SoC04 Tanzania Mpya, Mtizamo Mpya na Raia wenye Furaha

Tanzania Tuitakayo competition threads

Edson Eagle

Member
Apr 20, 2024
29
11
Kuna ule msemo wa kwamba "penye nia pana njia" Tanzania yenye viongozi wenye mtizamo na matarajio makubwa wakitia nia katika haya yafuatayo basi nchi yetu itazidi kupiga hatua kubwa.

1. Serikali iboreshe nyanja zote za usafirishaji wa bidhaa, malighafi na watu katika maeneo mbimbali ili kuongeza kasi ya uzalishaji na utendaji kazi kwaajiri ya kuijenga Tanzania yenye maendeleo makubwa. Miongoni mwa nyanja hizo ni pamoja na viwanja vya ndege, treni za mwendo kasi pamoja na barabara katika maeneo mbalimbali nchini hii itachochea pia katika suala la ajira na uwekezaji.

Screenshot_20240512-104821.png

2. Kuhakikisha mtaala mpya katika elimu unaandaliwa mazingira rafiki, na kuleta manufaa makubwa, kwa mfano elimu ujuzi, serikali ihakikishe shule zinakuwa na madarasa yenye sifa zote na vifaa vya fani husika bila kusahau walimu wenye ujuzi na ubunifu wa fani mbalimbali kwaajiri yakuwajenga wanafunzi katika ubora mkubwa kwa vitendo na sio kwa nadharia ili badae wanapohitimu waleta mabadiriko chanya na makubwa nchini kwa kuwajengea wahitimu uwezo wa kujiajiri nakutatua changamoto mbalimbali ktk jamii. Tutoke kuleee kwa kumaliza kidato cha nne halafu unajua hesabu za kutafta umri wa watu usiowajua.
Screenshot_20240512-104650.png


3. Serikali iweke mazingira rafiki yatakayo wafanya wasomi na watu mbalimbali nchini kuweza kukutana na watu wa mataifa mengine duniani katika maswala ya elimu, siasa, afya, biashara, uchumi na viwanda. Lengo nikuwafanya wawe na mawazo na fikira mpya kutoka nchi zingine zilizoendelea ili wajue wapi waboreshe nakuifanya Tanzania iwe na maendereo makubwa. Mazingira hayo ni pamoja na
a. Kujenga masoko makubwa na mazuri ya biashara.
b. Kujenga vyuo vikubwa na vyenye hadhi ya kimataifa, n.k

Screenshot_20240512-105122.png
Screenshot_20240512-105122.png


4. Kuhakikisha katika sekta ya utalii miundombinu pamoja na mazingira yawe yenye kuvutia ikiwa ni pamoja na kujenga hoteli nzuri zenye hadhi ya kitalii nakufanya matangazo mbalimbali kuhusu utaliiwetu katika vyombo vya habari . Lakini pia kuweka wafanyakazi wenye ubunifu na taaluma mbalimbali za mataifa ya kigeni kwa mfano:-
a. Lugha za kigeni.
b. Vyakula vya kigeni.
c. Mavazi ya kigeni.

lengo nikuwavutia watalii kutoka sehemu mbalimbali za dunia, hii italifanya taifa kuwa na fedha za kigeni nakuinua uchumi wa nchi.

Screenshot_20240512-104317.png


5. Vyombo vya habari vyenye uhuru usiovuka mipaka. Serikali ihakikishe uhuru na usalama wa vyombo vya habari na waandishi wa habari kwa ujumla kwa kuzingatia sheria, kanuni na miongozo ya ukusanyaji, uandikaji na utoaji wa habari pasipo kuvuka mipaka wala kukiuka haki za binadamu. Lakini pia kuwa na utaratatibu rafiki utakaowafanya waandishi wa habari kutambulika ktk jamii kwa urahisi. Na mwisho waendeshe vipindi mbalimbali vyenye mtizamo chanya nakuchochea maendeleo ya jamii na si-vinginevyo.

Screenshot_20240512-150039.png


6. Kuchochea uzarishaji wa bidhaa bora na zenye kukubarika kitaifa na kimataifa ili kuweka ushindani wa kibiashara ndani na nje ya nchi ya Tanzania. Katika suala zima la uzalishaji wa bidhaa bora serikali ihakikishe kunakuwa na viwanda vikubwa vyenye teknolojia ya kisasa pamoja na wafanya kazi wenye ujuzi mkubwa katika kubuni bidhaa bora. Hii italifanya taifa kwanza kutumia bidhaa zake za ndani pili itachangia kukuza ushindani wa kibiashara lakini pia kufanya bidhaa za Tanzania ziweze kuuzika hata katika mataifa mengine duniani na hili linawezekana kabisa.

MWISHO: penye nia pana njia kama serikali itatia nia katika mambo hayo italeta maendeleo makubwa pamoja nakufungua nafasi za ajira ndani ya nchi lakini pia kutengeneza soko la ajira kwa Watanzania kuajiriwa nje ya nchi.
 

Attachments

  • Screenshot_20240512-150013.png
    Screenshot_20240512-150013.png
    685 KB · Views: 2
Sawa, sawia
Wapanue bongo kwa kuangalia nchi nyingine zinafanyeje.... na point hizi ulizosema ni muhimu kwa Tz tuitakayo
...."kuwajengea wahitimu uwezo wa kujiajiri nakutatua changamoto mbalimbali ktk jamii......waandishi wa habari kutambulika ktk jamii kwa urahisi. Na mwisho waendeshe vipindi mbalimbali vyenye mtizamo chanya nakuchochea maendeleo ya jamii na si-vinginevyo"..
 
Uhakika kabisa🤝
Sawa, sawia
Wapanue bongo kwa kuangalia nchi nyingine zinafanyeje.... na point hizi ulizosema ni muhimu kwa Tz tuitakayo
...."kuwajengea wahitimu uwezo wa kujiajiri nakutatua changamoto mbalimbali ktk jamii......waandishi wa habari kutambulika ktk jamii kwa urahisi. Na mwisho waendeshe vipindi mbalimbali vyenye mtizamo chanya nakuchochea maendeleo ya jamii na si-vinginevyo"..
 
Back
Top Bottom