MsemajiUkweli
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 13,171
- 23,991
Neno demokrasia ni neno ambalo kila kukicha linakosa maana yake halisi!
Neno Demokrasia kwa sasa limekuwa kama lungu linalotumiwa na Mabeberu wa nchi za Magharibi katika kutimiza malengo yao na sio kutimiza malengo ya nchi wahusika.
Kwa sasa tunaambiwa Tanzania imeshindwa kutimiza matakwa ya kidemokrasia katika Uchaguzi Mkuu 2015 mpaka Marekani ameamua kukata misaada yake kwa Tanzania.
Mimi sina tatizo na uamuzi wa Marekani kwa sababu pesa ni yao na wanaweza kuamua kuitumia wapendavyo, tatizo langu ni sababu wanayotoa katika kusitisha misaada kwa Tanzania. Marekani wanataka kutuaminisha kuwa maamuzi yao yamefanyika based only kwenye misingi ya demokrasia ambayo wanadai lazima iwe inclusive and representative.
Swali la kujiuliza, hivi Tanzania na Misri, nani mwenye demokrasia ambayo ni inclusive and representative?
Kuanzia mwaka 1948 mpaka 2015, Marekani imetoa msaada unaokadiriwa kuwa $76 billion kwa serikali ya Misri. Kipindi chote cha utawala wa Muhammad Hosni El Sayed Mubarak kuanzia mwaka 1981 mpaka 2011, Marekani alikuwa anaongoza kwa kutoa misaada kwenye utawala wake pamoja na uwepo wa ukandamizaji wa kile Marekani anakiita demokrasia.
Mwaka 2013, aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la Misri, Jenerali Abdel Fattah Al-Sisi ambaye kwa sasa ni Rais alipindua serikali ya Mohamed Morsi ambayo ilichaguliwa na wananchi wa Misri katika Uchaguzi ambao ulikuwa huru na haki. Pamoja na Mapinduzi yaliyofanyika Misri, hatukuwahi kusikia Marekani akiinyima misaada kwa sababu ya kusigina demokrasia.
Hata Uchaguzi uliofanyika baada ya Jenerali Fattah Al-Sisi kufanya mapinduzi ya kijeshi ambapo katika uchaguzi huo alipata ushindi wa asilimia zaidi ya 96 wakati inafahamika uchaguzi huo haukuwa huru na haki lakini serikali ya Marekani iliutambua na kumkaribisha Rais Field Marshall Abdel Fattah Al-Sisi kukutana na Rais Obama kwenye Ikulu ya Marekani.
Kwa sasa Misri ni police state kitu ambacho ni kinyume na maana ya neno demokrasia katika definition ya Marekani.
Katika mwaka wa fedha wa 2017, Rais Obama ameomba kwenye Congress kiasi cha $1.3 billion kama msaada kwa Misri katika nyanja za kijeshi na pia ameomba kiasi cha $150 million kama msaada wa kiuchumi.
Kwa kutumia vigezo vya Marekani, nani mwenye demokrasia kati ya Tanzania na Misri au kuna masuala mengine yamejificha nyuma ya pazia la geopolitical game.