Tanzania kama taifa tunaelekea wapi..?

Bahimba

JF-Expert Member
May 8, 2013
510
346
Nakumbuka mwalimu wangu aliwahi kuniambia ukiwa muongo usiwe msahaulifu, nimekaa nikawaza nakuwazua hivi inchi hii tunaelekea wapi.? Jana wakati mkuu katika hotuba yake akiwa anawaapisha wateule wake, alionekana kukerwa na mitandao ya kijamii ambayo imekua ikitoa taarifa za uongo, moja wapo ikiwa ni pamoja na kuandika taarifa zilizomuhusu katibu mkuu wake kua alikua na mpango wa kuongea na waandishi wa habari siku moja baada ya NAPE kutumbuliwa,

Rais aliongea kua huo ni uongo kwa sababu Kinana kamtuma India kwenda kutibiwa, tena akafika mbali zaidi kua atakua huko ndani ya siku 14,

Sasa nimejaribu kuweza kwa sauti,

1.Unamtumaje mtu kwenda kutibiwa.?
2.Kwa nini upange kua atakua huko katika kipindi cha siku 14...?

Alijuaje kua hiyo tiba itachukua siku hizo? Jamani fikeni sehemu washauri wa mh, mmwambie ukweli , hivi inawezekana mke wa Rais atibiwe muhimbili halafu Kinana amtume akatibiwe India,? Mbona tunafanywa kama watoto wadogo ni hayo tu.
 
Nadhan Mh rais ana ndoto kubwa kuhusu nchi hii,

Kule anakotaka kuifikisha ndiko tunakokwenda,

Mh rais ndiye dereva wetu, anakotupeleka ndiko tunakwenda, ndoto yake ni ndoto yetu.
 
"taifa limepoteza muelekeo linaenda kama gari bovu"-rais wa awamu ya pili aliyasema hayo wakati wa utawala wa awamu ya tano
 
Mwenyew nlishangaa sana eti "nimemtuma kutibiwa" nkawaza labda anaeumwa ni pombe then katibu ndio akatumwa kutibiwa kwa niaba ya pombe...
The rest is senselessness hakika hatuna rais kile ni kituko cha karne
 
me nipo naenda tu wala sitaki kujua tunaenda wapi tena.. dereva ukimuuliza anakuambia atakufunga mdomo au tunaenda viwandani mbona njia siyo unatafuta ugomvi na dereva asije akapindua gari bure nikafa .. nimeamua kuchili tu
 
Me naenda nnapokufahamu sitaki mtu anifate kila mtu apite njia yake tukutane hukoooo
 
Back
Top Bottom