Tanzania govt on Homosexuality: We can do without UK aid | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania govt on Homosexuality: We can do without UK aid

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by EMT, Nov 3, 2011.

 1. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #1
  Nov 3, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280  Mh Membe leo amekutana na waandishi wa habari kutujulisha yaliyojiri kwenye mkutano wa Jumuiya ya Madola uliofanyika huko Australia hivi karibuni. Mh Membe ametoa tamko dhidi ya kauli iliyotolewa na Waziri Mkuu wa Uingereza ya kutishia kusitisha misaada ya kiuchumi kwa nchi za Jumuiya ya Madola zinazopinga suala la mahusiano ya watu wa jinsia moja.

  Mh Membe amesema Katiba ya nchi inatambua familia kwa maana ya mahusiano ya kijinsia kati ya mume na mke na si vinginevyo. Amesema pia jadi na utamaduni wa Watanzania unaruhusu uhusiano wa mwanaume na mwanamke tuu na si vinginevyo. Mh Membe amesema Tanzania haikubaliani kwa namna yoyote ile na kauli ya Cameron na kwamba tutakuwa tayari hata kujitoa kwenye Jumuiya ya Madola kama Uingereza itashinikiza Tanzania itambue mahusiano ya watu wa jinsia moja.

  UPDATE 1:

  Balozi kapiga mkwara! Nov 4, 2011

  UPDATE 2:

  From Reuters 4th Nov. 2011

   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 2. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #2
  Nov 3, 2011
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Mwnyekiti wake vp anasemaje ama ndio anachekacheka tu hata kwenye isue serious kama hii. Ok Membe mzuri sn kwa porojo, isue ya Gaddaf alisemaje na ikawaje? Bendera gan inapepa sasa hv, UK tutaipinga kwa nguvu ya umma na si hii serikali legelege na dhaifu haiwezi kupinga.

  Tutumiea nguvu ya umma, tena kesho tuandamane na kuchoma bendera za uwngereza kuonyesha msisitizo!
   
 3. K

  Kapwani JF-Expert Member

  #3
  Nov 3, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 668
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Haya angeyasema kule kule australia alipokuwa nao hao watoa hoja.....kuja kutueleza sisi huku haisaidii hata kidogo , alitakiwa asimame hadharani kupinga hoja hii lakini kule kule, ukute kule alikuwa mdogoo kama piritoni ametua hapa anajitutumua!

  mix with yours
   
 4. F

  FUSO JF-Expert Member

  #4
  Nov 3, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,860
  Likes Received: 2,338
  Trophy Points: 280
  kumbe wazungu washatuona sisi mazezeta -- yaani kitendo cha kutuambia kama hatutaki ushoga tusiwaombe hea ni dharau kubwa sana, kama mwalimu angekuwapo basi huyu balozi wa nchi iliyotamka angepewa masaa 24 awe ametimka.

  Yoote tufanyieni lakini na hili la ushoga jamani? kaaaa.... sasa mmefika mbali - kama ni hela basi wacha tufe na umaskini wetu.
   
 5. F

  FJM JF-Expert Member

  #5
  Nov 3, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Membe na wenzake wanataka tuache kuongelea madudu wanayofanya badala yake tujikite kwenye kauli za wakina Camoroon. Ni siku ya ngapi sasa tangu Cameroon atoe hiyo kauli? na serikali hii haina historia ya kufanya maamuzi magumu kwa hiyo asitupotezee muda na madai kuwa 'watajitoa' kwenye umoja wa madola! Wana huo ujasiri?

  Watu hawana mishahara na miradi ya barabara imekwama.
   
 6. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #6
  Nov 3, 2011
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,318
  Likes Received: 610
  Trophy Points: 280
  Isije ikawa msimamo kama alioutoa wakati walibya walipopandisha bendera yao ubalozini Dar. Sijui msimamo wa serikali yetu ni upi kuhusu Libya leo hii. They are reputed for a serious lack of principles and consistency. Sitashangaa sana kesho wakigeuka na kusema mashoga nao wana haki zao sawa na binadamu wengine.
   
