"Tanzania hamna press" ni usemi unaojirudia rudia hapa JF, haswa ukipendwa kutumiwa na mwenzetu Kuhani, ambaye ni mtu makini sana na amechanganua kwa urefu na mapana mengi ambayo huwa mara nyingi yanasemwa na kuandikwa bila kupingwa au kukosolewa hapa jamvini.
New Media ikihusisha ma-blog na social networks imewezesha kuunganisha watu wengi ukiachilia mbali kuwahabarisha watu katika karne hii ya 21. Tukikubali kuwa Tanzania yetu bado iko nyuma sana ki-teknolojia, hata hii ya TEKNOHAMA (habari na mawasiliano) ambamo imeonekena kusogea mbele zaidi.
Sasa wanaJF, ili kuepukana na usemi huu kubadilika kuwa 'buzzword', yakuwa Tanzania hamna press hivyo kuhalalisha mengi ambayo yanaweza kuongelewa kuhusiana na Tanzania bila kupingwa au kuishia kupuuziwa; naomba tuuangalie 'usemi' huu kiundani zaidi kwa kujiuliza maswali yafuatayo:
---Je, ni kweli Tanzania hamna press?
---Kama Tanzania hamna press, je kuna critics wa hiyo press?
---Je, kuna aina za press?
---Kama kuna aina tofauti tofauti, zipi ziko juu na zipi zimedumaa?
---Kama Tanzania hamna press ni kipi kifanyike kuleta hiyo press?
Naomba kuishia hapa kwa sasa. Asanteni.
SteveD.
Kuhusu ndege ya Maliasili iliyoanguka na kuua, mtangazaji wa Taarifa ya Habari ya Tanzania Broadcsting Corp. ya saa 2 usiku EAT, July 4, 2008, amesema mara tatu, Watumishi watatu wa Wizara ya Maliasili wamekufa papo hapo baada ya ndege kuanguka..."
Sasa, hii ndege ilipotea kwanza, na hakuna aliyeshuhudia wanakufa papo hapo.
Hako katofauti kana umuhimu gani?
Inawezekana Marehemu walighalaghala porini dakika, hata masaa kadhaa, bila msaada ambao ungeweza kuwaokoa. Hujui walikufa hapo hapo.
Katika nchi zilizoendelea, kushindwa kusaidia walioofikwa na maafa kama wangeweza kuokolewa ni skandali kubwa. Tanzania hatujafika kuwa na uwezo wa kufikia kwa haraka kwenye kila pori kuokoa watu.
Lakini usisema kwamba walikufa papo hapo. Hujui.
Sasa hii taarifa ndio Watanzania millioni 40 wamesomewa jioni ya leo!
Cheesy press!
Watanzania millioni 40 - 1 aliyesoma = Watanzania 39,999,999
Watanzania millioni 40 - 1 aliyesoma = Watanzania 39,999,999
Kuhani nimeamua kukuchokoza tu mkuu wangu...
Watanzania millioni 40 - 1 aliyesoma = Watanzania 39,999,999
Kuhani nimeamua kukuchokoza tu mkuu wangu...
SteveD,
Yule msomaji mmoja pale anasoma kitu alichotaarishiwa na Wahariri na Waandishi wengine wa Tanzania Broadcasting Corp.
Kwa hiyo TBC nzima wamepotosha Watanzania millioni 40 - staff ya TBC - myself ≠ 39,999,999.
Nimeipenda hiyo ila umesahau - watoto waliokuwa wamelala, na wasio kuwa na radio, au TV au mawe (batteries) ili kusikiliza radio na radio ya kijiimefungwa mwenyekiti hayupo leo. Lol
Hapa unaweza kusema kwamba nina justify notion kuwa Tanzania hamna press, hapana. Najaribu kujenga kesi kuwa, iwapo unajua fika kwamba Tanzania haina air ambulances, haina medical resource n.k. nzuri za kufikia matukio ya ajali, iweje sasa mwana habari aripoti kwa precise data wakati mazingira yake hayamruhusu?
Jamani mimi naona mnawalaumu mno kupita kiasi. Sidhani kama wana nyenzo/ resources zitakazowawezesha kufanya kazi yao kwa umahiri. I think some of you are being overly critical. I'll cut them some slack given that we're a third world country....
...huu ndiyo msimamo wako kwa sasa, daima au? je hii ni criticism inayofaa au ili kuwa mahiri tunatakiwa kuchukulia kila jambo na mazingira yake kuliko ku-paint kila kitu with the same brush?After what happened with Wangwe and the controversial coverage of the story ni ubabaishaji mtupu hapa Bongo.
Nyenzo gani? Kwani tunaongelea mainjinia hapa wanaojenga madaraja au madaktari wanaofanya upasuaji?
Nyenzo gani wanahitaji hawa waandishi, kujua kuandika kunahitaji nyenzo zaidi ya ubongo mzuri na kujua kuutumia? Unataka kusema hawana vitabu? Au wanahitaji vitabu kujua kuwa mnapo fake kuandika habari tatu tofauti kutoka katika script moja you have to at least change it up a little?
...huu ndiyo msimamo wako kwa sasa, daima au? je hii ni criticism inayofaa au ili kuwa mahiri tunatakiwa kuchukulia kila jambo na mazingira yake kuliko ku-paint kila kitu with the same brush?
SteveD.