Tanzania iachane na mpango wa kujiunga na Shirikisho la EA na Mkataba na Ulaya.

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
16,997
20,329
Kila binadamu ameumbwa na mitazamo yake, yaweza kuwa mibaya au mizuri, na ifahamike kuwa juu ya kila jambo kuna mtazamo hasi na chanya. Siku wote tukiwa na mtazamo mmoja basi tutakuwa tumechagua kuwa wajinga.

Mtazamo wangu juu ya Tanzania mbele ya uso wa dunia, Kuhusu Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, upo tofauti kabisa na wengine.

Kwanza ninafikiri Tanzania HAINA SABABU za MSINGI za kujiunga na kile kiitwacho Shirikisho la Afrika Mashariki, na kwamba kutakuwa na dola moja, sarafu moja na mengine mengi yanayotafsiri umoja miongoni mwa nchi hii sita kwa sasaa.

Nina sababu zenye maneo zaidi ya milioni moja kupinga uanzishwa na uhimizaji wa umoja huu, lakini nitaeleza moja kwa kifupi tu ambayo ni usalama wa Tanzania.

Tanzania imewekeza vizuri mfumo wa ulinzi katika nchi zote za kusini mwa Jangwa la Sahara, hivyo jaribio lolote la kuunganisha nchi hizi na maslahi yao kutailazimu Tanzania kubadili mfumo huo na ama kuathiri kabisa medani nzima ya kiulinzi iliyowekezwa tangu baada ya kuvunjika kwa Afrika Mashariki ile ya nchi tatu. Tunaziongoza vizuri nchi zote za kusini mwa Jangwa la Sahara tukiwa Dar es Salaam, Tuna raslimali watu wa kutosha huko, pia tuna ardhi ya kutosha hapa na tunayo migogoro yetu ya ardhi ya kutosha.... tusiitafute mingine....nk.

Sababu ya kuungana inaweza kuwa na maana nje ya mifumo ya kiusalama lakini ndani ya taifa lililowekeza vya kutosha ulinzi wa mipaka yake na maslahi yake huko ugenini, mashirikiano ya namna hii hayana mashiko.

Jambo la pili Mimi ni ninapinga mkataba wa ushirikiano kati ya ulaya na afrika, ndio ninapinga, tena Tanzania imeridhia, huu ni mkataba wa kikoloni, ni njia mpya ya kuinua uchumi wa ulaya zaidi kwakutumia utajiri wetu wa Afrika, ni mfanyabiashara au mkandarasi gani kati yetu Watanzania anayeweza leo kwenda kuomba tenda Uingereza na akashinda? Huu ni ukoloni mpya, lazima wafanyabiashara na makandarasi tuamue kusimama wenyewe leo.

Niishauri serikali ya Tanzania, iendelee kuwapiga danadana hivihivi wabia wa ushirikiano wa Afrika Mashariki mpaka Yesu na Mtume Mohamed wanaporudi, pia ijiondoe kwenye mkataba wa Afrika na Ulaya, huu ni mkataba wa kikoloni.
 
Wewe utakuwa mtanzania mwenye asili ya uingereza maana baadhi ya waingereza wanataka brexit yaani kujitoa jumuiya ya ulaya, sasa mawazo hayo ya waingereza ndiyo umeyaleta hapa Tanzania kwamba na sisi tuwe na tanexit, kwa kiasi Fulani nakuunga mkono
 
hiyo kitu haiwezi kutokea africa na duniani kwa dunia ya sasa sababu watu sasa ivi wanapenda madaraka kupita kiasi
 
Mada kama hii uliyotoa yericko ina tija kwa usalama wa taifa nafurahi kuona watu watabisha kwa hoja na sio kuanza kuingiza siasa
Binafsi naweza kukuunga mkono kama nikajua na manufaa tutayopata kiuchumi kwenye hilo shirikisho ili nijue niegemee wapi
 
Back
Top Bottom