Tanzania has fake journalists

Nilufer

JF-Expert Member
May 10, 2012
9,565
13,540
Kwenu,
Waandishi wa Habari,

Ni bora vyombo vya habari msusie kuandika habari za Mh.Makonda watu tupumue ila Dunia na WaTanzania wote tumejua Vyombo vya Habari ndio adui wa Maendeleo ya Nchi yetu.

Vyombo karibia vyote vya Habari kuungana na Watuhumiwa wa Madawa ya kulevya kutaka kumkwamisha Mkuu wa Mkoa wa Dsm ni aibu kubwa na haijawahi kutokea!

Miaka yote mnaandika makala ndefu kwenye Magazeti,Redioni na Tv kuhusu kupambana na Madawa ya Kulevya ulikuwa ni unafiki mtupu.

Kwa hili tumejua Vyombo vya habari havina nia nzuri na Taifa letu kwa kufifisha kwa makusudi vita ya Dawa za kulevya yanayoteketeza nguvu kazi ya Taifa.

Sekta ya Habari inahitaji watu wenye Weledi wa kukemea Maovu ili Taifa lisonge mbele,kuliko sasa hivi inaonekana wanarubuniwa kiurahisi na watu wenye fedha kuandika mambo wanayotaka.
Binafsi nilisha acha kununua Magazeti muda mrefu kutokana na kuandika habari za kupika.

Mkiendelea kumsusia Mkuu wa Mkoa na sisi hatuta nunua Magazeti yenu.

Nawasilisha,
 
Kiroja kingine hiki huku...

Eti kumkwamisha Mkuu wa Mkoa... Mkuu wa Mkoa yupi?! Huyu huyu ambae alikuwa anawapa muda wauza mihadarati wapate kupoteza ushahidi kabla hawajaenda kuhojiwa na polisi?!

Una macho lakini huoni na una masikio lakini husikii!!!

Yaaani Mkuu wa Mkoa huyu huyu ambae leo anafanya live tv coverage na kutangaza "...chige nina taarifa unajihusisha na mihadarati kwahiyo Jtatu unatakiwa kuripoti Central!!"

Anasema hayo wakati kumbe ni kweli nauza mihadarati lakini kwa msaada wa RC Kilaza; amenipa fursa ya kupoteza ushahidi wote na Jtatu ninapoenda polisi nahojiwa na kukataa tuhuma za RC Bashite!! Sirro anatuma vijana wake kwenda kunipekua na wananikuta clean kwa 100%... yote hayo yamefanikiwa kwa sababu ya Ubashite!!!
Halafu ndo unasema anakwamishwa wakati amejikwamisha mwenyewe na uBashite wake!!!
 
Kwenu,
Waandishi wa Habari,

Ni bora vyombo vya habari msusie kuandika habari za Mh.Makonda watu tupumue ila Dunia na WaTanzania wote tumejua Vyombo vya Habari ndio adui wa Maendeleo ya Nchi yetu.

Vyombo karibia vyote vya Habari kuungana na Watuhumiwa wa Madawa ya kulevya kutaka kumkwamisha Mkuu wa Mkoa wa Dsm ni aibu kubwa na haijawahi kutokea!

Miaka yote mnaandika makala ndefu kwenye Magazeti,Redioni na Tv kuhusu kupambana na Madawa ya Kulevya ulikuwa ni unafiki mtupu.

Kwa hili tumejua Vyombo vya habari havina nia nzuri na Taifa letu kwa kufifisha kwa makusudi vita ya Dawa za kulevya yanayoteketeza nguvu kazi ya Taifa.

Sekta ya Habari inahitaji watu wenye Weledi wa kukemea Maovu ili Taifa lisonge mbele,kuliko sasa hivi inaonekana wanarubuniwa kiurahisi na watu wenye fedha kuandika mambo wanayotaka.
Binafsi nilisha acha kununua Magazeti muda mrefu kutokana na kuandika habari za kupika.

Mkiendelea kumsusia Mkuu wa Mkoa na sisi hatuta nunua Magazeti yenu.

Nawasilisha,
angalia nitakuweka kwenye list ya madawa ya kulevya kiniudhi.
 
Back
Top Bottom