Tanzania imegawanyika makundi mawili ambayo ni WAFAIDIKA vs WAATHIRIKA na Madawa ya kulevya

COARTEM

JF-Expert Member
Nov 26, 2013
3,600
3,651
Niukweli usiyopingika kuwa kwa sasa nchi ina makundi mawili.
Kundi la kwanza: WAFAIDIKA NA MADAWA YA KULEVYA
Kundi la pili: WAATHIRIKA NA MADAWA YA KULEVYA.

1. WAFAIDIKA NA MADAWA YA KULEVYA: ni wale wafanyabiashara hiyo, ndugu zao wanaowategemea, wanasiasa wanaofadhiliwa na drug dealers hao pia na vyama vya siasa vinavyobebwa na dru dealers hao. Kundi hili limekuwa likihakikisha wanadhoofisha vita hii kwa kuwatumia watu maarufu kupinga kiaina vita hii na hata kurubuni medias mbalimbali kubadilsha upepo wa tuhuma zao na kupandikiza tuhuma zisizo na mashiko kwenye mitandao.
shukrani kwa Rais MAGUFULI na vyombo vyake vya usalama kusimama imara na kuhakikisha vita hii inafanikiwa, maana jitihada hizo zinaonekana kila mkoa hapa Tanzania.

2. WAATHIRIKA NA MADAWA YA KULEVYA: ni wale Mateja, ndugu zao hao mateja, na watu wote wanaopata madhara ya kusumbuliwa na mateja popote pale Tanzania.
Familia ambazo zina mateja zipo kwenye mateso makali sana maana kila siku ni kesi za kuibiwa vitu ndani, vijana hao kuambukizwa magonjwa mbalimbali ikiwemo HIV/AIDS, Homa ya ini n.k n.k.
Mtaani watu wanaibiwa na kuporwa mali zao na vijana wanaotumia dawa za kulevya ili waweze kujipatia pesa za kununulia dawa hizo.

ANGALIZO: Ukimuona mtanzania yoyote anapinga jitihada hizi za kupambana na dawa za kulevya zilizowekewa CATALYST na Paulo Christian Makonda basi ujuwe mtu/kikundi/Chama hicho ni WAFAIDIKA NA MADAWA YA KULEVYA.
 
Back
Top Bottom