Leo ni mwezi wa tano tunakaribia kuingia wa sita,yaani tuna miezi chini ya 5 tufanye uchaguzi mkuu ambao tunatumaini utaleta msukumo mpya katika maendeleo ya nchi yetu.
1.Hatujui ilani ya uchaguzi ya vyama
Si chama tawala wala cha upinzani kilichosema kikipata ridhaa ya wananchi kushika madaraka kitafanya nini kwa nchi hii. Wananchi watapata muda gani wa kusoma na kuielewa election manifesto na kuweza kufanya maamuzi ya kuchagua chama kipi?
2.Hatumfahamu nani anatakayepeperusha bendera ya chama chochote ya kugombea uraisi
Mwaka jana, raisi wa sasa wa Msumbiji alikuja nchini akiwa ni mteule wa chama chake cha FRELIMO kugombea nafasi ya uraisi. Wananchi wa Msumbiji walipata muda ya kumtathimini na baadaye wakapiga kura ya kumchagua.
Hapa kwetu, tumeshuhudia watu wakizuiwa hata kusema nia zao za kutaka kuchaguliwa nafasi ya juu ya uongozi wa nchi yetu katika chama tawala!
Wapinzani ndo hao wako kama fisi vile. Wanasubiri masalia yatakayotemwa na chama tawala ili na wao wapate uhai. Kwa maneno mengine ni kuwa wanajifahamu kabisa kuwa uwezo wa kuongoza nchi hawana. Sana sana wanaweza jiongoza wao wenyewe tu.
Walau CUF wamejitahidi maana wameshateuwa wanaogombea nafasi za ubunge na kama kawaida,kwa upande wa visiwani, nafasi ya uraisi .ni yule yule juzi , jana, leo na hata milele
Ukitazama muda ambao chama tawala watamteua mgombea wa uraisi, hautoi muda wa kutosha kwa wananchi kumtathimini vya kutosha na uwezekano wa mdahalo utakuwa finyu maana nchi yetu ni kubwa kwahiyo kuzunguka nchi yote kunahitaji muda mwingi ambao hautakuwepo (miezi chini ya 3)
Kwa wapinzani, ni mpaka wasubiri masalia halafu wagombane weee wenyewe kwa wenyewe ndiyo tutajua nani atapeperusha bendera yao au zao (itategemea kama UKAWA bado itakuwa na pumzi ya uhai wakati huo)
Kwa jambo nyeti kama hili, mpaka leo tunakaribia uchaguzi hatujui kwa miaka mitano ijayo nani atatuongoza na atasimamia nini............Hivi tumelogwa au?