Tanzania: Maraisi waliotawala na sehemu ya sifa zao | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania: Maraisi waliotawala na sehemu ya sifa zao

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MAGEUZI KWELI, Mar 13, 2012.

 1. MAGEUZI KWELI

  MAGEUZI KWELI JF-Expert Member

  #1
  Mar 13, 2012
  Joined: Jul 16, 2011
  Messages: 1,943
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 145
  Nimeona tuangalie tulipotoka na tulipo, na kuangalia japo juu juu sifa za Marais walioitawala tanzania na ni nini walichokiacha kwenye fikra za watanzania na nini cha kujivunia kwa utawala wao.
  Kama kuna pongezi au la? Tukumbuke tawala zote ni chini ya Ilani ya CCM.

  1> Mwl J.K Nyerere - Alikuwa rais wa kwanza Tanzania, Aliweza kuifanya Nchi kuwa moja hasa kuondoa madoa ya ukabila,
  Hakuweza kuwafungua sana akili watanzania japo tulikuwa nyuma sana kimaendele, lakini utandawazi ulikuwa nadhani mwiko, na kama si kulazimishia, Computer alikuwa hajui.
  Siasa ya ujamaa ilikuwa ni sera yake, lakini hakuwaandaa watanzania katika kuendeleza sera hiyo ambayo ilisaidia sana Vietnam wakawa atleast na mafanikio Fulani.
  Wahindi walitona wajinga sana kwa taifa hili na walikuja na upuuzi wao kutuokota watanzania baada ya kuona ajali zinakuwa nyingi sababu ya barabara mbuvu, walileta kitu kiitwacho OKO.Radio zilitangaza live kwenye maonyesho na msumari ukitoboa tyre then msumari unatoka wenyewe.upuuzi mtupu kwa watanzania
  > Nywele za Rasta na nguo za mitumba na Television na mabank toka nje ilikuwa marufuku.

  2> Ally H Mwinyi: Mzee wa Ruksa, Aliachilia Biashara huria sana na japo zilikuja kwa kasi, Watanzania walijua nini tulistahili na kwa nini hatukuwa nacho.
  Alikuwa na kazi kubwa kuwacontrol washauri wake na vijikashfa vingi viliibuka vya kuhujumu uchumi wa nchi ikiwa ni pamoja na pembe za Ndovu kukamatwa Airport, na Ngorongoro iliponea Chupuchupu kuliwa kama njugu.
  TV tuliziita Video. kila kitu Ruksa.

  3> Benjamen Mkapa: Mzee wetu alipambana sana na mifumko ya bei ikiwa ni pamoja na kuboresha njia za uchumi, speed ya mafanikio ukilinganisha na utawala wake kulikuwa na tofauti kubwa sana, Khasha za mabilioni ya pesa kama Mil 900 za mrema na mengine ziliibuka.Mawaziri kama Idd Simba kujiuzulu kwa Khashfa za mamilion. nk
  Majambazi waliongezeka ndani ya taifa hili na kuifanya nchi isiwe mahali salama kabisa.
  BOT ilichakachuliwa sana kupitia Epa, na Viongozi walijikusanyia mali pale walipoweza,
  Watanzania walikula majani Ndege ya rais ikanunuliwa, Rada Chenji bado inadaiwa mpaka leo baada ya kuinunua kwa bei isiyo ya kawaida.

  4> Jakaya Kikwete :Amepokea kijiti toka kwa Mkapa,ARI MPYA NGUVU MPYA NA KAZI MPYA Kweli alipambana na mizizi yote iliyokuwa imeshikilia ujambazi nchini na sasa umepungua sana.
  Vita ya mafisadi ameweza kupambana nayo juu na hakuna hukumu iliyotolewa mpaka sasa kwa mafisadi,
  Waziri mkuu aliachia ngazi kwa kashfa ya ufisadi na Vijisent viliibuliwa benk za ughaibuni.
  Ameweza kuongeza njia za mawasiliano na kiasi jamii inaona kazi inayofanyika chini ya utawala wake.
  Migomo imekuwa ya hali ya juu kwa taasisi nyingi kudai maslahi yao na wakati mwingine imefanikiwa ikiwa ni baada ya kero na usumbufu kwa jamii.
  Ni raisi asiyekurupuka kutoa maamuzi japo ni magumu lakini yenye maslahi kwa taifa.
  Mishahara ya wafanyakazi imeongezeka ila haziendani na gharama za maisha kwa sasa
  FALSAFA YA TUMESUBUTU, TUMEWEZA NA TUNASONGA MBELE imekuwa na kioo kisicho na taswira halisi ya kinachoonekana kwa taifa hili kwa sasa.
   
Loading...