#COVID19 Tanzania inajipima mabavu dhidi ya Covid-19; yupi atakuwa wa kwanza kusalimu amri?

Kuna mtu mmoja inasemekana ndiye anaongoza kuidharau COVID'19 lakini cha kusikitisha ni kwamba kila mara Covid'19 ikilipuka anakimbilia kujificha kwenye kitovu cha utalii.
 
Ni mwenda wazimu tuu anayeweza kudhani Mwenyezi Mungu anaweza kuipendelea Tanzania zaidi ya Jerusalem, Mecca,Madina , Vatican na Canterbury
Jiwe aagize chanjo ambayo sisi tusio muaamini tununue chanjo
Fools paradise
 
nahisi mwendawazimu utakuwa wewe.
Maana MUNGU anasema niombeni NITAWAJIBUNI Kama hawakumuomba na wanategemea akili zao.
Ulitaka mungu afanye nini?
MUNGU ANAONESHA UWEZO WAKE NA UWEPO WAKE.
Ndo mjue MUNGU YUPO
Ni mwenda wazimu tuu anayeweza kudhani Mwenyezi Mungu anaweza kuipendelea Tanzania zaidi ya Jerusalem, Mecca,Madina , Vatican na Canterbury
Jiwe aagize chanjo ambayo sisi tusio muaamini tununue chanjo
Fools paradise
 
Corona ipo kila mtu ajiongeze mwenyewe kama kweli unapenda watu wako basi chukuwa tahadhari.

Siasa ina sehemu zake lakini sio katika mambo ya msingi kama haya, ndio maana mkuu kila mkutano analazimisha watu waamini hakuna hasa katka siku za karibuni ukiona mtu anatumia nguvu sana kukanusha kitu basi ujuwe kuna jambo.

Sawa sawa ukiona mtu anaapa sana miungu wote hajafanya basi tia shaka. Naunga mkono hoja yako.
Tatizo wote wanatumia nguvu,hao wanaosema corona hakuna na hao wanaosema ipo wote wanatumia nguvu na kuna msukumo wa siasa nyuma yake.
 
Daktari unafahamu kuwa uko chini ya wizara ?
Mimi Ni mwanataaluma wa Public health nachotambua Ni kosa kutangaza Hali ya hatarii au mlipuko ukiwa muhudumu katika sekta ya Afya taarifaa zotee zinatakiwa kupitia mfumo wa IDSR(integrated disease surveillance and response) na mwenye mamlaka ya kutangaza Ni wazirii au mtu mwingine mwenye dhamana huyo daktarii anakiuka miiko ya msingii kabisa... Hafai.
 
Hapana unakosea sana katika hili, mimi namuunga mkono Rais kuondoa hofu katika jamii ila ni juu yetu kuwa waangalifu ugonjwa upo.

Halafu wanunuzi wa chanjo Tz wala sio walengwa kama tunaongelea biashara, nchi tajiri duniani wameanza au wameshanunua dawa in advance ndio wenye pesa nchi nyingi za Africa tutakuja kupewa bure tu.

Kumbuka chanjo za watoto zote ni bure kutoka UN hatulipi kitu na matokeo chanjo wa watoto sote tunajuwa faida yake. siasa pembeni corona ipo ndio maana unaona siku za karibuni raisi kila mara anaongelea hilo hatuna corona sababu anajuwa hofu iko.

Hawana sababu ya kutulenga sisi maana sio wanunuzi hata tungekubali corona ipo zaidi tungepata misaada na chanjo za bure.

Lini serikali imetoa tamko la kuikataa chanjo ya corona?

Je watu wanaosema hakuna takwimu za corona Tanzania wanajua kwamba wagonjwa wanaofika hospital wakiwa na dalili za corona wanapimwa na kupatiwa huduma stahiki?

Hata kama mtu humpendi kiongozi usipoteze uzalendo kwa nchi yako kiasi hiki
 
ucheni unafiki na uongo, hakuna mtu aliyesema virusi vya corona ni kitu ca kufikirika..... nadhani Rais na watanzania tunaamini hii kitu ni real ndio maana tukaamua kumuachia Mungu maana yeye ndio mjuzi wa kila kitu.

Kuhusu chanjo najua serikali ILIWEKA MAMBO CLEAR KABISA KWAMBA HAINA MPANGO WA KUAGIZA HIZO CHANJO INSTEAD INAENDELEA NA UTAFIT WA LOCAL MEDICS,

Ahsante.
Wamarekani, Wachina na Urusi wanagombea "abiria" wa chanjo zao...wapo wanamwagiana fitina!
 
Waliobuni hii biashara ya corona lazima watakua wanamuangalia rais wetu John Pombe Magufuli kwa jicho la husda sana.

Au nakosea ndugu yangu Sumu ?
Wameishaanza kugombania masoko yenye walaji wengi kama India, Brazil, Afrika, nk! Watengenezaji wa chanjo wa Marekani, Urusi na Uchina wanapakua chanjo hata kabla " hazijaiva" kuwahi wateja!
download (1).jpg
 
Lakini tusisahau kuwa Corona inaambukiza vipi nimonia nayo inaambukiza?

Mimi sipingi TANZANIA kuwa na Corona Ila taarifa ziwe za ukweli.

Tangu tarehe 17 mwezi wa 3 mwaka 2020 mpaka Leo Kama Corona ingekuwepo TUNGEKUFA WENGI sanaaa.

Na wagonjwa wangeongeza lakini mbona hatuwaoni hao wagonjwa
Tatizo sasa hivi ukisema mtu kafa kwa nimonia utaambiwa hiyo ni corona wanaficha kwa kudanganya kuwa ni nimonia.
 
Lakini tusisahau kuwa Corona inaambukiza vipi nimonia nayo inaambukiza?.
Mimi sipingi TANZANIA kuwa na Corona Ila taarifa ziwe za ukweli.
Tangu tarehe 17 mwezi wa 3.mwaka 2020.mpaka Leo Kama Corona ingekuwepo TUNGEKUFA WENGI sanaaa.
Na wagonjwa wangeongeza lakini mbona hatuwaoni hao wagonjwa

Hakuna aliyekataa hakuna CORONA ila wale wahasishaji wa vifo vya corona wangesema;

Wangapi Kati yao walishaugua vipimo vikaonyesha wana corona ili tuongee tukiwa na hakimu japo za makisio? Au waseme kama wakiumwa wanapiga nyungu na kupona

Wangapi wameshapata takwimu toka mahospitalini kuonyesha idadi? Najua mgonjwa ukiwa na dalili kwenye hospital zetu unapimwa

Watu wanakufa miaka yote ila siku hizi kila anayekufa naona kuna watu wanakuja kucomment "Corona", nadhani njia sahihi ya kusema vifo vimeongezeka sababu watu wanakufa kwa corona ni hao wenye wanasema watuletee walau takwimu za watu waliokufa january 2018,2019 na 2020 tulinganishe na takwimu za vifo vya january 2021 ndio tuweze kuongea

Vinginevyo haya maneno bora yaachwe maana hii ni upotoshaji, kujitisha na kuwatisha watu wasiokua na uelewa
 
Back
Top Bottom