Michael Chairman
JF-Expert Member
- Apr 11, 2015
- 922
- 583
Dunia inakaliwa na binadamu zaidi ya bilioni saba duniani kote , dunia hii pamoja na wakazi hao inazo zaidi ya mbegu za mazao bora 80,000 ambazo zote hizi ni kwa ajili ya chakula hata hivyo si zaidi ya 8,000 ya mbegu ambayo imekwisha kutumika ni mimea isiyozidi 20 tu ndiyo inayotegemewa kutoa tisa ya kumi ya chakula kwa ulimwengu wote huu.
Zaidi ya watu milioni kumi duniani kote huenda vitandani kwao usiku wakiwa na njaa na mamilioni ya watu duniani hufa kwa njaa kila mwaka. hali hii imelata utata na hata kuwachanganya wakazi wa dunia hii lakini pamoja na hayo imekuja kukugundulika kuwa duniani na kwenye nchi yangu yaTanzania hakuna njaa , wengi watauliza kama hakuna njaa kuna nini sasa? majibu ya swali hilo ni kuwa kilichopo duniani na Tanzania kwa ujumla kuhusiana na NJAA ni.....
UMASKINI , wengi wa wakazi wa dunia hii na Tanzania kwa ujumla ni maskini ( ama kwa lugha nyepesi wanatatizo la UCHUMI) hali inayowapelekea kushindwa kununua chakula kilichopo kwa mfano leo kibarua wa kitanzania anayefanya kazi ya kumwaga zege anapokea kwa kutwa Tsh 3000/= fedha hii haiwezi kununua kitini cha mahindi kwa ajili ya chakula cha kutosha kwenye familia ya watu saba.
Vyakula vipo vingi na vyakutosha, Shirika la umoja wa mataifa la chakula linasema kuna chakula kingi sana ambacho kinaweza kuwalisha watu wa dunia nzima zaidi ya mara tatu , kwahivyo tatizo la uchumi au umaskini uliokithili hauwezeshi watanzania kuweza kumudu kununua chakula kwa ajili ya familia zao, ni watanzania wengi hasa wafanyakazi (vibarua kama mimi) wanashinda njaa mchana kutwa wakitafuta mkate wa kupeleka kwenye jamii zao kwani wakisema wapite kwa mama muuza kununua chakula bajeti ya familia inaharibika na kupelekea watanzania kulala njaa.Tatizo kwa kiasi kikubwa limechangia matatizo yafuatayo....
Uzalishaji kidogo wa chakula kutoka mashambani;
kutokana na watanzania wengi kutokuwa na uchumi imara hali hii imepelekea kufanya uwekezaji kidogo sana kwenye kilimo na kusababisha kutoa mavuno machache mengi ya mazao hufia shambani aidha kwa sababu ya wadudu , uangalizi mbovu , kukosa elimu ya upandaji sahihi, mbegu mbovu , kukosa mbolea n.k , yote haya yanachangiwa kwa kiasi kikubwa na hali mbaya ya maisha ya watanzania au wakulima ambao kama watawekeza nguvu zao tu kwenye kilimo familia haitakwenda hospital , haitakwenda shule n.k ,
Tanzania ni miongoni mwa maeneo yalipochimbwa maeneo ya kuhifadhia maji ya Mwenyezi Mungu yaani maziwa , mito , hata bahari ni aibu kutokutaka kutumia ubunifu huu wa mwenyezi Mungu hata kwa kuendeleza kilimo cha umwagiliaji ambacho kwa dunia ya leo ndiyo kilimo madhubuti cha kufukuza njaa na kuleta utajiri utokanao na mazao.
Tatizo la pili linaloleta matatizo ya njaa ni usambazaji wa chakula,
ambalo nalo limesababishwa na tatizo namba moja ,leo utashuhudia kuna maeneo yanacho chakula cha kutosha tu lakini hakuna miundombinu ya kufanikisha chakula hicho kufika maeneo ambayo yana uhaba wa chakula ama yana ukame wa chakula hakuna barabara , hakuna mawasiliano , hakuna kila kitu bali kuna chakula tu, tatizo hili ndilo linazikumba nchi nyingi duniani.
Tatizo la tatu chakula kuharibika au uharibifu wa chakula,
kuna maeneo mengi sana hapa Tanzania watu wake hawajui kuhifadhi chakula , toka wanapoanza kuvuna mpaka wanapoweka kwenye maghala chakula kingi kinagaribika kwa kuanguka chini , kuuoza na kuliwa na wadudu waharibifu wa chakula , leo utakuta jamii moja inatumia kiasi kikubwa cha chakula kwa ajili ya kupika pombe kama mbege , wanzuki, number one , kindi, n.k hii yote ni kuharibu chakula , na vilevile utakuta familia moja inapika chakula bila kufanya mahesabu ya watu wangapi watakula na watakula kiasi gani cha chakula leo utapita majalalani utakuta vyakula vingi vimetupwa tu haya nayo ni matumizi mabaya ya chakula , nitoe pongezi kwa kampuni bunifu zinazoleta njia bora za uhifadhi wa mazao kama PICCS.
kwa kiasi kikubwa haya ndiyo baadhi ya mambo yanayochangia ukosefu wa chakula na kuleta njaa.
my take tuboreshe uchumi wa wanainchi hakuna baa la njaa