Tanzania inaongoza duniani kwa kuathirika na Malale: Ugonjwa hatari kuliko yote barani Afrika

Mgambilwa ni mntu

JF-Expert Member
May 30, 2017
2,869
3,188
Kuibuka kwa Ugonjwa wa UKIMWI (AIDS) nchini miaka ya 1980s, kulifanya Ugonjwa hatari wa Malaria kupoteza nafasi ya kwanza kama Ugonjwa hatari barani Afrika. Hali hii inaweza kuleta shida kwa msomaji wa taarifa hii kuwa, Ugonjwa hatari barani Afrika kwa miaka yote umekuwa ni Malale (sleeping sickness/trypanosomiasis/nagana) unaoambukizwa na Mbung'o (Tse tse fly) wanaosababisha vimelea aina ya Ndorobo (Trypanosoma). Ndorobo aina ya T. brucei Rhodesiense wanaopatikana Afrika Mashariki na Kusini ndio hatari kuliko aina ya T. brucei Gambiense wa Afrika Magharibi.

Hatari ya Ugonjwa wa Malale ni kuwa, unashambulia binadamu (sleeping sickness), pamoja na mifugo (nagana) hasa ng'ombe, huku Ugonjwa huo ukiwa hauna tiba kwa miaka mingi.

Wakati Wabantu wanahama kutoka Afrika Magharibi miaka ya 1,500 BC, chakula chao kikuu kilikuwa viazi vikuu (yams) lakini walipofika eneo la Maziwa Makuu, waliingiliana na Jamii za Nilotes na Hamites (waliohamia kutokea Sudan/Ethiopia) na kujifunza kulima mtama na uwele, pamoja na teknolojia ya ufuaji vyuma. Kikubwa kingine walijifunza ufugaji wa mifugo hasa ng'ombe, hivyo Jamii hizo za Kibantu zilipoanza kuingia nchini kuanzia miaka ya 1,000 AD, waliingia na mifugo waliyopata kutoka kwa Jamii za Nilotes.

Hata hivyo, changamoto kubwa waliyokutana nayo nchini Tanzania, ni uwepo wa Mbung'o katika eneo kubwa la Tanzania, lililofunikwa na Miti ya Miombo. Eneo hilo lililojaa mbung'o ni pamoja na Mikoa ya Kigoma, Tabora, Katavi, Rukwa, Ruvuma, Mtwara, Lindi, Pwani, Morogoro na Tanga, Geita. Vilevile, nusu ya Mikoa ya Mbeya (Chunya/Mbarali), Kagera (Biharamulo) na Mara (Serengeti), Singida (Manyoni), ilikuwa pia imejaa mbung'o.

Kwa kuwa, shughuli kuu na rahisi ya Jamii hizo za mwanzoni kuingia nchini ilikuwa ni kilimo na ufugaji, ilizilazimu Jamii hizo kutafuta maeneo yenye hali nzuri ya hewa (Milima ya Kilimanjaro, Meru, Uluguru, Usambara, Rungwe, Nguru, Hanang', Udzungwa, Kipengere, Upare, Ufipa, pamoja na Ukanda wa Ziwa Victoria). Aidha, kwa kuwa, Mbung'o hawasitawi kwenye maeneo yenye ukame, ilisababisha ukuaji mkubwa wa shughuli za ufugaji katika maeneo yenye ukame katikati ya Tanzania kuanzia kwa Wasukuma, Wanyamwezi, Wanyilamba, Wanyaturu, Wagogo, Wambulu, Wadatooga (Waberbaig), Wamasai na Warangi.

Ndiyo maana leo hii, Eneo lililoko kati ya Tabora - Kahama - Biharamulo - Kasulu - Sumbawanga - Mbeya - Iringa hadi Manyoni, ni theluthi ya Tanzania lakini lina wakazi wasiozidi milioni 5 (kati ya Watanzania zaidi ya milioni 45 (2012). Eneo lingine kubwa la Mikoa inayozunguka Mbuga ya Selous (Ruvuma - Lindi - Morogoro lina wakazi wachache sana licha ya ukubwa wake huku likiwa na mvua za kutosha kuivisha mazao.

Kwa kuwa Dunia nzima, ni Afrika pekee inayosumbuliwa na Mbung'o, Tanzania ni ya tatu nyuma ya DRC na Angola kwa kuwa na maeneo makubwa yaliyoathirika na Malale. Hata, hivyo Ndorobo aina T. brucei Gambiense, hawana athari kubwa kimaisha kama wa T. brucei Rhodiense, Ndiyo maana Tanzania ndiyo imekuwa mwathirika mkubwa wa mbung'o kuliko kote barani Afrika.

IMG_3420.GIF
IMG_3423.JPG
IMG_3428.PNG
IMG_3431.JPG
 
Ukitazama Ramani hiyo Afrika Mashariki, upande wa Tanzania, utaona kuwa, eneo lenye mbung'o linachukua wastani wa asilimia 60% ya ukubwa wa Nchi yetu but kiasili limekuwa na mifugo isiyofikia asilimia 10% ya mifugo (ng'ombe, mbuzi, punda na nguruwe) nchini.

IMG_0732.JPG


Ramani nyingine za Tanzania na Afrika Mashariki:
IMG_0733.JPG IMG_0745.JPG
 
Leo hii kutokana na ukame mkubwa unaoyakumba maeneo ya wafugaji Mikoa ya katikati na kaskazini mwa nchi, imesababisha wafugaji hao hasa wasukuma kukimbilia katika Mikoa ambayo kiasili imekuwa makazi ya mbung'o hasa Katavi, Rukwa, Mbeya (Chunya na Mbarali), Ruvuma na Morogoro, hadi mkoani Pwani.
 
Back
Top Bottom