Tanzania govt on Homosexuality: We can do without UK aid

Nikitilia shaka kuwa Camerun ni SHOGA,hakuna atakae kataa moja kwa moja kutokana na kauli yake..
Hawa wanalengo la kupotezea muda tu jamani..
Tuache kujadili mambo ya msingi kama UMEME,MALARIA, NJAA,UPATIKANAJI WA MAJI SAFI,NJIA ZA UCHUKUZI,MAKAZI BORA,AFYA na mengine kama hayo,tuanze kuzungumzia UCHOKO(USHOGA)
tuachane na vichaa wa kiingereza hawa..
2jadili UFISADI NA wizi ulikithiri nchini mwetu..
 
Wewe utakuwa Mjinga kweli; Issue ya Mashoga ni sababu wengi wanakimbilia Uingereza kuogopa kuuwawa, ni sawa sawa na wakati Zeruzeru wetu walivyokuwa wanakimbilia Uingereza

Serikali inatakiwa kuweka sheria kali za Uraia; sasa hivi kila mtu ana haki mkononi mnamshika Mwizi mnamuua kwa kumuwekea tairi kiunoni

Sheria za Mwananchi lazima zizingatiwe na sio kuruhusu Ushoga; Jamani endeleeni kimaisha Watanzania!!!

It is their Tax Money anyways they can do whatever with their Money: Tanzanians we should clean our house get rid of FISADI's we have enough Minerals and GAS to build our country we really don't need them British it is NEO-COLONIALISM
 
Ukoloni lengo lake kubwa lilikuwa kugawana resources zetu. kwa maana ya ardhi, madini... Kulaani ushoga ni kumiss target. Tukatae dhana nzima ya wazungu kutuona sisi ni mazuzu. Na sasa tuandae kikao cha commonwealth hapa afrika na tuwaambie, everyone for her/himself and the hardway is the only way. SAWASAWA?
 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe alitoa msimamo huo leo Jijini Dar es Salaam akisema huko ni kwenda kinyume na sheria na utamaduni wa nchi yetu inayotambua ndoa ya mme na mke kama kiini cha familia.

Alitoa msimamo huo kufuatia kauli ya Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron kuwa wana mpango wa kusitisha misaada kwa nchi ambazo katiba na sheria zake hazitambui mashoga na ndoa zao.

"Nchi yetu inaheshimu sheria na utamaduni wake hivyo hatupo tayari nchi nyingine kutuwekea masharti kama hayo ya kuwa na uhusiano wa jinsi moja, hili ni tamko hatarishi linaloweza kuvunja uhusiano na nje", Waziri Membe aliwaambia waandishi wa habari.
 
ntafurahi wakianza kwanza na jumba la malkia tusikie kwanza mjukuu wa malkia kafunga ndoa ya kishoga ndo wengine tufuate
 
Wewe utakuwa Mjinga kweli; Issue ya Mashoga ni sababu wengi wanakimbilia Uingereza kuogopa kuuwawa, ni sawa sawa na wakati Zeruzeru wetu walivyokuwa wanakimbilia Uingereza

Serikali inatakiwa kuweka sheria kali za Uraia; sasa hivi kila mtu ana haki mkononi mnamshika Mwizi mnamuua kwa kumuwekea tairi kiunoni

Sheria za Mwananchi lazima zizingatiwe na sio kuruhusu Ushoga; Jamani endeleeni kimaisha Watanzania!!!

Watanzania tumeendelea kimaisha tatizo ni huyu ccm mwanga na mchawi mkubwa. hizi sheria kali za uraia mbona tunazo, jinsi tunavyo waadhibu waarifu wetu inaendana na maadili na mazingira yetu, hatuitaji kufuata hayo unayoyaona huko ughaibuni uliko wewe.

Hao unaowasifia wanatumia mihela mingi sana kupambana na waarifu kwa vile wanajifanya kuwaadhibu waarifu eti ni kinyume cha haki za binadamu kwa hiyo miarifu yao inaua ovyo ovyo na inawekwa ndani miezi michache tu na baadae iko mitaani, wana tatizo la vijana walevi wa pombe, madawa na bangi, ambao hawafanyi kazi yoyote lakini wanapewa social benefit, mapolisi kucha kuchwa wako mabarabarani na mitaani kudhibiti hao wahuni wa social, police hawana mamlaka yeyote maana wahuni na waarifu wana haki kuliko police wenyewe. Hayo sisi hatuyawezi kwanza hatuna hiyo miela ya kuchechezea namna hiyo.

