Tanzania Redcross bado kwafukuta

Tanzania Redcross bado kwafukuta

Dadiz

Member
Joined
Jun 30, 2018
Posts
20
Reaction score
8
Wiki mbili zilizopita tuliandika waraka mfupi ambao ulilenga kufichua njama za baadhi ya watendaji na viongozi wetu wanaokesha kuhujumu chama chetu cha Redcross. Leo tunaandika tena kwa ufasaha zaidi na tutajikita katika maeneo sita kati ya maeneo 21 yaliyopo.

1. Hoja kuu inayotafuna chama chetu kwa sasa ni mnyukano wa kimaslahi. Kuna watendaji wanatumia fedha nyingi kuhakikisha mambo yao yanaendelea kufichwa ikiwemo kuhakikisha uchaguzi haufanyiki ili kuzuia maovu yao yasianikwe na uongozi ujao. Wanajua kuwa uongozi ujao unaweza kuvumilia huo uozo. Wanajua kabisa kuwa babu akiingia madarakan hatavumilia uzembe, wizi na ubadhirifu sababu ambayo iliwafanya wamchukie na kuamua kumwondoa mwaka 2015.

Wanatumia kila mbinu kumzuia ama kuhakikisha wanaahirisha uchaguzi ufanyike watakapokuwa tayari kumkabili. Sote tunajua kuwa Babu alikaa madarakani kwa miaka miwili tu (2013-2015) lakini cha moto walikiona. Aliisafisha nyumba mpaka unawezona sindano uvunguni. Wanajua yale mambo ya kukata kata majina kwa sasa hayawezekani tena mana baadhi yetu walitukata majina tulipogombea mikoani mwaka 2012 kwa uonevu na chuki binafsi.

2. Tunajua na wanaelewa kuwa katika uchaguzi wa mwaka huu baadhi ya wenyeviti wa mikoa hawana dalili za kupata ushindi. Kwa mfano Mwenyekiti wa mbeya hana tawi hata moja ambalo wanachama wamelipa ada huku mwenzake anayejiita “mwenye nguvu” huko Arusha amekalia kuti kavu kwa sababu nyingi. Sababu ya kwanza hana matawi kama mwenzake wa Mbeya, pili hakubaliki kwa wanachama wenzake anapingwa na tatu katiba mpya inataka mtu ili agombee mkoa awe mwenye elimu ya form of 4 jambo ambalo kwake ni mtihani mpya. Anachopanga ni kama alichofanya mwaka 2012 ambacho kwa leo hatutaelezea sana. Ila anajua mwaka huu lazima ang’oke kwahiyo aanze kuaga kabisa. Tunataka damu mpya mikoan. Hatutakubali Wenyeviti wenye miaka zaidi ya 60 Mikoani, lakini tunahitaji mtu mzima mwenye weledi ngazi ya Taifa ili alee vijana.

3. Jecha alikuwa Kaimu Rais kuanzia 2016 mpaka sasa. Ni moja ya watu dhaifu na wanafiki sana duniani. Dawa yake inachemka. Hatujasahau kuwa wakati Babu lao anafukuzwa urais mwaka 2015 yeye Jecha alimshauri aende Mahakamani lakini leo yeye ndio anashikilia azimio la 2013 walililoazimia ili kumsulubu Rugambwa kuwa mtu akipeleka chama mahakamani afukuzwe uanachama. Kwake Jecha madaraka ndio kipaumbele cha kwanza. Hata kwenye chama chake cha CUF huko Pemba mgogoro wake na wenzake ni madaraka. Hana utu wala urafiki. Kwa sasa mipango yake ni kugombea Urais au Makamu wa Rais wa Chama chetu ila anashau ufisadi wa jengo la Viva Tower alipopata kale kamgawo na ushahidi tunao wa maandishi alivyosaini na kiwango cha pesa alichochukua. Alivyo zwazwa anasainishwa pesa ya rushwa. Tutatoa tamko lake peke yake mana huu si wakati wa wezi kuendelea kudunda.

