Kafulila: Kwa mara ya kwanza chini ya Rais Samia Tanzania imefanyiwa Tathimini na International Credit Rating Agency na kuibuka Vinara

CM 1774858

JF-Expert Member
May 29, 2021
5,084
4,301
IMG-20240510-WA0199.jpg

" Chini ya awamu ya sita kwa mara ya kwanza katika historia ya Tanzania tumefanyiwa Credit rating ( solicited ) kama Taifa.

Hata hivyo Tanzania tumefanya vizuri zaidi kuliko nchi zote za Africa Mashariki EAC na baadhi ya nchi nyingi za SADC tukiwa vinara kwa B+.

Tathimini hiyo iliyofanywa na taasisi maarufu na zakuaminika zaidi duniani za MOODY'S na FITCH ambazo pia ni vinara duniani katika kazi hiyo,

Huu ni ushahidi kuwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan anajenga uchumi wa kisasa na kuiweka nchi kwenye mizania bora zaidi ya kupimika kiuchumi kwenye medani za uchumi kidunia"

Amesema hayo David Kafulila, Mkurugenzi wa Kituo cha UBIA kati ya Serikali na Sekta Binafsi ( PPP) wakati akihojiwa kwenye kipindi cha DK 45.

Kafulila ameongeza kwamba Tathimini hizi zinachangia na kuongeza zaidi imani ya uwekezaji na wakopeshaji kwani zinapima afya ya uchumi wa nchi yetu kwa uhuru na uwazi zaidi.

Mkurugenzi David Kafulila anaendelea kwa kusema, nadhani inafahamika kwa wote hata katika benki zetu za kawaida tu kwenye mikopo ya kibiashara,

Wewe ukiwa imara kiuchumi ukienda benki kukopa watakukopesha kwa masharti nafuu zaidi kuliko ukiwa hoi kiuchumi (desperate) ambapo utaambulia masharti magumu kama ya mikopo ya kausha damu.

Hongera kwake Rais wetu Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa na nzuri anazozifanya katika kusisimua na kukuza uchumi wetu.

Changamoto ni nyingi ni kweli lakini nchi ipo kwenye mstari sahihi na inazidi kuchukua sura mpya katika ujenzi wa uchumi wa soko kikanda na Kimataifa "

Uchumi unapaswa uteremke chini that is all
Bila shaka ndio unaelekea chini, Uchumi wetu bado uko Pyramidal in structure ndio maana unaona huko juu Matajiri ni wachache wakati huku chini masikini ni wengi.

Kadiri muda unavyosogea ndio watu wengi zaidi watafikiwa na ukuaji huu wa kiuchumi.
 
2025 hakuna haja ya Uchaguzi, Tusichezee Fedha za Umma, Rais ni Samia kwa zaidi ya 83%
 
  • Thanks
Reactions: Tui
=====
"Chini ya awamu ya sita kwa mara ya kwanza katika historia ya Tanzania tumefanyiwa Credit rating ( solicited ) kama Taifa.

Hata hivyo Tanzania tumefanya vizuri zaidi kuliko nchi zote za Africa Mashariki EAC na baadhi ya nchi nyingi za SADC tukiwa vinara kwa B+.

Tathimini hiyo iliyofanywa na taasisi maarufu na zakuaminika zaidi duniani za MOODY'S na FITCH ambazo pia ni vinara duniani katika kazi hiyo,

Huu ni ushahidi kuwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan anajenga uchumi wa kisasa na kuiweka nchi kwenye mizania bora zaidi ya kupimika kiuchumi kwenye medani za uchumi kidunia"

Amesema hayo David Kafulila, Mkurugenzi wa Kituo cha UBIA kati ya Serikali na Sekta Binafsi ( PPP) wakati akihojiwa kwenye kipindi cha DK 45.

Kafulila ameongeza kwamba Tathimini hizi zinachangia na kuongeza zaidi imani ya uwekezaji na wakopeshaji kwani zinapima afya ya uchumi wa nchi yetu kwa uhuru na uwazi zaidi.

Mkurugenzi David Kafulila anaendelea kwa kusema, nadhani inafahamika kwa wote hata katika benki zetu za kawaida tu kwenye mikopo ya kibiashara,

Wewe ukiwa imara kiuchumi ukienda benki kukopa watakukopesha kwa masharti nafuu zaidi kuliko ukiwa hoi kiuchumi (desperate) ambapo utaambulia masharti magumu kama ya mikopo ya kausha damu.

Hongera kwake Rais wetu Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa na nzuri anazozifanya katika kusisimua na kukuza uchumi wetu.

Changamoto ni nyingi ni kweli lakini nchi ipo kwenye mstari sahihi na inazidi kuchukua sura mpya katika ujenzi wa uchumi wa soko kikanda na Kimataifa.

View attachment 2998488
===
Kafulila mwamba sana ila atakuwa bora zaidi akiwa Bungeni
 
Back
Top Bottom