kiwango cha rushwa barani Afrika. Sakata kama EPA, Richmond, Escrow, na mikataba ya madini ni mifano halisi ya jinsi utajiri wa nchi unavyopotea.
C. Mikopo ya Miradi Mikubwa Isiyo na Tija ya Moja kwa Moja
Miradi kama ujenzi wa Magufuli City, ununuzi wa ndege, na ujenzi wa majengo makubwa Dodoma imeigharimu serikali mabilioni ya shilingi kwa mkopo. Miradi hii ni “necessary but not urgent,” wakati sekta muhimu kama elimu, afya, maji, na kilimo zinakosa fedha za kutosha.
E. Ukosefu wa Uwazi katika Usimamizi wa Rasilimali
Hakuna upatikanaji wa hadharani wa mikataba ya kimataifa kuhusu madini, bandari, au gesi. Hii huweka mianya ya ufisadi na upendeleo wa makampuni ya kigeni.
F. Mfumo wa Elimu Usiohusiana na Maendeleo
Mfumo wa elimu umeendelea kuzalisha wahitimu wasioweza kushindana katika soko la ajira au kujiajiri. Tija ya elimu haionekani kwenye uzalishaji wa taifa.
4. DENI LA TAIFA NA MAISHA YA MWANANCHI WA CHINI
Hadi kufikia mwaka 2025, deni la taifa linakadiriwa kuwa zaidi ya TSh trilioni 105. Hili linaifanya serikali kutumia sehemu kubwa ya mapato kulipa madeni badala ya kuhudumia wananchi. Matokeo yake:
Vituo vya afya havina dawa wala vifaa
Elimu ya msingi na sekondari inakosa walimu na madarasa
Bei ya bidhaa muhimu iko juu
Watanzania zaidi ya milioni 15 wanaishi chini ya dola 1.90 kwa siku
5. NANI WA KULAUMU KWA TANZANIA KUFIKIA HAPA?
1. Viongozi wa Serikali (Serikali zote tangu Uhuru)
Sababu: Wamekuwa wakipewa mamlaka ya kusimamia rasilimali, kutunga sera, na kuhakikisha maendeleo ya wananchi, lakini wengi wao wameweka mbele maslahi yao binafsi au ya chama kuliko taifa.
Mifano:
Kufanya maamuzi ya kifedha bila mashauriano ya kitaalamu au uwazi (mfano: mikopo ya mabilioni ya SGR, Stiegler’s Gorge, Magufuli City na mengineyo).
Kuwekeza zaidi kwenye miradi ya kuonekana kisiasa badala ya afya, elimu, maji, au sekta ya kilimo ambayo ndiyo injini ya maisha ya watu wa kawaida.
2. Chama Tawala (CCM)
Sababu: Kikiwa chama kilichoshika hatamu za uongozi tangu 1961 (Tanganyika) na 1964 (Zanzibar), hakiwezi kukwepa lawama. Mfumo wa chama kimoja hadi 1992 uliua ushindani wa kisera na uwajibikaji.
Madhara: Ukosefu wa checks and balances. Mfumo uliojenga viongozi wa "ndiyo mzee" bila uwajibikaji wa kweli kwa wananchi.
3. Bunge na Wawakilishi Wetu
Sababu: Bunge limegeuka kuwa muhuri wa kupitisha maamuzi ya serikali bila uchambuzi wa kina wa bajeti au mikataba.
Matokeo: Limepoteza nguvu ya kuisimamia serikali kwa niaba ya wananchi. Wabunge wengi hawasemi ukweli kwa kuhofia kupoteza nafasi zao au kukatwa kwa posho.
4. Vyombo vya Habari na Wasomi Wanyamavu
Sababu: Wasomi wengi wamekuwa wakikaa kimya au kuwa waoga kusema ukweli kuhusu hali ya taifa. Vyombo vya habari pia vingi vinaogopa kuikosoa serikali.
Matokeo: Kukosekana kwa sauti huru ya kuhamasisha mabadiliko au kuelimisha wananchi kuhusu haki zao na udhaifu wa sera.
5. Wananchi Wenyewe
Sababu: Tumekuwa tukiridhika na hali duni, kuchagua viongozi kwa misingi ya ukabila, udini, au takrima. Tumeacha kuhoji na kudai uwajibikaji.
Matokeo: Tumewapa mamlaka watu wasiofaa, halafu tunakaa kimya tunaponyonywa.
Lawama kubwa zinaenda kwa viongozi waliokalia madaraka bila dira ya kweli ya maendeleo ya watu. Lakini pia CCM kama taasisi, wabunge wasio wakilishi wananchi ipasavyo, vyombo vya habari na wasomi wanyamavu, pamoja na wananchi wenyewe kwa kutokuwa na mwamko wa kudai haki yao.
