Tanzania haishushwi Uchumi wa Kati na taasisi ya Moodys. Bado Tanzania yaipiku Kenya

kapyela

Member
Feb 13, 2013
11
8
TANZANIA HAISHUSHWI UCHUMI WA KATI NA TAASISI YA MOODYS. BADO TANZANIA YAIPIKU KENYA!

HOJA TISA (9) KUWEKA SAWA MJADALA RIPOTI YA MOODYS YA AGOST22, 2020

Na David KAFULILA

Baada ya Taasisi ya kimataifa ya MOODYS kutoa ripoti yake jana kuhusu uchumi wa Tanzania kumejitokeza mjadala ambao nimeona usinipite bila kuchanga maoni yangu.

Baada ya kupitia maoni ya walio wengi, naomba niseme mambo tisa(9) kwa afya ya mjadala huu;

Kwanza niseme tu kwamba Taasisi na Serikali nyingi duniani zinazoendeshwa kisasa duniani hulipia tathimini hizi kama njia kupata mikopo katika masoko ya kimataifa. Na tangu tupate uhuru, ni awamu ya 5 iliyofanikisha kufanyiwa tathimini hii ambayo kwa mara ya kwanza ilifanyika mwaka2017.

Pili, ni suala la ufahamu kwamba duniani kuna taasisi hizi( credit rating agencies)zaidi ya 70 kimataifa zinazofanya kazi ya kupima uwezo wa kiuchumi wa Serikali, Mashirika na Kampuni kuweza kukopa hasa kwenye masoko ya kimataifa.Taasisi hizo zinaitwa CREDIT RATING AGENCIES!

Tatu ni suala la ufahamu tena kwamba ingawa Taasisi hizo zipo zaidi ya 70 duniani, lakini asilimia 95% ya kazi hizo zinafanywa na Taasisi3 tu, ambazo ni MOODYS, STANDARD& POOR NA FITCH.

Hivyo Serikali au Shirika likifanyiwa tathimini na moja kati ya taasisi hizo matokeo yake huheshimika zaidi.

Nne ni suala la uelewa tena kwamba Taasisi hizi hazihusiki kupanga madaraja ya uchumi wa nchi kwamba nchi fulani itakuwa uchumi wa juu au uchumi wa kati au uchumi wa chini.

Bank ya dunia ndio inapanga madaraja hayo. Taasisi hizi hazihusiki. Hivyo kusema kwamba Ripoti ya Moodys imeshusha Tanzania kutoka uchumi wa kati nikuchanganya madesa kwa lugha ya chuo.

Tano, Ndio sababu ripoti ya MOODYS ya April2017, iliipata Tanzania daraja la B1 juu ya nchi zote za Afrika Mashariki zilizokuwa na B2 ingawa Tanzania ilikuwa haijaingia uchumi wa kati ilhali Kenya ilikuwa tayari uchumi wa kati.

Habari ya Tanzania kuipiku Kenya kwa tathimini ya MOODYS ilizua mjadala nchini Kenya ( Rejea Gazeti la DailyBusiness nchini Kenya la April4,2017).

Sita, ingawa ripoti ya MOODYS ya April2017 ilitupa B1 lakini ilitupa alama hasi ( negative outlook) kwasababu ya kutokubaliana na msimamo mkali Sekta ya madini nchini.

Saba ni ukweli kwamba ingawa Tanzania imepewa daraja la B2 Agost22, 2020 kutoka B1Aprili2017 , bado Tanzania ipo mbele ya mshindani wake kibiashara Kenya. Kenya imebaki na B2 ya mwaka2017 lakini ameshuka kwa kupata alama hasi ( negative outlook 2020 kutoka positive outlook mwaka 2017) wakati Tanzania ikiwa na B2 chanya( Positive outlook).

Nane, katika Afrika mashariki, ingawa Kenya inaongoza kwa uchumi mkubwa lakn umadhubuti wa uchumi kumudu kukopa kwa vigezo vya MOODYS, Tanzania bado inafanya vizuri kuliko Kenya na hakuna nchi Afrika mashariki yenye daraja kubwa kwa afya ya uchumi kuliko Tanzania kwa mujibu wa MOODYS.

Tisa na mwisho nimalizie kujibu hoja ya kama matokeo ya taasisi hizi yanaweza kupingwa au kuwa na kasoro;

Prof. Mathew Occra, gwiji la uchumi duniani alipata kusisitiza kwamba ripoti za taasisi hizi pamoja na heshima yake bado ni maoni yanayoweza kukosolewa.

Ndio sababu kufuatia mgogoro mkubwa wa kiuchumi mwaka 2008, Marekani ilizitoza faini kiasi cha $864m kutokana na kukosea tathimini zake.

Vivyo hivyo hata kwetu Tanzania, mwaka 2017 ingawa zilitupa daraja kubwa kuliko nchi yoyote Afrika mashariki, lakn ilitupa alama hasi ( negative outlook) kutokana na hatua kali za Serikali dhidi uwekezaji sekta ya madini.

lakini ukiangalia kiuhalisia, leo Tanzania inafanya vema zaidi katika sekta ya madini kulinganisha na tulikota kutokana na mbinyo uliowekwa na JPM katika sekta hiyo.

Mauzo ya dhahabu pekee yameongezeka kwa zaidi ya $800 kutoka $1.3bn mwaka 2015 mpaka $ 2.13bn- Rejea BoT reports 2016&2020
 
Sikuwahi kujua kuwa kwa mujibu wa wanaccm SI unit ya Tanzania ni Kenya.But kitu pekee ninachojua ni kwamba Tanzania ina resources nyingi kuliko Kenya.Tumekosa viongozi tu otherwise SI unit yetu ilipaswa iwe nchi mojawapo ya ulaya au america
 
Sikuwahi kujua kuwa kwa mujibu wa wanaccm SI unit ya Tanzania ni Kenya.But kitu pekee ninachojua ni kwamba Tanzania ina resources nyingi kuliko Kenya.Tumekosa viongozi tu otherwise SI unit yetu ilipaswa iwe nchi mojawapo ya ulaya au america
Lazima utambue kuwa Kenya kwa Afrika mashariki inafanya vizuri. uchumi wa kenya unategemea sana biashara ya kimataifa. hata hapa kwetu Tanzania Kenya ndio nchi iliyowekeza zaidi kwa takwimu hizi utakubaliana nami kwanini kenya iwe reference yetu kwa nchi za Afrika mashariki.
 
Back
Top Bottom