Tanzania loans society

Tanzania loans society

PRINCE GEORGE

New Member
Joined
Jan 11, 2012
Posts
4
Reaction score
0
Jamani kuna hii (TANZANIA LOANS SOCIETY) naomba kujua ni vipi nitaweza kuifikia na nikihitaji kupata fomu ili niweze kuupata huo mkopo,plz naomba msaada wenu kama mtaweza kunia na link yake itakuwa pouwa sana
 
Jamani kuna hii (TANZANIA LOANS SOCIETY) naomba kujua ni vipi nitaweza kuifikia na nikihitaji kupata fomu ili niweze kuupata huo mkopo,plz naomba msaada wenu kama mtaweza kunia na link yake itakuwa pouwa sana

Hao ni matapeli
 
Tanzania Loans Society ni tawi zawa la Shirika kubwa nchini marekani liitwalo Advolticies Power Loans Society (APL Society) linalo'ongozwa na Rais Barack Obama. Tanzania Loans Society ni tawi ambalo limeanzishwa mwaka 2012 kwa dhumuni la kutaka kuwasaidia watanzania ambao wanahali duni (masikini) kwa kumuwezesha kumpatia kila mtanzania mkopo wa fedha na zawadi ya Tshs.300,000 bure kwa kila mtanzania atakaejiunga na kua mwanachama wa Tawi hili.

Tawi hili lilianzishwa nchini Tanzania baada ya Rais wa Jamhuri wa muungano wa Tanzania alipokua katika ziara yake nchini marekani alipata fursa ya kuonana na Rais Barack Obama ndipo alipopewa muongozo na mchanganuo wa shirika la kuwasaidia wamarekani (APL Society) wasiokua na uwezo wa kifedha. Rais Barack Obama alikua na moyo thabit wa kuonesha kujali na akawa tayari kumsaidia Rais Jakaya Kikwete dhidi ya wananchi wake masikini akamshauri kikwete afungue tawi dogo ambalo litakua ni sehemu moja wapo ya shirika la APL SOCIETY ili kuwasaidia watanzania kupata fedha za mikopo.

Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr. Jakaya Mrisho kikwete alikubaliana na shauri hilo la Rais Barack Obama na kukubali kuanzisha tawi zawa la APL Society na kulipa jina Tanzania Loans Society, Rais Kikwete alitia saini ya makubaliano ya wazi nchini marekani na zilitolewa fedha za mtaji wa kuanzishwa kwa tawi hili na jumuia ya madola nchini marekani kiasi cha shilingi billion miatano.

Lakini kutokana na majukumu ya Rais jakaya mrisho kikwete kuwa mengi hivyo ikawa ni vigumu kwa yeye kusimamia na kuendesha mradi huu hivyo aliamua kugawa majukumu haya kwa Waziri mkuu wa Tanzania Mh. Mizengo na Ridhiwani Kikwete ambae ni mtoto wa Rais Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na Bank kuu ya Tanzania (B.O.T) na NMB.

Tanzania Loans Society inawakilishwa na Rais Jakaya kikwete, inaongozwa na General Manager Mh. Mizengo Pinda na inamilikiwa na Loan Officer Ridhiwani Kikwete kwa udhamini wa Rais Barack Obama. Lengo la kuanzishwa Tanzania Loans Society ni kutaka kuwasaidia watanzania wenye hali ya chini kimaisha

Nifursa kwa kila mtanzania mwenye umri wa miaka kuanzia 18 na mwenye akili timamu ajiunge na chama cha Tanzania Loans Society ili aweze kupata msaada wa kifedha.
Tutahakikisha kila mtanzania atakaejiunga na chama hiki kwa kujaza fomu ya uanachama na akachangia ada ya uanachama Tshs. 15,000 akawa mwanachama wa Tanzania Loans Society atapatiwa mkopo wa fedha anaohitaji pia kila atakaejiunga tutampatia zawadi ya uanachama / kianzio cha maisha Tshs.300,000 laki tatu bure.

Mtu yoyote anaruhusiwa kujiunga na mradi huu ili kutimiza ndoto zake unachotakiwa nikua na vigezo vifuatavyo, uwe ni mtanzania, uwe na akili timamu, uwe umetimiza miaka18 na uwe na kitambulisho cha aina yoyote ile. Kama unavigezo tajwa hapo unaruhusiwa kujaza fomu na ukajiunga ukawa mwanachama na kuchukua mkopo wa fedha kiasi chochote unachohitaji kuanzia laki moja na kuendelea, kila atakaejiunga nakua mwanachama wetu tutampatia zawadi ya shilingi laki tatu bure.


