Tanzania haina utamaduni

Tanzania haina utamaduni

Glasnost

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2017
Posts
266
Reaction score
259
Hakuna kitu kinaitwa utamaduni wa Mtanzania. Kumekuwa na tabia ya wananchi kuamini kuwa Tanzania ina utamaduni na hasa pale jambo fulani linapotokea au katika njia ya kuhamasisha, kutetea na hata kutambulika katika nyanja tafauti hapa duniani. Kwa hivyo jambo lolote linapofanyika basi mtu huweza sema kwamba, “huo si utamaduni wetu” bali ni tabia za kuiga lakini ukitazama unagundua kuwa tuna tamaduni nyingi tu na hivyo mtu huwezi sema kwamba, “ huyu amevunja utamaduni au kakiuka mila zetu”.

Sheria za kukandamiza sanaa kama kufungia miziki, filamu, magazeti, mitandao ya kijamii kama njia ya kupunguza vitendo hivyo ni kutojua tulipotoka na tunapokwenda.

Uelewa mdogo wa watunga sheria,wananchi, viongozi wa dini katika kufanya maamuzi ni tatizo liliota sugu na umefika mda wa kukemea na kufuta fikra hasi juu ya nini hasa maana ya utamaduni. Hapa kila kiongozi lazima atetee filosofia yake lakini ukweli ni kwamba aidha kwa upande wa dini au desturi za ughaibuni, mashariki ya kati na Asia sio tamaduni zetu. Fursa zinapotea kwa visingizio vya ajabu kwa kutunga na kutumia sharia za ughaibuni na nchi zisizo na mwingiliano au ukaribu wa aina yoyote.

Suala la kodi ambalo serikali zilizopita na ya sasa zimekuwa zikipigania na kuakikisha zinatekelezeka, wakati ndio huu wa mabadiliko yenye chanya na sio sharia kandamizi na maamuzi hasi kwa taifa huru. Sanaa itakuwa kimbilio la wawekezaji wa ndani na nje pia wanafunzi watavutiwa kusoma, kufanya sanaa kama kazi yenye kipato toshelezi na ya kueshimika.

Suala la uchi. Mila na desturi za makabila mengi hapa Tanzania kuhusu uchi au nusu uchi halijawahi kuwa tatizo, kwa mfano kwa mwanamke kuwa matiti wazi sio kosa au uvunjivu wa maadili na desturi. Lakini leo hii tunaona vyombo vya habari wakiziba na hata kutoonyesha kabisa kipande cha sehemu hiyo. Swali la kujiuliza hapa je ni ukweli huu ni uvunjifu wa utamaduni wa Mtanzania au ni utamaduni kutoka nchi za kigeni?

Lugha kutotumika ipasavyo na hapa nazungumzia lugha ya taifa Kiswahili kwenye ya utangazaji wa habari, sanaa, uandishi wa vitabu. Lugha bado ina vikwazo vingi. Mtu unasoma kitabu cha mapenzi au cha stori ya kufikirika lakini unakuta mtunzi anatumia maneno yasiyovutia, ni kama anazungumza na mtoto wake au wazazi wake. Sote tunajua kuwa mtu anapokuwa na hasira lugha huwa na maneno makali na pia katika mapenzi, wapenzi utumia maneno tafauti katika kupendesha mapenzi yao au kumvutia mwenzake.

Tuache kudanganyana kuhusu utamaduni wa mtanzania. Leo hii sharia nyingi hazina sura ya utanzania bali uigaji na utumwa wa kuabudu mila na desturi za wengine na kudhani ndio utaratibu sahihi. Suala la ndoa za kimila la kuwa na mke zaidi ya mmoja ni suala la kutambulika na katiba ya nchi hii na mambo mengine mengi tu. Tusiishi kwa kumfurahisha mtu au watu fulani huku tukipoteza tamaduni zetu na kuona ni sawa kabisa.

Wakati umefika kutumia lugha ya Kiswahili ipasavyo bila vikwazo kwa visingizio vya kukiuka maadili, mila na desturi.
 
Back
Top Bottom