Tanzania taifa liliopoteza mwelekeo,....!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania taifa liliopoteza mwelekeo,....!!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by THE DON KIBEDAI, Dec 7, 2011.

 1. T

  THE DON KIBEDAI Member

  #1
  Dec 7, 2011
  Joined: May 27, 2011
  Messages: 29
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  tanzania taifa ililopoteza mwelekeo, matumaini hayapo tena juu ya
  ​
  1;maisha bora,
  2;huduma za afya bora,
  3;elimu bora,
  4;miundombinu bora,
  5;nishati bora,
  6;unafuu wa gharama za maisha

  ni lini watanzania wenzangu tutachukua hatua dhidi wale waliolihujumu na wanaolihujumu taifa na kulipotezea mwelekeo,....???

  Ni lini watanzania wenzangu tutajua tunachotakiwa kukipigania na tukipiganie vipi,...???

  Ni lini watanzania tuta acha kuomba haki zetu na kuanza kuzidai haki zetu,....????

  Ni lini watanzania tutasimama kama taifa kwa masilahi ya taifa na kuamua mstakabari wa taifa letu bila kujali itikadi za vyama vyetu,dini zetu,tofauti za makabila yetu,...???

  "ukimwona kobe kainamaa ujue anatunga sheria","kimya kingi kina kishindo kikubwa"...methali hizi sizani kama zinaukweli kwa watanzania wenzangu kwani wengi wetu tumekuwa washabiki wa kisiasa bila kuweka masilahi ya taifa hili mbele,...

  Wengi wetu tumejawa na tamaa na ubinafsi ,...hii imetufanya tumeligawa taifa kwa wale wenye nacho na wasio nacho,...kwetu sisi ni bora leo na sio kesho,...

  Naomba kutoa rai kwa watanzania wenzangu, huu ni wakati wa kuungana kama taifa hasa katika kipindi hiki chenye changamoto na matatizo lukuki yanayotukabiri bila kusahau machakato wa kupata katiba mpya,...!!

  Tujaribu kuweka siasa kando kwenye maswala ya kitaifa yenye manufaa kwa wote, tumukemee yeyote yule mwenye nia mbaya dhidi ya taifa letu kwa kauli moja iliyoshiba umoja wetu kama taifa.

  Wewe ni moja wale watu milioni arobaini,..timiza wajibu wako kama mtanzania kwa kuvitendea haki vizazi vyetu vijavyo,...!!!
   
Loading...