Kuwa omba omba ni kubaya sana. Ukiwa omba omba kimsingi lazima uwe M.A.L.A.Y.A pia kwani kila utakayemuomba analo atakalotaka kwako! utamkatalia? Sasa hali inaanza kuwa dhahiri shahiri kuwa wale tunaowaomba huwa hawatupi kwa moyo mweupe. Wanataka vile vile tufuate na ustaarabu wao, kwani ikiwa sisi tungekuwa wastaarabu, kwa nini tuwaombe wao?
Ni lazima tujifunze kujitawala wenyewe kwa kutumia rasilimali tulizonazo wenyewe! Tukishindwa, tuwe tayali kwa mambo kama haya. Tujiulize ni kwa nini good governance inatushinda, fedha zetu tunatapanya kwenye starehe za viongozi tu?
Hayo ni matusi madogo, bado tutatukanwa makubwa zaidi, ikiwa hatuwezi kusafisha nyumba zetu!! Kujitegemea ni neno ambalo tumelizika na ujamaa.
Huwezi kulishwa kila siku kwa miaka 50, ukatarajia anayekulisha akuheshimu! Tuamke usingizini.