Baada ya kusoma alama za nyakati kuwa hawezi kushinda ameamua kubadili gia anakesha kusogeza mbele uchaguzi, anataka ufanyike oktoba 2020 akiamini atakuwa kapata hela ya uchaguzi ikiwa ni sehemu ya mgawo wake wa fedha anazopata kila uchaguzi mkuu unapofanyika ambayo chama chake cha CUF kinapata kutokea uarabuni. Hata hivyo ujinga wote huo bado anakwama kuutekeleza na hatofanikiwa kutokana na ukinzani mkali kutoka kwa Katibu Mkuu Ndg Kejo ambaye amesimamia kidete iwe jua iwe mvua lazima taratibu zizingatiwe na uchaguzi mkuu ufanyike mwaka huu kama ilivyopangwa. Hongera brother Kejo hakika wewe ni moja ya wazalendo wachach uliyebakia ndani ya Chama . Ni bahati mbaya tu kuwa Kejo hapati ushirikiano toka kwa NEC, Kamati ya mpito wala Kaimu Rais Jecha mana wote wana agenda za matumboni.

4) Kamati ya Mpito Dhaifu. Katika timu ya watu 10 wa Kamati ya mpito, ni watu wanne tu ambao hawana upande wala maslahi binafsi. Natamani leo iitwe NEC tuunde Kamati ya Mpito mpya iwe na watu makin kama Mwenyekii wa Kigoma, Kagera, Shinyanga, Morogoro, na Unguja. Sio hawa wachumia tumbo.

Kwa mfano, tangu katiba ipite Novemba 24, 2018 hawajaweza kufanya uelimishaji wa katiba mpya wala uhamasishaji wa ada mpya kwa kisingizio kuwa hakuna fedha. Cha kushangaza ni kuwa fedha za kupishana angani kwa watendaji mafisadi wanazo lakin za kueneza chama hawana.

Pili ni NEC ilipitisha azimio la ada iwe 1,000 kwa mwezi sawa na 12,000 kwa mwaka au 6,000 kwa miezi sita lakin leo badhi yao wakiongozwa na Jecha wamebadilika. Leo Care Committe wanakuja juu ili kuvuruga chama kwamba lazima mwanachama alipe ada ya mwaka yote sio ya mwezi tena wala miez sita. Huu ni uzwazwa na kukosa elimu! Vyama vyote nchin hakina hata kimoja kinachoforce mwanachama lazima alipe ada ya mwaka bali asiwe na madeni, kule SIMBA, YANGA, ROTARY CLUB, SCOUT, BASKTBALL, CUF MBAO FC, CHADEMA, CCM Hadi ACT kote hawana upuuzi huu. Ni aibu kubwa kwetu.

Kwa mara nyingine tunaona akili ya kipeke ya Kejo amefanya tafiti ya kina na ameona wanampoteza sasa amesimamia wanachama walipe ada yoyote hadi 6,000 lakini wasiwe na madeni. Si rahisi kupata watu wenye upeo wa kiwango hicho. Baya zaidi ni kwamba wao kupitia Halmashauri kuu Taifa ndio walipitisha viwango hivyo ili vikasimamiwe lakini ghafla ati Care taker Committee inajivisha jukumu la kutaka kupunguza katikati ya safari. Wanasahau Care Taker jukumu lao ni kusimamia maamuzi ya NEC sio kubadilisha. Kwamba mkitaka badili ada za uanachama au za fomu za kugombea uongozi sharti iitwe NEC nje ya hapo tutawaburuza mahakamani tena.

