Tanzania kwanini ni wazito kufuata taratibu?

kipara kipya

JF-Expert Member
May 2, 2016
17,342
21,446
Tumeshudia mara nyingi mtanzania ukimwambia fuata utaratibu kama umemtuma avunje,tuangalie mifano midogo tukianzia kwenye mabasi ya abiria unaweza kuta nyote mmekata tiketi mtu siti yake.

Haionyeshi dirishani lakini akakomaa huyo ili tu akae yeye,angalia pale uwanja wa taifa jinsi taratibu za uingiaji zinaharibiwa,turudi huku sasa tumepata mabasi mapya yaendayo kasi lakini tayari tumesikia wengine walipanda wakagoma kushuka mpaka wakashushwa kwa nguvu ili mradi tu humo ndani taratibu zilivunjwa wengine wamekaa viti vya walemavu.
 
Sasa kama kwenye hayo magari ikitokea hajapanda mlemavu na viti vilivyobaki ni hivyo vya walemavu watu wasikae?
 
Jamii yoyote ile duniani ambayo inashindwa kuheshimu na kufuata taratibu ilizojiwekea,hiyo ni jamii ya WAHUNI.Mtu yeyote bila ya kujali elimu,cheo,hadhi,umri n.k. ilimradi hafuati taratibu,ni MHUNI.Na kwa mantiki hiyo basi,nchi hii uhuni umekithiri kwani tunaishi kihuni.
 
Ukienda kwa wenzetu ndio utajua sisi labda bado tupo kwenye evolution. Hadi hasira wakati mwingine.
Hakuna order, hakuna utaratibu, kila mtu ana haraka, kila mtu ni mjuaji, watu ni wachafuzi wa mazingira.

Tukiambiwa hili hapana, ni kama tumewekewa mafuta ya taa. Poor nchi yangu.
 
Haya mabasi hata nchi za wenzetu yapo na viti vya wazee/walemavu vimeandikwa kabisa pisha akiwepo mtu wa hvy anaehitaji seat. Kwamba unatuhusiwa kukaa mpaka akitokea mwenye kuhitaji
Hao tayari taratibu kwao ni kawaida lakini utakuja shuhudia mzee hapishwi siti wala mjamzito,si unaona mpaka leo hii maguta na bodaboda wanapita kwenye hizo barabara za hayo mabasi au hujaona dereva akiendesha gari no entry?
 
wabongo wana laana
Sio laana Mkuu,ile siasa ya BANGI eti UJAMAA,ndio imeacha MTINDIO wa UBONGO yaani Mtanzania wakati ule hakuwa HURU kama tulivyokuwa tunaimbishwa mashuleni ati TUMEPATA UHURU,kumbuka enzi zile kila kitu kilifichwa na kutolewa kwa wananchi kwa upendeleo,rushwa ukilinganisha na foleni ndefu kupita maelezo ili kupata chochote kile tena kwa pesa yako mwenyewe huku MIGAMBO isio na elimu na mengi MABUBU na VIZIWI yamesimama na MARUNGU kupiga watu bila hatia,baada ya watu kadhaa kutangulia mnaambiwa bidhaa imekwisha,mnarudi kesho alfajiri kupanga foleni tena na mambo yanakuwa yale yale,kwa hiyo watu walileemaa na wamekosa ustaarabu na hawaoni faida ya USTAARABU tena.
 
na ndio mabingwa wa kupenda kutoa rushwa ili asifuate utaratibu.
Kabisa Mkuu na yote hiyo ililetwa na siasa kijinga baada ya UHURU,sababu tulishajengewa FIKRA,UTAMADUNI NA KULAZIMISHWA KUKUBALI kuwa ukifuata utaratibu utalala na njaa na kama unataka huduma yoyote lazima UTOE RUSHWA kama unataka kupanda basi lazima upitie dirihani kama unataka kuingia mpirani mpaka uruke ukuta,kama unataka utibiwe lazima utoe rushwa na ukwepe foleni,sasa hiyo mpaka ifutike bado tuna safari ndefu.
 
Jamii yoyote ile duniani ambayo inashindwa kuheshimu na kufuata taratibu ilizojiwekea,hiyo ni jamii ya WAHUNI.Mtu yeyote bila ya kujali elimu,cheo,hadhi,umri n.k. ilimradi hafuati taratibu,ni MHUNI.Na kwa mantiki hiyo basi,nchi hii uhuni umekithiri kwani tunaishi kihuni.
Na ndio maana hatusongi mbele ki mfumo, kila mfumo uko shaghalabaghala, si elimu, afya, makazi. Kila mtu anajifanyia la kichwani mwake.
 
Hahahahh. Hii nchi ni ngumu sana kuongoza, lazima kichwa kiumbe, ndo sababu Magu anasema anajuuuuta kugombea uraisi.
Ndio zetu kuvunja utaratibu viwanja vya michezo mashuleni vimejengwa madarasa,viwanja vya wazi vimejengwa majumba
 
Sisi Waafrika hasa waTZ ni watu wa hovyo sana yaani hatuna ustaarabu kabisa anzia na bodaboda yaani hawa watu ni wapumabav.u sana halafu wakiambiwa wafuate sheria wanalalama kuwa wanaonewa
 
Sisi Waafrika hasa waTZ ni watu wa hovyo sana yaani hatuna ustaarabu kabisa anzia na bodaboda yaani hawa watu ni wapumabav.u sana halafu wakiambiwa wafuate sheria wanalalama kuwa wanaonewa
Sijawahi ona watu wapumbavu kama baadhi ya hawa bodaboda. Nimeangalia jinsi wanavyotumia barabara za mwendo kasi, serikali ikiendelea kuwachekea tutakuwa na miji ya hovyo kabisa.
 
The true test of civilization is, not the census, nor the size of the cities, nor the crops, but the kind of man that the country ,turns out.
 
Ni wagumu kufuata utaratibu kwa sababu sheria Tanzania ni kisu cha mkate, si msumeno. Leo unafanya kosa hufanywi chochote, kesho unafanya unanyooshewa tu kidole, keshokutwa unafanya unatoa rushwa, mtondogoo unaiba unaambiwa rudisha, kwa hiyo hakuna hofu juu ya madhara ya kufanya makosa. Na tabia hii pia inaanzia kwenye taasisi za malezi hasa nyumbani na shuleni. Mtoto hafundishwi kuwa kila kosa lina matokeo. Mwanafunzi anapewa mtihani, anaambiwa ajibu maswali mawili, yeye anajibu matatu na hafanywi chochote. Tena mivyuo mingine inamwambia mwalimu asahihishe yote matatu halafu achague mawili yenye alama za juu! Hii nchi ni kama jehanam kwa watu waliostaarabika wanaofata sheria. Ukiwa dereva ukafata sheria za barabarani uwezekano wa kugongwa au kufika nyumbani kesho ni mkubwa, achilia mbali matusi na kejeli. Unasimama nyuma ya zebra cross watu wavuke, nyuma huko anakuja dereva mwenzio "mstaarabu" amekanyaga mafuta ya kutosha halafu anawapigia honi wavukaji wampishe haraka iwezekanavyo. Anashika breki za ghafla, anashusha kioo anamwaga matusi!! Waenda kwa miguu nao ni hadithi nyingine ndefu. Boda boda mmeshasema. Huko kwenye taasisi nako ukifata taratibu nako inakula kwako. Ni kujifunza tu uvumilivu na kutokulalamika maana unaweza kupata maradhi yatokanayo na stress.
 
Back
Top Bottom