CarolNdosi
Member
- Jul 16, 2015
- 45
- 505
Habari za Jumapili Bandugu. Kwa wale mlioshiriki kwenye Jumapili ya Matawi leo, baraka za mwenyezi Mungu ziwe nanyi na muwapendao.Nina imani kabisa haswa wale wa KKKT Jumapili hii itakua ya shauku sana baada ya WARAKA.
Hivi karibuni kumekua na matukio kadha wa kadha ambayo yamejaribu kukemewa na asasi zisizo za kiraia, taasisi mbali mbali, balozi na hata watu binafsi. Rejea barua yangu kwa Rais wetu Mpendwa Dr John Joseph Magufuli.
Kila mmoja amejaribu kuongea analoweza kwa kuzingatia haki na sheria za nchi na historia yetu kama Tanzania.
Leo naomba niwasilishe mawazo yangu; kuna hawa vijana wa mtandaoni siku hizi wanaotumia nguvu ya ziada kunyamazisha mawazo yoyote yanayokinzana NAO. Ni vijana ambao tumeona wakijaribu kwa hali na mali kwa madai ya kuweka taswira ya nchi sawa, kwa kupinga makala mbali mbali zinazoongelea matukio yanayotokea, kuleta maelezo yao na ‘conspiracy theories’ za matukio mbali mbali, saa nyingine kabla hata ya matamko ya mamlaka husika.
Kwa upande mwingine, wananihamasisha kuona jinsi gani mtu anaweza kupigania chama chake. Inatia moyo. Inanikumbusha kampeni ya Mahaba 2015.
Inavunja moyo lakini kuona kuna wengine wako tayari kuweka ‘uchama’ mbele ya maslahi ya taifa kama taifa. Kukataa kuwa nyeusi ni nyeusi na kujaribu kutuaminisha kuwa ni kijivu ni zaidi ya MAHABA, ni delusion.
Wengi wamekua wakitusema kuhusu ‘Uhuru wa Kujieleza’, ambayo kinadharia kabisa ni haki ya msingi ya kila Mtanzania.
Kwanini na mimi nisishiriki kutoa maoni yangu kwa yanayoendelea nchini? Cha kusikitisha zaidi ni kila utakapo toa maoni ambayo sijui hata wanatumia vigezo gani kuamua kuwa ‘haya hayafai’, utaona wengi tu wanakuja kukutahadharisha na KUKUTISHA -”dada nyama choma haitorudi tena ujue- dada si una watoto unalea mwenyewe angalia wasije wakakupoteza- dada angalia Nondo wamemfanya nini- dada unawatafuta watu wasiojulikana” etc etc etc.
Kuna vitisho uraiani vikihusisha mamlaka husika kuliko mamlaka husika yenyewe inavyovitoa — rejea tamko la ‘mtabaki vilema’. Ni mjumuisho wa vitisho tunavyotoa raia huku mitaani ambavyo vinafanya uamini kabisa kuna upotevu wa misingi kadhaa iliyokua inatulindia amani yetu.
Ndugu zangu, Tanzania ni yetu SOTE. Ni yangu, ni yako, ni ya yule ni ya wale. Hamna aliye na uchungu zaidi ya mwananchi wa kawaida ambaye hajawahi kuonja ‘priviledge’ ya aina yoyote kutokana na exposure au wadhifa.
Tukiona kuna uvunjifu na ukiukwaji wa haki za binadamu TUTAONGEA kwasababu ni haki yetu kikatiba. Tukiona kuna uminywaji wa demokrasia TUTAONGEA kwasababu ni haki yetu kikatiba.
Nafarijika kuona kesi mbali mbali zinafunguliwa kudai haki. Inatia moyo, ilibidi kukimbilia mahakama kwenye mambo kadha wa kadha toka mwanzo. Ingawa majibu mengine yanavunja moyo kama ya Kesi ya Mwenyekiti wa mtandao wa wanafunzi- Abdul Nondo aliyeshtakiwa kwa kosa la kujiteka mwenyewe na kunyimwa dhamana kwa kuhofia atatekwa akiachiwa.
Hamna utawala wowote uliofanikiwa kutawala kwa hofu, mara nyingi historia imeonyesha anguko lake huwa ni baya sana.
Hili kundi la watu lililojipa jukumu la kutia hofu wana nchi kila wanapo jaribu kuelezea maoni yao halitakuwepo milele. Bahati mbaya wengine tunaishi na nyie mtaani hivyo tunajua kabisa ‘motivation ya kuongea hivyo imetoka wapi’.
