Mfikirishi
JF-Expert Member
- Jan 16, 2012
- 10,405
- 12,096
Wakuu!
Nimekuwa nikifuatilia kwa karibu matukio yanayotokea nchini na nimebaini kuwa ni jambo la muda tu ili tuifikie Tanzania yenye maendeleo; nchi yenye uchumi wa kati barani Afrika. Imetuchukua muda mrefu kufika huko kwa sababu ya uelewa duni wa wananchi na fikra potofu za watawala kuwa maendeleo yetu yataletwa na misaada toka kwa wajomba!
Kwa muda mrefu sasa tulikuwa tumesinzia tukitegenea IMF, WB na wahisani watuamshe! Rasilimali tunazo za kutosha angani, juu ya ardhi, ndani ya maji na chini ya ardhi! Napata faraja ninapowaona wananchi wengi wanakuza uelewa wao kuhusu utajiri wa nchi yao! Pamoja na watawala kufanya kila aina ya hila ili tu wananchi wasijue utajiri wa nchi yao lakini wengi wanazidi kufunguka macho na masikio! Ukisikia watu wanavyojenga hoja kuanzia kwenye vijiwe vya kahawa kwa haraka unagundua kuwa Tanzania ya sasa si ile ya 1987!
Nadiriki kukiri kuwa ipo siku na haipo mbali sana...ipo siku ambayo watanzania kwa umoja wao bila kujali tofauti zao, bila kujali wanakotoka, bila kujali hali ya hewa, bila kujali gharama wanayoingia kwa sasa na bila kujali muda wala nguvu zao... kwa wingi wao wataungana na kufanya maamuzi Hiyo siku imezuiliwa sana kwa mabavu, hoja muflisi, hadaa za hapa na pale! Lakini kwa sasa hiyo siku imekaribia na hakuna wa kuizuia!
Lakini kufika huko tunahitaji kuunganisha nguvu zetu na kuwaelimisha wananchi hasa wa vijijini! Napongeza juhudi za Kinana na timu yao wanaozunguka kuwaelimisha wananchi kuhusu udhaifu wa Serikali yao na utajiri wa nchi yao! Napongeza harakati za UKAWA kuimarisha juhudi zao za kuwafikia wananchi wakiwa wanaongea lugha moja! Upinzani umefanya mengi kutufikisha hapa tulipo!
Tunategemea muungano wa UKAWA utakuwa chachu ya kutufikisha kwenye Tanzania Mpya! Ili tufike huko tunahitaji kusema HAPANA KWA KATIBA PENDEKEZWA! Mchakato wa Katiba mpaka sasa umewasaidia wananchi kujua maadui zao! Kwa sasa ni rahisi sana kufikisha ujumbe na ukaeleweka vema!