 7. K

  Kapwani JF-Expert Member

  #7
  Nov 3, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 668
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mmmmh ina maana ishu ya ushoga ndio ishu pekee iliyoletwa na waingereza inayoboa? tungekuwa na msimamo kama huu kuupinga ubeberu wao toka awali 1961 na kuendelea tusingefika hapa......tumezoea kuwalamba miguu kwa kila kitu tukiamini misaada yao ndio itakayotuoa na athari yake ndio hiii.....kilichotakiwa kupingwa kutoka awali ni dhana ya utegemezi, yanayondelea sasa ni makandokando ya utegemezi

  mix with yours
   
 8. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #8
  Nov 3, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Guys Membe is another joker do not take him serious an opportunist MP na Waziri.Alitakiwa kukatalia kule kule then tusome juu kwa juu .Leo anaueleza hapa ina maana mkutano mzima issue ilikuwa hii pekee ?Haya ile change anayotaka hajui kwamba walifanya biashara na mashoga ? ipi misaada ya Ulaya anaelewa vyanzo yake vya kodi ni vipi ?Aaache zake hapa huyu .
   
 9. MKWECHE

  MKWECHE JF-Expert Member

  #9
  Nov 3, 2011
  Joined: Apr 8, 2011
  Messages: 299
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Misaada kama misaada haina shida!Kibaya ni Masharti ya misaada Husika,kama masharti yanalenga kulazimisha Nchi Idharau misingi ya Heshima,Utu na Haiba ya watu wake basi misaada hiyo ni ya Kijinga na si ya kuipokea wala kuikubali!"Mtu mwenye akili akikuambia kitu cha Kipumbavu wakati akijua na wewe unaakili timamu ukakikuba anakudharau!JK
   
 10. Washawasha

  Washawasha JF-Expert Member

  #10
  Nov 3, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,689
  Likes Received: 410
  Trophy Points: 180
  safi kabisa huyu Mr.Gay Cameron anataka kutuletea uchizi wa kwao huko si akabanduane yeye na baba yake kama kamchezo hiko anakapenda.Poor Cameron.Na log off
   
 11. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #11
  Nov 3, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Kwa hili I second you mr Membe ingawa huaminiki so what is plan B kushusha bendera ya ma-gay wa uingereza?
   
 12. Invarbrass

  Invarbrass JF-Expert Member

  #12
  Nov 3, 2011
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 505
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Najua Cameron hakunilenga mimi maaana siombi msaada. Kazi kwenu watembeza bakuli.
   
 13. TOWNSEND

  TOWNSEND JF-Expert Member

  #13
  Nov 3, 2011
  Joined: May 8, 2011
  Messages: 2,597
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  Kwanini mlikubali kuhongwa suti? Naanza kupata picha
   
 14. Invarbrass

  Invarbrass JF-Expert Member

  #14
  Nov 3, 2011
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 505
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Ombaomba huwa wanadharilika kamuulize matonya nani alimtoa Dar.
   
 15. Jumakidogo

  Jumakidogo R I P

  #15
  Nov 3, 2011
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 1,859
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Membe hizo ni kelele za chura. Ubavu wa kujitoa jumuia ya madola unao? Mi naona pengine hata safari za JK kwenda kuomba omba zitapungua. Kumbe wanaendaga huko kujipendekeza wenzao huwa wanawatamani.
   
 16. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #16
  Nov 3, 2011
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Mkuu we acha tu inauma sana serikali ya magamba zote ni legelege, baada ya mwalimu, mwnykiti anaenda UK anarudi anajisifu wafadhili wamekubali kuongeza misaada. Rais anaenda kuomba msaada unategemea nn?
   
 17. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #17
  Nov 3, 2011
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  membe bwana anachekesha sana... ana ubavu wa kuipinga UK? ...lazima serikali itambue mapunga na yapewe viti maalumu bungeni
   
 18. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #18
  Nov 3, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Hapo kwenye red pitia huu uzi: https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/188720-bravo-jk-kuwatolea-nje-balozi-shoga-wa-uingereza.html
   
 19. Washawasha

  Washawasha JF-Expert Member

  #19
  Nov 3, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,689
  Likes Received: 410
  Trophy Points: 180
  Mzee Yusufu Makamba ndiye aliyemkimbiza Matonya Dar. ina maana wazungu ndio wanatufukuza kwa ule usemi "AKUFUKUZAYE HAKUAMBII TOKA" wao wanajua nchi nyingi za kiafrika zitapinga na ndio urafiki utakapoishia hapo.Nalitafuta sana tamko la Zimbabwe mwenye nalo alibwage hapa.Na log off
   
 20. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #20
  Nov 3, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Hivi wao waingereza wana viti maalumu vya gays?
   
Loading...