Zaidi Care Committee hiii imeibua jambo jipya kuwa kama mkoa hauna matawi 5 usifanye uchaguzi. Mana yake ni kwamba ikitokea mikoa ambayo ina matawi 5 haifiki 8 uchaguzi usogezwe mbele 2020 au 2021 au 2023 pale Mikoa yote itapotimizza Matawi hayo. Huu ni uzwazwa mwingine wa Jecha na jopo lake. Yani hawana aibu. Kila wafanyalo wanalenga mambo mawili moja ni kupata fedha ama kuendeleza udictator na kuua demokrasia kwenye chama(Nkurunzizaism)

Ikumbukwe katiba ya Redcross inasema uchaguzi ufanyike kila baada ya miaka 5 lakin tangu 2012 haujafanyika uchaguzi mwingine hadi leo. Hii si kwa bahati mbaya. Ni ukosefu wa democracy redcross. Wako madictator wachanga ndani ya Chama chetu ambao lazima wang’oke safari hii.

5) Mnyukano wa watendaji. Kwanza tunajua Menejiment imepasuka kila moja ana mtu wake mfukoni na wengine wanaendelea kutafakari. Ila tunajua wako watendaji watatu wakiongozwa na kijana mmoja ambaye katika siku za hivi karibuni amejitwalia nguvu kubwa ktk chama na tayari ameanza kupita pita mikoani kufanya siasa za uchaguzi. Tunamwonya aache Lasivyo tutamwanika na kila anachokifanya. Tunalo file lake la page 50 juu ya ufisadi alioufanya kuanzia aingie mpka sasa. Na tunajua also vyokuzwa huko alikotokea... Na tunajua kwasasa anachokitafuta ni nini. Atulie “kama Mungu alimwandikia atapata kwa muda wake” . Ila akiendelea atajukuta yuko uchi. Akumbuke watendaji hawaruhusiwi kushirki mambo ya siasa

6) Mwisho. Sisi vijana kutoka mikoa ya Arusha, Mwanza, Kagera Dar na Pwani ambao sasa idadi yetu imeongezeka hadi kufikia 16(baada ya wenzetu 5 kutoka Pwani na Kagera kuongezeka) hatuna ugomvi na mtu na hatutumwi na mtu. Tunawasihi viongozi wa NEC na na “Care taker Committee”wawe makin sana katika vikao vyao ambavyo tunajua vitakavyoketi kati ya tarehe 27 na 28. Watambue tumewapa dhamana hiyo kwa muda tu. Waweke mbele maslahi ya Chama chetu sio mambo yao. Waelewe kuwa tunafuatilia kwa ukaribu kikao chao na tutawataja wote kwa majina wenye lengo la kukwamisha cjama chetu kisisonge mbele. Wajue kuwa wakiazimia upuuzi tutajitokeza hadharani kuwapinga kwa majina. We are tired.

Aidha tunayo imani kubwa sana na Kamati ya uchaguzi kwamba itatenda haki maana imejaa wanasheria na wazee wenye busara na hekima wakiongozwa na Mzee Kalufya ambaye amekuwa mjumbe wa bodi kwa miaka zaidi ya 15, hawezi kubali ujinga wa aina yoyote. Kwa hilo hakika NEC inastahili pongezi mana iliona mbali kufuta utarartibu wa zamani wa kihuni wa kushugulikia watu bla sababu. Imani yetu kwa kamati ya Uchaguzi sio hawa kina Jecha.

Nchi nzima watu wanalipa ada na kuchukua fomu afu Jecha anaita Care Commiitee eti wakajadili kushusha ada na kusogeza uchaguzi mbele! Je mtawarudishia fedha ambao wameshalipa? Je ambao wamechukua fomu mtawapa hela zao? Mungu akunyime fedha sio akili na upeo!

Okay ngoja tuishie hapa kwa leo.

Ahsanteni sana, tukutane Habari Maelezo au Mahakama ya Kisutu baada ya Kikao cha Care Taker Committee Saa 4:00 asbuhi tarehe 28 au 29 Julai,2019.
 
Duh.
 
Back
Top Bottom