Tanzania taabani kwa maradhi matano hatari

Expedito Mduda

JF-Expert Member
Sep 22, 2009
521
234
Umaskini, Ujinga, Maradhi, Udini na Ufisadi ni maradhi ambayo amini msiamini yanaisokomeza Tanzania na kuimaliza kabisa.

Tanzania imejaliwa raslimali nyingi sana lakini ni bado ina umaskini wa kufa mtu ukilinganisha na nchi hata ambazo hazina raslimali kama zile zinazopatikana katia nchi yetu. Jamani hi bila kumung'unya maneno, nani kazembea na kutufikisha hapa tulipo? Serikali ndio mdau mkubwa wa kuhakikisha wananchi wanaondokana na hali mbaya ya umaskini uliokithiri. Umaskini kwa upande mmoja huondoka kwa kutoa elimu bora kwa wananchi ili waweze kubuni miradi yao ambayo itawaondolea umaskini. Elimu inayotolewa Tanzania ni ya ajabu na kichekesho utafikiri wanaopanga wana visa na nchi yetu. Tanzania ni nchi ya wakulima. Leo hii mtoto anakaa maisha ya shule kwa miaka na miaka lakini hafundishwi elimu ya kilimo hata kidogo.

Hivi huyo mtoto aliyeanza shule toka akiwa na miaka miwili na huko shule hakuna elimu ya kilimo na leo ana miaka ishirini na mbili (22) unafikiri ataweza kulima kweli. Atazalisha nini. Elimu ya madaftarini aliyosoma huko shuleni eti Kinjekile Ngwale aalikuwa nani inaakisi chochote kitakachomsaidia mtoto huyo aweze kujitegemea kweli. Toka uhuru TANU na mtoto wake CCM ni vyama ambavyo vimeongoza serikali. Mimi nataka kujua kama si serikali ya vyama hivyo ndo imefikisha Watanzania hapa ni na nani sasa. Kwa ukweli uliopo sisi Watanzania tusiposimama na kusema kudanganywa tumechoka, basi umaskini wetu hautaisha kabisa.

Ujinga mwingi wa Watanzania unatokana na kuwa mfumo wa elimu si ule unaolenga kumkomboa Mtanzania kifikra hata kidogo. Angalia vijana waliomaliza kidato cha nne ambavyo bado hawawezi kabisa kujitegemea. Hawana lolote la kufanya kwa sababu elimu walioisoma darasani haikulenga kuwasaidia kujikomboa kimaisha katika mazingira yao. Pia hawa vijana hawana ile hali ya kujiamini na hawana uwezo wa hata kuchambua lipi linaweza kumsaidia katika maisha na lipi haliwezi kumsaidia. Angalia katika chaguzi mbalimbali. Watu hawachagui viongozi waadilifu bali huchagua tu ilimradi wametimiza wajibu wa kuchagua. Elimu ya uraia haijaingia vichwani mwao. Na madhara ya hilo hakuna mtu hajalionja.

Maradhi ilitangazwa kuwa ni adui wetu tangu uhuru. Leo hii bado maradhi anatutesa na wala hakuna matumaini lini tutamshinda. Angalia vifo vya akina mama wajawazito. Leo katika miaka ya sayansi na teknolojia wanaahidiwa bajaj eti za kuwapeleka hospitali na wenyewe wanapiga vigelegele. Hivi mama mjamzito anaweza kukaa kwenye bajaj na akafika hospitalini kilometa thelathini kupitia barabara za vijijini. Kweli hivi sisi Watanzania tumekosa nini. Kama watu tunaotegemea watusaidia kutatua matatizo makubwa ya nchi halafu wanakuja na ahadi za bajaj vijijini kusiko na barabara, basi Tanzania taabani.

Nchi yetu toka mwanzo mpaka sasa haina dini. Leo kuna watu wanashabikia serikali ijiingize kushughulikia mambo ya dini. Hivi hawa viongozi tulio wapa dhamana ya kuongoza nchi wanatupeleka wapi? Katika awamu ya kwanza hakuna suala la udini lililojitokeza na kutusumbua akili zetu. Awamu ya pili masuala ya udini yalijitokeza yakakemewa sana na yakapoa. Katika awamu ya tatu hakuna masuala ya udini yalijitokeza. Awamu ya nne yamekuja kwa kasi mno. Ukiangalia hapa ni nani wanaanzisha hawa masuala. Je, ni wananch au viongozi. Mimi binafsi nahisi viongozi ni chanzo cha kuibuka kwa udini. Na hawa viongozi huibua msuala ya udini ili wawezo kupata kile wanachotaka kupata toka kwa wananchi. Hii inafanana na kiongozi mmoja aliyeenda sehemu fulani ya wanafunzi akatangaza siasa zake hapo na wale wanafunzi baada ya kujua na kuwa mashabiki wazuri wa siasa maana wamefundishwa na huyu bwana mkubwa wakaamua kumchangia pesa ili zimsaidie katika pilika zake za siasa. Cha kushangaza baada ya kupata kile alichokuwa anakihitaji akarudi kwa wale wanafunzi kuwaambia wasijihusishe na mambo ya siasa. Kwa haraka ndicho kinachoendelea hata katika masuala ya dini. Mtu anaanzisha udini yeye mwenyewe ili asaidike kupata kile anachotaka apate. Baada ya kupata chake anageuka na kuwaambia wengine ndo wameanzisha udini.

Watu wamekuwa wezi na wala rushwa kuliko muda mwingine wowote ule. Kwa kuwa huko nyuma hapakuwa na ufisadi wa kiasi hiki, basi uongozi wa sasa umeshindwa kabisa kuwadhibiti mafisadi.
TANZANIA TAABANI.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom