Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 21,441
- 40,534
Pamoja na mikanganyiko miingi iliyoko kwenye Jamii yetu kuhusu mambo ya kisiasa na kijamii, kuna jambo nataka kulijua. Ili nchi isonge mbele kiuchumi na kijami ni lazima kuwepo na sera zinazoongoza masuala hayo ya Kiuchumi na kijamii. Na sera hizo ni lazima zijengwe juu ya msingi wa mfumo wa uendeshaji mambo unaofuatwa na nchi husika.
Kwa mfano Misingi ya Chama cha "Democratic" na "Republican" vya Marekani kuhusu binadamu inatofautiana kabisa. Demokratik chenyewe kinaamini kuwa Binadamu ni mtu huru na anatakiwa kulindwa ili autumie uhuru wake huo kwa ukamilifu.
Ndiyo maana huwa Demokratik ikishika uongozi wa nchi ya Marekani basi na sera za nchi hiyo kuhusu mambo yafuatayo hubadilika. Kwanza ushoga huruhusiwa na mashirika yanayopiganiA haki za ushoga na usagaji husaidiwa fedha na taasisi za Kiserikali kama vile USAID na zinginezo. Utoaji mimba huwa ni jambo linaloruhusiwa na utaona wanaotaka utoaji mimba liwe jambo la kisheria wanapata nguvu sana kwa kuwa serikali ya shirikisho huwa inawaunga mkono.
Hoja kubwa ya Demokratik ni kwamba kama mtu anataka kutoa mimba wewe ambaye si sehemu ya mimba hiyo unaathirika kivipi. Au mtu anapenda kuwa shoga wewe ambaye jirani yake utapatwa na nini kwa yeye kuwa shoga au Msagaji? Demokratiki ni waungaji mkono wakubwa sana wa hoja ya kuwasaidia wagonjwa mahututi kujitoa uhai kwa usaidizi wa "wataalam" ili waondokane na mateso yanayowakabili.
Kwa hiyo utaona kwa sasa kwa miaka kama 8 ambayo Marekani inaongozwa na Demokratik na sera za nchi hiyo kuhusu ushoga zimebadilika. Kwa sasa majimbo yanayoruhusu watu kujitoa uhai yameongezeka, yanayokubali ndoa za jinsia moja yapo ya kutosha na watu wanaotoa mimba "Kisheria" wamekuwa wengi zaidi kuliko wakati nchi hiyo inaendeshwa na chama cha Republikan.
Ingawa Demokratik nao wana sifa nyingine nzuri ambayo mara nyingi huchaguliwa wakati uchumi wa nchi hiyo unapokuwa umedorora na wao hufanikiwa kuufufua, lakini pia wao huwa hawapendi kuingilia sana mambo ya mataifa mengine kutokana na misingi ya chama hicho kuamini kuwa kila mtu anao uhuru wa kujiamulia mambo yake mwenyewe bila ya kuingiliwa ingiliwa.
Republikan wao ni wahafidhina (Conservatives) wanaamini mtu ni mali ya jamii! Ndiyo maana wao huzuia utoaji wa mimba, huzuia ushoga na usagaji, hawaungi mkono kujiua kwa hiyari, wanapenda kuingilia mambo ya nchi nyingine kwa sababu hiyo wao ndiyo mara nyingi huanzisha vita na nchi nyingine na kutumia hela nyingi kwa ajili ya vita hizo na kuleta mdororo wa kiuchumi katika nchi yao.
Nimetoa mifano hiyo ili kuonesha misingi ya vyama au nchi jinsi inavyoathiri utungaji sera wa nchi husika. Kwa misingi hiyo ndiyo maana nataka kujua kwa sasa misingi ya uendeshaji wa mambo katika nchi yetu kisiasa ni ya Kijamaa au ni ya kibepai? Yaani sera za nchi yetu zinatungwa juu ya msingi wa Kijamaa au Juu ya Msingi wa Kibepari?

Last edited: