Tanzania ingekua na wanawake 10 kama huyu tungesonga mbele kimaendeleo.

kyagata

JF-Expert Member
Oct 18, 2016
8,972
16,951
wakubwa,heri ya jumapili?
kuna binti kanistaajabisha sana, huyu binti Nina uhusiano naye wa kama miezi minne hivi, sasa juzi alikuwa anasafiri kuelekea kituo Chake cha kazi Bahati mbaya gari walilokuwa wanasafiria likapata Ajali na yeye binafsi akawa ni miongon Mwa majeruhi.

Toka siku ya tukio nilikua nikimpigia simu alikua ananiambia kuwa nisubiri kidogo atanipigia hali iliyopelekea mimi nihisi labda yuko kwa mchepuko, Leo kanitafuta ndo ananieleza situation nzima ilivyokua na amenitumia picha akiwa hospital na picha ya gari ilivyobondeka...ananiambia hakutaka kunipa presha siku Ile.

Katika Ajali kapoteza pesa zake zote, simu na vitu vingine. So mimi kama mpenzi wake nimemuuliza nimtumie sh. ngapi ili kusaidia mahitaji yake ila amekataa hata senti yangu, nimembembeleza walau Nimtumie laki mbili basi hata Anunue simu nyingine amekataa badala yake ameniambia hiyo laki mbili niweke akiba

So nimemtafakari nimeona taifa letu lingekua na wanawake kumi kama huyu nadhani saivi tungekua tumewaacha mbali sana USA kimaendeleo.
 
wakubwa,heri ya jumapili?
kuna binti kanistaajabisha sana,huyu binti Nina uhusiano nae wa kama miezi minne hivi,sasa juzi alikua anasafiri kuelekea kituo Chake cha kazi Bahati mbaya gari walilokua wanasafiria likapata Ajali na yeye binafsi akawa ni miongon Mwa majeruhi.toka siku ya tukio nilikua nikimpigia simu alikua ananiambia kuwa nisubiri kidogo atanipigia hali iliyopelekea mimi nihisi labda yuko kwa mchepuko,Leo kanitafuta ndo ananieleza situation nzima ilivyokua na amenitumia picha akiwa hospital na picha ya gari ilivyobondeka...ananiambia hakutaka kunipa presha siku Ile.Katika Ajali kapoteza pesa zake zote,simu na vitu vingine.so mimi kama mpenzi wake nimemuuliza nimtumie sh ngapi ili kusaidia mahitaji yake ila amekataa hata senti yangu,nimembembeleza walau Nimtumie laki mbili basi hata Anunue simu nyingine amekataa badala yake ameniambia hiyo laki mbili niweke akiba
so nimemtafakari nimeona taifa letu lingekua na wanawake kumi kama huyu nadhani saivi tungekua tumewaacha mbali sana USA kimaendeleo.

Mnunulie simu na maitaji mengine umtumie la sivyo kuna njema itagharamia.
 
Hakuna wakati mzuri Wa kumfariji mtu kama wakati Wa shida,usimtumie hiyo laki mbili Bali panda gari nenda kamuone hali yake, kitendo cha kwenda tu ni zaidi ya Million maana utakua umeonyesha uungwana Wa hali ya juu
 
we kyagata wewe kwahiyo unataka kusema sisi ndo tunarudisha Tanzania nyuma sio?
Ndiyo mnaomba pesa mno, utadhani mizimu inadai kafara..!

Kuna kigori mpya nimempata shida anapenda starehe huyo kila kitu kubebwa km maiti.
 
sio kama kakataa... anakuweka sawa uingie kwenye 18 na ushaingia kwenye box *****... sasa ngoja atoke huko uone... acha ni subscribe tu..!
 
Jamani yaani kitendo kidogo tu hicho tayari ushamwagia sifa. Jiongeze:-

-hakupendi unajipendekeza ndio maana hali pesa zako hakuchuni kabisaa ili siku mkiachana usiwe na masimango ya ooh kala sana pesa zangu,mara nimemgharamikia sana

-hauna uwezo mkubwa kifedha anajishtukia atakufilisi ndio maana anakwepa kukupa majukumu makubwa.

-anakupenda ila hana amani na uhusiano wenu wa miezi minne

Katumia simu ya nesi,je picha za ajali nani alizipiga?kama ni wenzie je namba za wenzie kazikariri kiasi cha kuwaomba picha kwa watsup ya nesi ili tu akutumie!!?

 
Hakuna wakati mzuri Wa kumfariji mtu kama wakati Wa shida,usimtumie hiyo laki mbili Bali panda gari nenda kamuone hali yake, kitendo cha kwenda tu ni zaidi ya Million maana utakua umeonyesha uungwana Wa hali ya juu
Yes.
Naiunga mkono hoja hii kwa nguvu zangu zoote.
 
mwanamke ameshakwambia almepata matatizo kidume baada ya kujitutumua fasta unaanza kuuliza nikutumie sh ngapi!
siku nyingine demu akipata matatizo usiulize msaada unatoa vp, wewe ni kutuma tu haraka
 
Back
Top Bottom