Sijali
JF-Expert Member
- Sep 30, 2010
- 2,700
- 1,853
Kwanza acha niharakishe kusema, katika mambo mengi yanayohusu uongozi Tanzania, rais Magufuli amefanya vizuri sana. Hakuna mfano na awamu ya 4, ingawaje watu wanazungumzia kuikumbuka awamu hiyo.
La kushangaza ni kuwa katika hayo machache aliyokosea, ni mabaya mno kiasi cha kugubika mema yake. Na hasa la kushangaa Zaidi ni kuwa mengi katika haya mabaya hakuwa na haja kabisa ya kuyafanya, si kwa kudhamini kiti chake, si kwa kumletea sifa yeyote.
Sina haja ya kuyataja kwani Watanzania wote wanayajua. Haya yote yanahusu siasa za ndani.
Ila sasa rais wetu huyu anajitakia "maafa" kwa kuanzisha ugomvi usio na maana na jamii ya Kimataifa, na hasa hasa dhidi ya Madola makubwa yenye Satwa.
Moja ya sifa za mwanasiasa mahiri ni kujua namna gani ya "kuepuka shari" ingawaje anafanya hilo hilo lisilotakiwa. Ndiyo maana watu wengi wakainasibisha siasa na unafiki. Kwa sababu unaweza kabisa kufanya kile kile unachokitaka bila ya kuamsha hisia mbaya dhidi yako, kwa kubadilisha tu maneno mawili matatu katika msamiati unaoutumia.
Nakumbuka wakati Fulani nikiwa katika chumba cha habari cha shirika kubwa la habari tuliambiwa tusiandike "vikosi vya Israeli vimemwua kwa kificho kiongozi wa…) bali tuandike "Vikosi vya Israeli vimemlenga kwa kumwua kiongozi wa…)"
Pengine katika Kiswahili haidhihiri tofauti ya mawili hayo, lakini katika Kiingereza kuna tofauti kubwa sana kati ya "Israel forces have assassinated the leader of...)" na "have conducted a targeted killing against the leader of)" wale wajuao Kiingereza watafahamu. Ukitazama utaona umegeuza maneno mawili matatu tu, lakini kitendo ni kile kile. Lakini katika mfano wa kwanza, unaweza kuamsha maandamano na shutuma nyingi kutoka bodi za kimataifa, wakati katika wa pili watu wengi wataona huyo aliyeuawa amejitakia!
Na ndiyo hivyo mwanasiasa mahiri ajifunze mbinu hizi za kugeuza maneno.
Kwa ufupi, rais wetu inabidi aelezwe kuwa uwazi siku zote hausaidii na utaiweka Tanzania katika matatizo ya kujitakia.
Chukua mfano suala la watoto wa kike kukataliwa kurudi shule baada ya kuzaa. Dunia na "jamii iliyostaarabika" haikubali jambo hili hivi sasa. Katika miaka ya 40 na 50, hili lilikuwa jambo la kawaida kabisa.
Haikuwepo haja kuuambia ulimwengu mzima kuwa Tanzania haikubali jambo hilo. Ingeweza kuwa ni mwongozo tu uliowekwa shuleni. Kwa kufanya hivyo kungeiepushia Tanzania madhara ya "kubwata" hadi benki ya dunia imeinyima nchi shs. billioni 700 kutokana na kauli hiyo! Huu nauita upumbavu au kutokomaa kisiasa.
Ushoga: hata kama ni kweli kwa watu wengi katika jamii ya Tanzania hawakubali vitendo hivi…...lakini ni upumbavu wa kisiasa kwenda "Agora" (sokoni) na kipaaza sauti na kuitangazia dunia jambo hilo.
Labda uongozi wetu unadhania kujipiga kifua kusema wewe ndiye mwenye nchi na mwamuzi wa mambo ndiyo kunaonesha ushujaa na uzalendo……… hii ni dhana hatari ya kipumbavu. Kwa sababu Tanzania si kisiwa. Tanzania inazihitajia nchi nyingine kwa maendeleo yake na wala haijafika popote katika vigezo vya dunia.
Mapato yooote ya Tanzania kwa mwaka hayafikii hata nusu ya mapato ya shirika la Coca Cola, Amazon au Uber (iliyoanzishwa miaka 7 tu iliyopita!) Kwa kiasi hicho bado tuko nyuma!
Ikiwa nchi kama China, Iran, Urusi….zinaomba zikubalike katika mataifa ya magharibi, sembuse Tanzania?!