Binafsi naomba nisisitize tena, Hamna anayekinzana na dhana na azma ya maendeleo ya taifa letu. Hamna anayependa kuona taifa letu kila kukicha likiripotiwa kukiuka haki za binadamu, au uminywaji wa demokrasia. Na kama ni nchi yetu SOTE! Basi maoni ya wananchi, wa ngazi ZOTE ni valid! Ya MSINGI MNO.
Uongozi wowote huwa unatakiwa kujitathmini na kuangalia wapi wanaweza kukaa pamoja na wananchi waliowapa mamlaka ya kuongoza na kuwasikiliza.
Public outcry is just that, public outcry. Badala ya kutumia ‘vikosi’ na matamko kunyamazisha na kutoa vitisho kwa baadhi wanaojaribu kushirkiana na ‘watawala’ katika majadiliano na mawazo tofauti, ni vema tukajiuliza TATIZO LIKO WAPI??
Na je, is ‘silencing grievances’ the solution? Sio kwamba ndio inatengeneza vuguvugu zaidi?
Last week nilikua kwenye shirika moja la kimaendeleo wakaniuliza kama sidhani kama tulinyimwa uwanja mwaka jana leaders kufanya nyama choma kwasababu ya maoni yangu kuhusu ajenda mbali mbali za nchi. Nilisikitika mno, MNO. Aliyeniuliza alikua ni mtanzania mwenzangu lakini alitumia kiingereza hivyo hata wazungu walio kuwepo walisikia. Sikutaka wasikie kuwa hili linawezekana hata sumuni. Mimi sitaki kuamini kama linawezekana sababu itakua ni ukiukwaji wa hali ya juu na ugandamizaji uliotukuka ambao nakataa kuwa nchi yetu imefika huko. Yaani ukomoe ajira na kipato cha watu zaidi ya 500 na kusema ni kwasababu ‘Carol anaongea siasa’ Wallahi nisingependa kuamini kuna watu wenye roho ya shetani kiasi hiki ingawa ndio wanavyojaribu kuniaminisha.
Kuna mengi yanafanyika ambayo yangeweza kututia moyo katika safari yetu kama taifa lakini yamezidiwa na haya mengine YANAYOTISHA. Juzi nimeona pia Serikali imetangaza kuanzishwa kwa ‘Qualifying Test Centers’ ambazo hata waathirika wa mimba za utotoni wanaweza kuendelea na masomo. Nafarijika sababu naona kabisa MNATUSIKIA na mnajaribu kutekeleza. Niwapongeze wenzangu wa [HASHTAG]#ArudiShule[/HASHTAG] na niwasihi tuendelee. Hili limenipa moyo zaidi kusimamia ujenzi wa Mamaendeleo Vocational Academy ya waathirika wa mimba za utotoni maana zaidi ya 95% wanaoacha hawamudu ada za hizi QT centers wala VETA. Tunaendelea kushirikiana kuhakikisha hatumuachi mtu yoyote nyuma kama taifa.
Naamini vingine vinaweza kuwa hivi hivi, au vizuri zaidi kama kwa mfano tukitekeleza na kupata ufumbuzi wa maswala mbali mbali yaliyo jadiliwa kwenye kikao cha baraza la wafanyabiashara TNBC na rais wetu mpendwa Dr John Joseph Pombe Magufuli. Na kila siku anarudia kuwa ‘sidhani kama niliowachagua wananielewa’, inawezekana kabisa ukizingatia matamko ya baadhi ya viongozi. Wengi huwa tunabaki na bumbuazi, na unaishia kusema ‘ haiwezekana lazima ana backing kutoka juu’. Mkutano ule ingawa ulikutanisha wafanyabiashara wakubwa kwa mujibu wa uanachama na mualiko uliotolewa, naamini kabisa ‘approach’ ilitokana na mshinikizo wa umma kuhusu hali ya uchumi na kushuka kwa mzunguko wa fedha.
Tumtafute mchawi ni nani, na naomba tuwe na open mind ya kujua kabisa sio kila mtu ni adui yenu. Nchi ni yetu SOTE, na niliwahi kusema kila mmoja anajaribu kufanya analoweza kwa nafasi yake kusukuma gurudumu la maendeleo.
Tanzania ni yako, ni yangu, ni YETU. Kama ilivyokua ya Nyerere, ya Mwinyi, Ya Mkapa, Ya Kikwete. Get it? Na kama kweli ni ‘utetezi wa wanyonge’ basi turudi mezani tukachore tena maana wanyonge hawatetewi hivi.