Tanzania Safari channel

K A B U R U

JF-Expert Member
Nov 24, 2011
644
1,000
Nawapongeza sana hawa TBC na wadau wengine kwa kuleta Channel hii. Binafsi nifuatilia hii channel kwa kutumia Startimes, sijapata tatizo la kuganda picha. Nawapongeza zaidi kwa kutokuweka matangazo ya kibiashara.

Ila kuna kitu nataka kuwashauri hawa wahusika,

CONTENT
Unapokuwa unaonesha maeneo ya ndani ya nchi mfano mji wa Dodoma, ukiacha kufanya mahojiano na wenyeji wazee wenye taarifa za kina kama historia ya eneo, wazawa, matukio ya kustaajabisha, mila na desturi basi unakuwa hujafanya kitu. Kumbuka wafanyakazi wengi wa Serikali wamehamia Dodoma, wanatakiwa wahamasishwe kuijua na kutalii ndani badala ya yake ile makala ilionesha eneo la mnadani, ikaenda pale Simba hill area D na mitaa miwili mitatu wakawa wamemealiza makala, hakuna jipya. Ukilinganisha na makala ya Dar es Salaam iliyofanywa na Heel Kneel Production kwa ufadhili wa Dar es Salaam City Concil ilikuwa na maelezo mengi na mazuri, picha zilizopigwa kwenye angels mbalimbali kiasi kwamba hata kama unaishi Dar lakini unakuwa huchoki kuangalia na kusikiliza. Kuna msemo unasema "No research, no right to speak" . Kuna wiki moja Clouds fm kupitia kipindi cha power breakfast walikuwa na wiki ya Mzizima. ilikuwa ni well researched presentation, mambo mengi sana tulikuwa hatujajui tulielimishwa na wale wazee waliokuwa wanawahoji, sasa hiyo ni audio media inaweza kumgusa mtu, hii audio visual inashindwa nini?

QUALITY
Kuna walengwa wa aina mbili, watalii wa ndani na wa nje. Tunatarajia ubora wa picha uwe wa kiwango kinachoridhisha, mfano badala ya kupiga lateral view ni vizuri kuwa na aerial view ili kupata muonekano mzuri hasa eneo linalowasilishwa linapokuwa ni pana sana. Hizi kamera za kubeba begani tuachane nazo maana kila mtu siku hizi simu yake ni camera anaweza kufanya hivyo, tumpe mtazamaji kitu kipya. Ukilinganisha na makala za National Geographic Channel, huwezi kuona sura za watu mara kwa mara, lakini kwetu huku muda mwingi unaona wanaonyesha sura za watu badala ya kile wanachokiwasilisha.

DIVERSITY
Nawapongeza waandaaji kwa kuwa wameweka mchanganyiko wa makala, kuna wanyama wa mbugani, mila na tamaduni, miji n.k. Nadhani kuna maeneo ambayo hayajapewa nafasi, ingawa inawezekana ni mimi ndio sijayaona, nayo ni mali kale na hadithi zake. Hao hao TBC wana kipindi kinaitwa "Zamadamu" maudhui ya kipindi hiki yanaweza kuwa sehemu ya channel hii.

FACILITATION
Katika ile hali ya kukuza utalii wa ndani, napendekeza Channel hii itumike kama njia ya kuwawezesha watanzania kuelewa kwa urahisi jinsi ya kufika kwenye maeneo ya utalii na gharama zake. Ukiona watanzania wachache wanatembelea huko, sababu kubwa ni ufahamu wa hatua kwa hatua mpaka kufika huko, gharama, nini cha kubeba, faida utakazopata n.k. Tafiti zinaonesha kuwa hata mabenki, hasa SME based yalianza kuwafikia watanzania wengi baada ya kutoka kwenye closed bank halls na kwenda mitaani na kufungua wakala huko huko mitaani.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom