Tanzania hivi tuko kipindi cha mpito au tuna nini?

tikatika

JF-Expert Member
May 6, 2011
2,330
4,119
Yaan kila nikitafakari nakosa jibu, baada ya uchaguzi wa 2015 nilidhani kuna muda tutatulia kama taifa. Lakn ndio kwanza taifa lina hali ya sintofaham kama vile tumetoka kupinduliwa.

Ukitizama sana unaweza dhani uchaguzi utafanyika kesho, siasa zimepamba moto. Lakn ukitizama kwa jicho lingine unaweza dhani tumevamiwa na wageni tunajaribu kuwatoa katika nchi yetu. Maana mwendo tunaenda nao ni funga huyu peleka yule police, weka huyu mahabusu hakuna kutoka hadi upelelezi ukamilike.

Mtu anaweza kaa sello hata wiki asipelekwe mahakamani wakati sheria inakataza na hakuna anaye jali. Hii hali itaisha lini tuwe wote kitu kimoja tujenge nchi? Hii hali hatufiki popote.

Waliosema umoja ni nguvu hawakukosea . Walimaanisha hata maendeleo ya nchi hayawezi kuletwa na mtu mmoja.

Tafadhali watu wa serikali na wananchi kwa ujumla hii hali ya sintofaham itaisha lini?? Mimi siielewi huko mbeleni tutapoa au ndio tunazidi kuwasha moto?
 
Unahisi labda ni kwa sababu tumerithi vipandikizi vya kuomba hata tunavyostahili!? (Back to our Tz history) Au tumeamua kuangaliana!?
 
Back
Top Bottom