UTARATIBU WA KUJIUNGA:
Kujiunga na ili uwe mwanachama ni Rahisi Sana unachotakiwa ni kujaza fomu iliyopo Online katika tovuti hii utaiona Link hapo chini ya kujaza fomu imeandikwa "JAZA FOMU HAPA" katika fomu hii kuna sehemu utajaza kiasi cha fedha unachotaka ukopeshwe Ukishajaza fomu yote utatakiwa kuchangia mfuko wa wanachama kwa kulipia ada ya Uanachama shilingi elfu kumi na tano, ada hii ya uanachama italipiwa kwa njia ya Tigopesa na M-Pesa katika namba ya muweka hadhina mkuu wa Tanzania Loans Society ambae pia ni muweka hadhina wa bank kuu ya Tanzania BOT anafahamika kwa jina la Mohammed Malocho namba ya kulipia ni 0712 083 240 unaweza kulipia tigopesa katika namba hiyo 0712 083 240 jina litatokea Mohamed Malocho na kwa wateja wa Vodacom M-Pesa wanaweza kulipia katika namba hiyo hiyo pesa itatufikia. ukishalipia utatumiwa Code namba yako ya Uanachama na ndani ya dakika30 utatumiwa kiasi cha fedha za mkopo uliohitaji na utatumiwa Tshs.300,000 laki tatu bure kama zawadi kwa kila mwanachama atakae jiunga.


MAREJESHO YA MKOPO:

Marejesho ya mkopo yataanza kufanyika baada ya miezi miwili kupita kuanzia siku uliyochukua mkopo, utakapopatiwa mkopo utatakiwa ukae miezi miwili bila kulipia na baada ya hapo utaanza kua unalipia kila mwezi Tshs. 60,000 (elfu stini) mpaka deni lako lote litakapokwisha na hakuna riba kwa sheria ya dini hivyo utakachokopa ndicho utakacholipa.


KWANINI UNAJIUNGA ONLINE NA UNALIPIA ADA TSHS.15,000 (ELFU KUMI NA TANO) TIGO PESA?

Hili swali ni muhimu na wengi wanajiuliza wengine wanaingiwa na hofu kuona fomu zinapatikana Online na kwanini mtu asije ofisini na kujiunga ofisini? Jibu nikwamba tumefanya hivi kurahisisha upatikanaji wa huduma hii kwa kila mtanzania kwani ofisi zetu zipo Dar es salaam makao makuu jirani na chuo cha IFM jengo la Utumishi wa Umma ghorofa namba 30 floor ya 5. Tumeweka utaratibu huu watu wajiunge Online ili kila mtanzania apate mkopo kwani sio wote wanaoishi dar es salaam kuna wengine wanaish mikoani hivyo tungesema wote waje ofisini kuna wengine watashindwa kufika katika ofisi zetu ndio sababu ya kuwataka watu wajiunge Online.

JINSI YA KUJIUNGA UPATE MKOPO:

Kujiunga ni rahisi sana bofya katika hiyo link ifuatayo hapo chini imeandikwa "JAZA FOMU HAPA" Utaikuta fomu ya kujiunga ijaze.




maelezo haya fuatisha hapa! TANZANIA LOANS SOCIETY: MIKOPO YA FEDHA KWA KILA MTANZANIA

NB: kwa upande wangu naona hawa ni matapeli tu, ila unaweza kuwafuata for your own risk
 
Hao ni matapeli

Ni kweli kiongozi! Ukifuatilia thread ya tarehe 8/1/2013, "ukweli kuhusu Tanzania loans society" katika Business& Economic forum iliyochangiwa na Mwana memba "Msingi Hoja", utapata mbivu na mbichi ya hiyo Tanzania Loans society! Ni matapeli wa Kimkoa!
 
Sawa nimefanikiwa kujaza hiyo fomu na kulipa 15,000/=kama maelekezo yanavosema kuwa ni ada ya uanachama,tangu saa tatu asubuhi lakini mpaka sasa saa nane mchana bado sijapata taarifa yoyote kuhusu hiyo pesa
 
Sawa nimefanikiwa kujaza hiyo fomu na kulipa 15,000/=kama maelekezo yanavosema kuwa ni ada ya uanachama,tangu saa tatu asubuhi lakini mpaka sasa saa nane mchana bado sijapata taarifa yoyote kuhusu hiyo pesa

Inasikitisha sana kumwaona masikini mwenzako akipoteza ata kidogo alichonacho! Kwa nini mnakuwa warahisi hivi? Ndo maana kwa urahisi huu mnakuwa cheated na maccm!
 
Sawa nimefanikiwa kujaza hiyo fomu na kulipa 15,000/=kama maelekezo yanavosema kuwa ni ada ya uanachama,tangu saa tatu asubuhi lakini mpaka sasa saa nane mchana bado sijapata taarifa yoyote kuhusu hiyo pesa
Hapo ndio umeshaliwa kaka.. Wajanja ndio ugali wao..
 
Sawa nimefanikiwa kujaza hiyo fomu na kulipa 15,000/=kama maelekezo yanavosema kuwa ni ada ya uanachama,tangu saa tatu asubuhi lakini mpaka sasa saa nane mchana bado sijapata taarifa yoyote kuhusu hiyo pesa

:becky: pole kaka next time uckurupuke
 
Hawa watu wamesema wapo jengo la Utumishi wa umma floor ya 5 chumba namba 30 :
Wakuu mlio Dsm tutafutieni ukweli huo.
Na kama ni uongo kwa nini Mzee Mohamed Malocho asituambie na Mzee wa KAYA yule msemaji wake si anayaona haya ?
 
Back
Top Bottom