Sasa kama ili kuwepo jumuia ya madola ni lazima tuwe mashoga kama wao basi hakuna haja, kama tulikubali kula nyasi ili ndege ya mkulu wetu inunuliwe hili la mashoga tuko radhi hata kula mchanga.
 
Mh Membe:

Ubabe, vitisho, na kauli za kukurupuka kama kawaida kutoka kwa Bw Membe!

Hivi Tanzania tukijitoa kwenye Jumuiya ya Madola ni nani au nchi zipi zitaumia? Tanzania kwa jinsi uchumi wake ulivyo mdogo, siasa zake za ufisadi, na rushwa iliokithiri, na misaada inayopewa kila kukicha; tayari ni mzigo mkubwa kwa Jumuiya ya Madola.

Ni vipi Mh Membe aone kuwa kuna yoyote wa kutishika kuhusu Tanzania kujitoa Jumuiya ya Madola

Tukijitoa jumuiya ya madola tutakuwa tunajiumiza wenyewe na tutawapunguzia mzigo Jumuiya ya Madola.
 
Angeisema vipi hadharani na haikutolewa hadharani? Search mtandaoni uoneshe ni wapi palikuwa na press conferense au kikao chenye kujadili hilo.
 
Isije ikawa msimamo kama alioutoa wakati walibya walipopandisha bendera yao ubalozini Dar. Sijui msimamo wa serikali yetu ni upi kuhusu Libya leo hii. They are reputed for a serious lack of principles and consistency. Sitashangaa sana kesho wakigeuka na kusema mashoga nao wana haki zao sawa na binadamu wengine.

Msimamo wa Serikali kuhusu Libya haujabadilika. Pita pale ubalozini ukajionee. Kuhusu ushoga nashauri mtafute Mbunge alipeleke Bungeni kama hoja binafsi au liibue wewe kwenye mchakato wa Katiba unaokuja utapata majibu ya watanzania ikiwa ni kimbelembele au kukurupuka kwa Membe au ni matakwa na maoni ya wananchi wa tanzania.
 
Kwanza sijui tunafaidika na nini kuwa mwanachama wa CW zaidi ya kujikumbusha jinsi walivyokuwa wanatesa babu zetu huko nyuma. Ni wakati sasa inabidi waafrica tucheze mchezo wenyewe haya mambo ya kukaa tunategemea mkoloni kila kitu hatufiki popote.
 
nini faida ya kuendelea kuwa chini ya jumuia hii inayoongozwa na taifa lililobomoka maadili kabisa, si mwanzo wa kufanya hivi ni mwendelezo na ni sera zao za kudumu juu ya waomba misaada.

Tukumbuke kanisa la anglican makao makuu yake ni UINGEREZA na makao makuu ya kanisa hili walishaweka masharti kwa makanisa yanayotaka kupata msaada lazima waruhusu wachungaji na maaskofu mashoga na ikaleta ntafaluku mkubwa leo si tu kwa kanisa bali wamekuja na nchi kwa ujumla na wanalazimisha kuingiza kwenye sheria zetu za nchi nahofu mbeleni serikali ikishindwa kulipa mishahara ya watumishi wake wanaweza wakashinikiza kuwa kila anayetakiwa kulipwa mshahara lazima awe shoga na wataendelea mpaka kila nyumba lazima kuwe na shoga ..e.t.c

cha msingi ni kujitoa na shetani mwingereza kwani hawana maana zaidi ya kuleta vita na washirika wake NATO katika nchi zetu na kupora rasilimali zetu
 
Hebu na tutoke na kama ningeweza ningeanzisha hata maandamano ya kuwapinga mabwabwa haya na ikiwezekana tuwafukuze hata raia wake waishio hapa kwetu. Nyambafu zao na naniliu zao kabisa! Wanataka kutubashia!?
 
