Sijawahi kusikia nchi yoyote Dunia hii ikitaka kuandika Katiba mpya bila ya kuwa na political crisis yoyote ile, lakini nasikia kila siku watu hapa bongo tena wanaojiita wasomi wakidai Katiba mpya, yaani tutumie mabilioni ya fedha kuandika Katiba mpya wakati hakuna crisis yoyote ile nchini, hili halijawahi kutokea popote pale dunia hii, bali kinachofanyika ni nchi kufanya marekebisho ya Katiba iliyopo na siyo kuandika mpya.
Kudai Katiba mpya Tanzania ni sawa na kusubiri kumpata demu ambaye hakupendi, utasubiri miaka hata 50 haitatokea akaja kukubali.