Tanzania kuwa Taifa kubwa kiuchumi ukanda wa maziwa makuu

Super Brain

Member
Apr 17, 2016
45
38
Tanzania kuwa Taifa kubwa kiuchumi Afrika Mashariki.

Kutokana na project kubwa zinazoendelea baada ya rais Mpya kuingia nchini Tanzania wananchi mbalimbali wa Kenya wameanza kupata hofu kuwa huenda taifa la Tanzania linampango wa kuwa Taifa kubwa lenye nguvu zaidi kiuchumi.

Ushawishi wa rais kwa wananchi wake na umakini anaoanza kuuonyesha achilia mbali jitihada za kuwafanya viongozi wawajibike ni moja ya maswala yanayotajwa kuwahofisha watu wa Kenya.

Vitendo vya kifisadi vya nchini Kenya ni moja ya vitu vinavyotia hofu raia wa Kenya kwani Rais wao anaonekana kutojali .

Suala lingine limekuwa likielezwa kuwa baada ya kipindi cha miaka mitano Tanzania itakuwa mbali kiuchumi na kuipita Kenya kwani uchumi wa Tanzania unakuwa haraka kuliko ule wa Kenya.
 
Tuwe na vitendo zaidi, tupunguze maneno. Siyo kuwa hatuwez, ila tuko na maneno mengi kuliko vitendo
 
Kijana, unatakiwa uje na "facts" zinazothibitisha hoja yako sio kuja hapa na "illusions" kama vile unashindana na mtu kuposti hapa jukwaani.
 
Taiga kubwa haliji kwa Maneno matupu, kiongozi was nchi anapaswa kuwa na maono, then atengeneze mpango mkakati then awashirikishe wadau, then aweke malengo, maswali ni haya, wapi tunataka kwenda? Tutafika VP? Na tunatifika Lin? Nini nguvu yetu? Nini mathaifu yetu? Tutatumuaje nguvu yetu kuyashinda madhaifu yetu, maadili yetu ni yepi? Nani tufanye nae kazi? Mtindo wetu ni UPI? UPI ni miundo wetu? N.k
 
kwa maigizo haya na mizuka hii???? sidhani kama kunauwezekano wowote maana maigizo ya kutafuta kuandikwa kwenye magazeti hayawezi saidia taifa kupiha hatua
 
tz.PNG
CgUAwBOWsAAq3KZ.jpg
 
Tanzania kuwa Taifa kubwa kiuchumi Afrika Mashariki.

Kutokana na project kubwa zinazoendelea baada ya rais Mpya kuingia nchini Tanzania wananchi mbalimbali wa Kenya wameanza kupata hofu kuwa huenda taifa la Tanzania linampango wa kuwa Taifa kubwa lenye nguvu zaidi kiuchumi.

Ushawishi wa rais kwa wananchi wake na umakini anaoanza kuuonyesha achilia mbali jitihada za kuwafanya viongozi wawajibike ni moja ya maswala yanayotajwa kuwahofisha watu wa Kenya.

Vitendo vya kifisadi vya nchini Kenya ni moja ya vitu vinavyotia hofu raia wa Kenya kwani Rais wao anaonekana kutojali .

Suala lingine limekuwa likielezwa kuwa baada ya kipindi cha miaka mitano Tanzania itakuwa mbali kiuchumi na kuipita Kenya kwani uchumi wa Tanzania unakuwa haraka kuliko ule wa Kenya.

Kwa nini iwe "tetesi" tena iwapo unaongelea jambo ambalo ni halisi?
 
Kama Kenya kwa muda mrefu uchumi wao unakuwa kwa kiwango cha 3.5 hadi 5,Tanzania inakuwa kwa zaidi ya 6 ndiyo imechangia kwa kiasi kikubwa kupunguza gape lilikopo kwa kasi.Na inaelezwa baada tu ya miaka ya 1990 mwishoni Tanzania imekuwa ikienda vizuri kwan miaka ya 1980 Kenya walikuwa tayari mbali na kama wangeitumia vizuri nafasi yao wangekuwa mbali sana.Sasa gape lao linazidi kupunguzwa kwa kasi
 
Watanzania kwa kujipa moyo bana tumezidi, yaani tunapenda kuishi kwa matumaini, wewe ungekuwa mwanafunzi wangu ninayekusimamia kama professor wako lazima ningekupiga disco
 
Back
Top Bottom