Umasikini hasa wa mawazo ndio shida yetu kubwa kama taifa.

Hawa wazungu wanaona mkuu wetu wa nchi alivyo desperate kuzunguka kuomba misaada! Kila akipata upenyo wa kukutana na matajiri hawa basi ni kuomba misaada tu...ili uweze kuona hali hii inavyo'boa' unaweza kuilinganisha na watu wanaopenda 'kupiga mizinga' ...kila ukikutana nae hana habari nyingine zaidi ya kukueleza shida zake na kukuomba hela.

Sasa tunapofikia kupewa masharti kama haya mimi ningesema 'tunastahili' kwa sababu tunajidhalilisha wenyewe kwa kuombaomba kwetu. Pamoja na utajiri wote tulio nao lakini miaka 50 baada ya uhuru bado tunafikra za kuomba/kusaidiwa tu?

Huwezi kuwa ombaomba halafu ukasema eti hutaki masharti! Hakuna kitu cha bure...mwenyewe JK alishawahi kusema "ukitaka kula lazima na wewe ukubali kuliwa japo kidogo".
 
Hiyo mise...ge, baada ya kuona chumi zao zinayumba na wanaona aibu kusema kwamba ma wao ngoma ngumu ndio wametafuta mbinu ya kusitisha msaada(hongo.)
 
Safi sana cameron!! Wafrica tumezidi kuomba mana kila kitu tunacho mfano kama tanzania si yakuomba misada kwa madini mafuta gesi ardhi vivutio vya utalii, sisi si wakuomba msada wanatuzalau kwa kifupi cameron kamanisha kama mnataka misada muwe mashoga..

Ndio mana katulitea balozi basha ili atubaishie tupewe misada mana tumezidi kuomba na siku zote asili ya shoga ni mtu nguvu anazo na mgumu kujituma matokeo yake anapenda vya bure watu wanamla tigo, sasa kwa mtazamo wangu naona mtu akikuchoka akuchagulii tusi nimeumia sana na kauli yake aunt cameron na nampongeza kwa kututukana tuamke.
 
Jumuiya ya Madola inakosa relevance kwa siku za karibuni.

Kama kinachotuunganisha katika hiyi jumuiya ni Uingereza , na Uingereza ni mashoga na inelekea ni utamaduni wao.

Sisi tuliokuwa makoloni ya Uingereza SI mashoga wala hatuelekei kukubaliana na hilo kwa vile kimsingi ni tabia ya kishenzi.

Kulinda uhuru na ustaarabu wa Mwafrika tukijitoa katika umoja huu wa kishoga ni kulinda heshima yetu na ya vizazi vijavyo.
 
ukiwa omba omba ndio matatizo yake..kama sharti ndo hilo tuko sahihi tujitoe tu. waendelee kugongana wenyewe tu.tuache kuomba bana...
 
Sikubaliani na ushoga, nakataa, nakataa na nakataa. Naunga mkono juhudi za wale wanaosema kila liwezekanalo litumike kuonyesha hasira zetu na kukerwa kwetu na tabia ya Uingereza kuhusisha umaskini wetu na misaada ili tukubali kuimba wimbo wa Ushoga. Hii ni dharau, hii ni kejeli na haya ni matusi makubwa kwa taifa, kwanza wametuonaje watanzania na kwa nini wasipeleka Afrika kusini ambapo walisharidhia mambo hayo.

Baba wa taifa alishawahi kusema kuwa umasikini ni gharama, na inakuwa gharama kubwa ukipata baba anayependa kuishi kwa kuombaomba, wakati familia yake inadhalilika huku baba akibaki ombaomba akiimba sifa za wanaume wengine ikiwa ni pamoja na kuwatukuza. Tunaposema hapa kwa JF kuwa ogopeni misaada iongozeni nchi kujikwamua kiuchumi wakina Topical, Rejao, RW1, Mwita, Faiza foxy na wengineo wengi mumekuwa mnatukejeli kuwa safari za wakubwa nchi za nje zinalipa.

