Tanzania ninayoitaka, Wewe unasemaje? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania ninayoitaka, Wewe unasemaje?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by platozoom, Feb 1, 2012.

 1. platozoom

  platozoom JF-Expert Member

  #1
  Feb 1, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 7,320
  Likes Received: 2,291
  Trophy Points: 280
  Jamii yeyote ile huwapata viongozi inaofanana nao. Wanaiba tunaiba,wanapenda sifa za kijinga nasi tunapenda sifa za kijinga,hatuyajadili matatizo yetu kwa ukamilifu na wao hawajadili matatizo yetu kwa uangalifu.

  Hawa viongozi hawatoki mbinguni au jehanam -hapana tunaishi nao na kuzungumza nao.Miaka ya 70 tunaambiwwa rushwa ilikuwa miongoni mwa kada ya chini ya watumishi....wakakua,wakapata madaraka makubwa kama watoto wao na wa majirani wao na wa jamii yao,leo hao ndio wala rushwa wakubwa.

  Na sasa walio katika nafasi za kawaida za utumishi iwe sekta ya umma au binafsi wanapindisha taratibu za kazi zao,wanatoa rushwa na kupokea. Unajua nini kitakachotokea? nao watakuwa na madaraka makubwa mzunguko utakuwa uleule.Tunahitaji kujichunguza kama taifa tujenge hoja za kurekebishana na kuonyana kwa hoja. Tujadili na kuichunguzu miongozo bora juu ya kujitawala na namna tutakavyowapata viongozi wetu ili pindi tutakapobadili uongozi wa taifa letu tusijute.

  Wale viongozi tunaowapenda wakipitisha mambo ya hovyo tuwaambie na tusikae kimya au kuwatetea kwa hoja za kishabiki (suala la posho ni mfano mzuri sana taarifa zinaonyesha wanaoziunga mkono bungeni ni wengi ikiwemo na wa vyama vya upinzani tunavyoviamini).

  Tafakari.
   
 2. Michael Pima

  Michael Pima Member

  #2
  Feb 2, 2012
  Joined: Dec 26, 2010
  Messages: 46
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Suluhisho la yote haya na matatizo ya umaskini ambayo huletwa na uchafu huu ni sheria kuwa msumeno haswaa.
   
 3. platozoom

  platozoom JF-Expert Member

  #3
  Feb 2, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 7,320
  Likes Received: 2,291
  Trophy Points: 280
  Tunazo sheria msumeno,lakini sheria ni kama gari halitembei bila dereva au remote
   
 4. Michael Pima

  Michael Pima Member

  #4
  Feb 6, 2012
  Joined: Dec 26, 2010
  Messages: 46
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Ni kweli tunazo sheria msumeno lakini sio sheria msumeno haswaa. Zilizopo hazina uhaba wa madereva ama remote, tatizo ni kwamba zinasukumwa kuelekea mbele na hazirudishwi nyuma kama ipasavyo kwa misumeno. Nani wa kuusukuma msumeno mbele na nyuma???
   
Loading...