Ngamanya Kitangalala
JF-Expert Member
- Sep 24, 2012
- 501
- 1,214
Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na wawekezaji inatarajiwa kuanza kutekeleza miradi miwili mikubwa kabisa ya kimkakati( Strategic projects) katika ukuaji wa uchumi wetu
Kwanza, ni mradi wa kuchakata gas asilia, Liquefied Natural Gas( LNG) plant katika mkoa wa Lindi, mradi huu unatekelezwa kwa pamoja kati ya TPDC kwa upande wa serikali ya Tanzania, kwa kushirikiana na makampuni makubwa ya mafuta na gas hapa duniani, yakiongozwa na Equinor ya Norway, Royal Dutch Shell, Exxon Mobil na Ophir Energy, Tanzania inakadiriwa kuwa na hifadhi ya gas( Gas reserve) yenye ujazo wa cubic feet 57.54 milioni
Mradi huu mkubwa kabisa kuwahi kutokea katika nchi za Afrika mashariki, wenye thamani ya $30 billion unatarajiwa kuanza kutekelezwa mwaka 2022 na kukamilika mwaka 2028, kukamilika kwa mradi huu, inatarajiwa itaongeza ukuaji wa uchumi wetu kutoka 7% ya sasa mpaka 9% kwa mwaka
Mradi mwingine, ni mradi wa ujenzi wa kiwanda kikubwa cha kutengeneza mbolea katika mkoa wa Pwani, mradi huo wenye thamani ya $1.9 billion, utatekelezwa kwa pamoja kati ya TPDC kwa upande wa Tanzania na makampuni ya Ferrostaal ya Ujerumani, Haldor Topsoee ya Denmark na Fauji Fertilizer Company kutoka Pakistan, mradi unatarajiwa kuanza kutekelezwa mwaka 2021 na kukamilika mwaka 2024
Kiwanda hicho ndio kitakuwa kiwanda kikubwa kabisa cha kutengeneza mbolea katika ukanda huu wa Afrika Mashariki na kati
Kukamilika kwa kiwanda hiki, kutasababisha hupatikanaji wa uhakika wa mbolea, na kitasaidia kushusha bei ya mbolea na kuongeza tija kwa wakulima wetu, hasa ukizingatia kilimo kimeajiri zaidi ya 75% ya watanzania na ndio sekta inayoongoza katika kuchangia kwenye pato ghafi la taifa( GDP) 29%
Binafsi napenda kuchukua fursa hii, kuipongeza sana serikali ya awamu ya tano, chini ya uongozi wa mheshimiwa Rais wetu Dr John Pombe Joseph Magufuli,kwa jitihada kubwa wanazochukua katika kukuza uchumi wetu na maisha ya watanzania wote kwa ujumla 👏🏿👏🏿👏🏿👏🏿👏🏿👏🏿👏🏿
Mungu ibaraki Tanzania