SI KWELI Tanzania kuiunga mkono Iran kwenye vita

SI KWELI Tanzania kuiunga mkono Iran kwenye vita

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
kwa siku za hivi karibuni kumekuwa na chapisho linalosambaa kwenye mtandao wa kijamii wa facebook ikionesha gazeti la kishindo likieleza kuwa jeshi la tanzania linajiandaa kupeleka majeshi yake nchini iran kwa jili hya kuipiga Israel.


Tanznia Iran.jpg
 
Tunachokijua
Mnamo mwezi Juni Israel ilianzisha mashambulizi katika taifa la Iran na kuharibu baadhi ya mali zake huko maofisa kadhaa wa juu wa kijeshi wakiuawa. Mara baada ya shambulio hilo la kushtukiza Iran nayo pia imeendelea kujibu mashambulizi kuelekea Israel na kupelekea kuendelea kwa mzozo huo.

Madai

Baadhi ya watumiaji wa mitandao mbalimbali ya kijamii ikiwemo Facebook wamekuwa wakisambaza picha ikimuonesha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aikiambatana na ujumbe kuwa;

"Kutokana na vita inayoendelea kati ya Israel na Iran serikali ya Tanzania inaiunga mkono Iran"

Uhalisia wa taarifa hiyo

JamiiCheck imefuatilia taarifa hiyo kwa kina na kubaini kuwa ni uzushi kwani hakuna uthibitisho kuwa msimamo huo umetolewa na serikali ya Tanzania.

Kupitia hotuba alizozifanya Rais Samia katika ziara zake na matukio mengine ya kiserikali hakuwahi kutamka msimamo wa Tanzania dhidi ya vita inayoendelea katika mataifa hayo.

Aidha hakuna taarifa kwa umma iliyotolewa kuonesha msimamao wa Taifa wa la Tanzania kuunga mkono Iran wala Israel katika vita inayoendelea.
Back
Top Bottom