Sasa nawambia sawa zimelipa na kulipa kwenyewe leo wamewaambatanishia fedha zao na utamu wa ushoga ambao kwa taifa letu ni uchungu usiotafunika wala kumezeka. Kubalini yote sasa, mnalalama nini? Sisi ni nchi isiyokuwa na maadili ya Taifa, hatujawahi kutamka yale ambayo tunayataka na ndiyo maana wao hawajisikii taabu kututajia yao ili yawe yetu.

Wazungu hao walituheshima miaka ile, wakatuogopa sasa hawapati shida kututamkia matusi kama sehemu ya mawasiliano ya kawaida na serikali yetu. Wanadiriki kutuandikia barua ya kumleta balozi shoga, balozi shoga! shoga aje kufanya kazi ya ubalozi Tanzania! Waingereza uthubutu huu wanautoa wapi? Mnadhani eti kwa sababu sisi ni marofa?

Hapana kuna kitu kingine na hiki ndiyo kizungumzwe hapa. Wapo wanaosema kuwa sababu nchi yetu haina ya mahusiano ya kimataifa kama ipo inasemaje na ni ya lini? Je tuna maadili, na miiko ya taifa ambayo itakuwa misingi ya kuheshimiwa kwa sababu marafiki zetu watakuwa wametujua katika yale tunayokubaliana na yale tusiyokubalina ili tuweke uwigo wa kuheshimiana.

Tumeshuhudia Taifa limekuwa likipoteza misingi ya utaifa kwa kutokemea tabia za ukosefu wa maadili mema hasa kwa kundi la vijana lakini viongozi wetu kutoka makundi mbalimbali wamekaa kimya, tunashuhudia watu wanatembea uchi, kundi la ushoga linakuwa na kuongeza, klabu za maajabu hapa Dar, uvaaji usioendaneka na mila na desturi za nchi yetu, viongozi, wazazi, na wanachi tupo kimya kama vile hatuoni. Kwani mnafikiri Uingereza wameota kusema twende Tanzania kumpleka shoga?

Wanazotakwimu za kutosha na sitashangaa kama wana majina ya viongozi wanaoendekeza tabia hiyo, wanajua tabia hii imeenea kiasi gani na inashabikiwa kiasi gani na watu gani.

Ni ukichaa kuchimba shimo la kufugia panya halafu ukashangaa kuona nyoka amekutembelea, ulitaka nani akutembelee? Ni upumbavu kuruhusu mwanao kuuza bangi halafu ukashangaa kumuona anavuta.

Tunataaruki kukemea na kutaka kukata matawi ya ushoga wakati mti na mizizi yake iko imara. Katika vita hii ya ushoga si Uingereza bali mioyo na tabia za watanzania ambazo viongozi wetu waliacha zikajipanua bila uoga. Ni Uhuru na haki gani za mtu binafsi zinakuwa kero kwa watu wengine tena sehemu kubwa ya jamii ambayo anaowajibu kuitumikia.

Haki na uhuru usiozingatia maadili ya nchi ya nchi ni uchafuzi wa mazingira, haki ya mtu mmoja ni lazima itii matakwa ya jamii yake hilo halina mjadala hata kwao waingereza na wamerekani mabingwa wa haki za binadamu


Haya bwana kazi kwenu viongozi wetu wa makundi mbalimbali tuliwapa fursa ya kutuongoza basi na mtuongoze vizuri kutambua tataizo linalotukabili katika ushoga mimi na washukuru waingereza kufanya jambo ambalo limetuamsha kwa wakati mmoja watanzania na sasa tunakaribia kuzungumza lugha moja tusiishie kuukataa ushoga wa Waingereza tuukatae ushoga wetu hapa nchini tunazo taarifa, tunawajua watu hao tuwashughulikie sasa. Kama tulikuwa tunasubiri fursa na wakati muafaka sasa Waingereza wametuwezesha kupata hiyo fursa tuanze kujitathimini leo

.
Watanzania hii ni kazi kwelikweli lakini tutafika tu. Hizi ni harakati zingine za ukombozi ambazo zitawajenga watu kuthamini mila na desturi zao. Aluta continua

HUU NI MSALABA MWINGINE WA CCM NA SERIKALI YAK
 
Kama tumeshindwa kujitegemea kwa miaka 50 ya uhurui itatubidi tukabali masharti, hatuna jinsi!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Back
Top Bottom