6. Mapendekezo ya Mabadiliko
1. Marekebisho ya kisheria na kisera kwa kuongeza uwazi wa mikataba ya kimataifa na mashirika ya umma.
2. Kuweka mipaka ya ukopaji wa kitaifa kwa kipaumbele cha sekta za huduma za msingi.
3. Kuimarisha taasisi za uwajibikaji kama TAKUKURU, Bunge, CAG, na Mahakama kwa kujitegemea kisiasa.
4. Kuwekeza kwa vijana kupitia elimu inayozalisha ajira na ujuzi wa uzalishaji.
5. Kuwezesha sekta binafsi na viwanda vya kuongeza thamani kwa rasilimali zetu.
6. Kujifunza kutoka kwa nchi zilizofanikiwa kwa muktadha wetu, si kwa kufuata kila kitu bila uchambuzi wa kina
7. NCHI TUNAZOWEZA KUIGA
Rwanda
Pamoja na kupitia mauaji ya kimbari mwaka 1994, Rwanda leo ni mfano bora wa nidhamu ya fedha, uwazi katika utawala, na matumizi sahihi ya rasilimali. Wamewekeza kwenye TEHAMA, viwanda vidogo, na usafiri wa umma wa kisasa.
Botswana
Tangu uhuru, Botswana imesimamia kwa mafanikio madini ya almasi kupitia kampuni ya Debswana, kwa uwazi na kwa manufaa ya wananchi. Miundombinu bora, elimu, na huduma za kijamii zimepewa kipaumbele.
Malaysia
Ilipitia umasikini mkubwa miaka ya 1960, lakini leo ni taifa lenye uchumi wa viwanda. Mafanikio yao yamejengwa juu ya elimu bora, uwajibikaji wa serikali, na mazingira wezeshi kwa uwekezaji wa ndani na nje
Vietnam
Baada ya vita vya muda mrefu, Vietnam ilijenga uchumi wake kupitia kilimo cha kisasa, viwanda vya nguo, na usindikaji wa mazao ya kilimo.
8. HITIMISHO
Tanzania si nchi masikini kwa sababu haina rasilimali; ni nchi iliyofanywa masikini kwa sababu ya matumizi mabaya ya rasilimali hizo, uongozi mbovu na rushwa . Taifa linahitaji uongozi wa maono, uzalendo wa kweli, na mipango ya maendeleo inayomgusa mwananchi wa kawaida.
Kama Rwanda na Botswana waliweza, nasi tunaweza. Lakini hatuwezi kuendelea kwa kutumia mfumo ule ule uliotufikisha hapa. Ni wakati wa kuchagua mwelekeo mpya: wa uwazi, uwajibikaji, na maendeleo jumuishi.
9. Orodha ya Rejea
1. Tanzania Investment Centre (TIC) – Investment Opportunities Reports
2. Tanzania Mining Commission – Annual Mining Performance Report
3. U.S. Geological Survey (USGS) – Minerals Yearbook: Tanzania
4. World Bank – Tanzania Economic Updates
5. Energy and Water Utilities Regulatory Authority (EWURA) – Annual Reports
6. Helium One Global Ltd – Project and Resource Estimates
7. Tanzania National Parks Authority (TANAPA) – Conservation and Tourism Statistics
8. World Travel and Tourism Council (WTTC) – Tanzania Country Profile
9. Ministry of Livestock and Fisheries – Blue Economy Policy Documents
10. FAO – Fisheries and Aquaculture Country Profiles: Tanzania
11. Institute of Marine Sciences (UDSM) – Research Publications
12. Tanzania Ports Authority (TPA) – Annual Port Performance Reports
13. National Bureau of Statistics (NBS) – Household Budget Surveys & Economic Indicators
14. United Nations Development Programme (UNDP) – Human Development Reports
15. Ministry of Finance and Planning – Budget Speeches & Public Debt Reports
16. Controller and Auditor General (CAG) – Annual Audit Reports
17. International Monetary Fund (IMF) – Tanzania Debt Sustainability Analysis
18. Transparency International – Corruption Perceptions Index
19. Afrobarometer – Public Opinion Reports: Tanzania
20. Legal and Human Rights Centre (LHRC) – Tanzania Human Rights Reports
21. Tanzania Extractive Industries Transparency Initiative (TEITI) – Contract and Revenue Data
22. OECD – Development Pathways: Malaysia, Rwanda, Botswana, Vietnam
23. UNCTAD – Investment Policy Reviews
24. World Bank Country Profiles – Rwanda, Botswana, Malaysia, Vietnam