Tanzania ijayo ya vyama vingi katika siasa

mayaJr45

JF-Expert Member
May 12, 2016
560
205
Najaribu kuangaza na kufikiria mawazo ya wanasiasa wetu hasa chipukizi hatima yao miaka kadhaa mbele.Napata majibu mengi na mitazamo mingi

a) Bado mpaka sasa wengi wana tegemea kufikia mafanikio kwa kupandikiza chuki kuhusu CCMA na Mapungufu ya serekali.

b)kutumia kigezo cha takwimu z
a sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 kwamba 60% ya wapiga kura ni vijana na 100% ya vijana ni wafuasi wa upinzani.

c)Kudharau jitihada za serekali ya chama cha mapinduzi kujielekeza kurudisha heshima ya utumishi wa Umma, kupambana na Ufisadi , kujielekeza kutatua kero mbalimbali

Nimeongea hayo kwa maana moja bado kuna watu wanaendelea kuwa na mawazo potofu kuelekea siasa mpya ya vyama vingi nchini.Wasomi na wachambuzi mbali mbali walishasema awamu hii ni mwiba mchungu kwa wapinzani wasipo jipanga katika siasa za kushindana katika sera zenye kupata tafsiri yenye uhalisia kwenye jamii yetu .
Zitto Kabwe alishalisemea hilo na Dr kitila Mkumbo.

Nchi hii inawapiga kura wa aina tatu kwa mtazamo wangu nasema hivi kwakua sanduku la kura mwisho wa siku ndio linatoa majibu ya nani anashika dola.

a)Wale ambao ni wafuasi wa chama fulani kwamba hata iweje kama ni CCM ni CCM na kama ni CHADEMA NI CHADEMA ;

b)Wanaomchagua mtu kwa jina lake na umaarufu wake ;

c)Wanaotegemea na kushawishiwa na sera za wahusika .

Nazungumza hivi kwa maana.Nitumie mifano ya majimbo mawili Kigoma mjini na Simanjiro.Simanjiro inaonyesha MH Magufuli alipata kura nyingi kuliko wapinzani wake ila ubunge na udiwani CCM haikupata kura nyingi.Kigoma mjini pia Uraisi CCM kura nyingi Ubunge na Udiwani ukaenda ACT .

Kwa mifano hiyo maana yangu ni siasa inabadilika Tanzania kutokana na hamasa ya watu kujua wanataka nn na Kiongozi wa aina gani kwa maeneo flani kwamba hawajali wewe ni CCM ,CHADEMA ,ACT kikubwa wanaangalia mtu atakae waondoa pale walipo .Zitto kafanikiwa maana kapigiwa kura na wana CCM.Bado watu wanafuata na kuamini kwenye siasa yake iliyompa umaarufu miaka ya 2005.

Nahitimisha kwa kusema hivi bila kujali itikadi siasa inabadilika tuende na mabadiliko hayo.
 
Kwa Tanzania sio kweli kuwa sanduku la kura ndilo linaamua nani awe kiongozi wa nchi bali ni:-

"Dola, Wenye mamlaka na Mbinu hasa Goli la Mkono"

You need evidence? = Tanzania mainland and Zanzibar 2015 General Elections.
 
Kwa Tanzania sio kweli kuwa sanduku la kura ndilo linaamua nani awe kiongozi wa nchi bali ni:-

"Dola, Wenye mamlaka na Mbinu hasa Goli la Mkono"

You need evidence? = Tanzania mainland and Zanzibar 2015 General Elections.
kwa point flan learn kufocus point ya mada husika .u ddnt
 
Kaka umefanya uchambuzi mzuri sana , kakini nadhani hukuzingatia ili la kuwa mshindi na la kutangazwa kuwa mshindi
Unaweza kuwa umeshinda lakini usitangazwe kuwa mshindi, na unawezwa kushindwa na ukatangazwa kuwa mshindi
Hoja yako ingekuwa na uzito kamili kama ungeanza kulizungumzia la TUME HURU YA UCHAGUZI na pia vyombo vya ulinzi na usalama vile HURU
 
Back
Top Bottom