Rais Magufuli: Tanzania tumesitisha usajili wa meli zote 470, tumejitoa Comprehensive Refugee Response Framework (CRRF)

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,968
141,975
Karibuni tufuatilie matangazo haya mubashara kupitia luninga ya TBC!

======

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amewahakikishia Mabalozi na wakuu wa mashirika ya kimataifa waliopo hapa nchini kuwa katika mwaka 2018 Serikali ya Awamu ya Tano itaendeleza juhudi za kuboresha mazingira ya uwekezaji ikiwemo mapambano dhidi ya rushwa, kuboresha miundombinu ya barabara, reli na usafiri wa anga, kuongeza uzalishaji wa umeme na kukabiliana na vikwazo vya biashara.

Mhe. Rais Magufuli amesema hayo leo tarehe 09 Februari, 2018 katika hafla ya mwaka mpya aliyowaandalia Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini, iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Kutokana na dhamira hiyo Mhe. Rais Magufuli ametoa wito kwa Mabalozi hao kuwahamasisha wawekezaji na wafanyabiashara kutoka nchi zao, kuja hapa nchini kuwekeza na kufanya biashara mbalimbali na kwamba Serikali itatoa ushirikiano wowote utakaohitajika.

Aidha, Mhe. Rais Magufuli amesema mwaka 2017 ulikuwa wenye mafanikio makubwa kwa Serikali kitaifa na kimataifa, ambapo iliendelea kutekeleza mpango wa maendeleo wa miaka 5 (2016/17-2020/2012) unaolenga kuiwezesha nchi kuwa ya uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025 na ametaja baadhi ya mafanikio hayo kuwa ni kuziba mianya ya ukwepaji wa kodi kulikowezesha kuongezeka kwa mapato kwa asilimia 7.87, ikiwemo rekodi ya juu kuwahi kufikiwa hapa nchini ya ukusanyaji wa Shilingi Trilioni 1.66 mwezi Desemba 2017.

Mafanikio mengine ni ukuaji mzuri wa uchumi wa asilimia 6.8 katika nusu ya kwanza ya mwaka 2017, kudhibiti mfumuko wa bei uliokuwa chini ya asilimia 5.5, kuongezeka kwa akiba ya fedha za kigeni na kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo pamoja na kuboresha huduma za kijamii zinazowagusa zaidi wananchi kama vile afya, elimu na maji.

Kuhusu azma ya kujenga viwanda, Mhe. Rais Magufuli amesema utekelezaji wa azma hii unakwenda vizuri ambapo katika kipindi cha miaka miwili viwanda 3,500 vimejengwa na vingine vingi vinaendelea kujengwa.

Aidha, Mhe. Rais Magufuli amesema kama ilivyofanya katika mwaka 2017 Tanzania itaendelea kutekeleza majukumu mbalimbali ya kikanda na kimataifa ikiwemo kushiriki katika juhudi za kutafuta amani, kushiriki harakati za usuluhishi wa migogoro ikiwemo ya Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Jamhuri ya Afrika ya Kati, Lebanon, Sudan na Sudani kusini.

Hata hivyo ameelezea kusikitishwa kwake na uamuzi wa Umoja wa Mataifa kuanza kutekeleza sera ya kupunguza gharama kwenye misheni za kulinda amani kwani kwa kufanya hivyo itadhohofisha jitihada za kutafuta amani kwenye maeneo yenye migogoro na kuhatarisha maisha ya walinda amani pamoja na raia wasio na hatia wanaoishi kwenye maeneo yenye migogoro.

Pia, Mhe. Rais Magufuli amesema pamoja na nia njema ya mpango wa majaribio wa kutafuta suluhu la kudumu ya tatizo la wakimbizi (Comprehensive Refugee Response Framework – CRRF) Tanzania imeamua kujitoa kutokana na changamoto za kiusalama na ukosefu wa fedha za kugharamia mpango huo.

Mhe. Rais Magufuli amezungumzia taarifa za kukamatwa kwa meli zenye kupeperusha bendera ya Tanzania zikiwa zimehusika katika uhalifu na kuwahakikishia Mabalozi hao kuwa meli hizo sio za Tanzania bali zilijipatia usajili wa Tanzania, na kwamba kufuatia hali hiyo Tanzania imechukua hatua ya kusitisha usajili wa meli zote 470 zenye usajili wa Tanzania na kusitisha zoezi la usajili mpya wa meli wakati uchunguzi zaidi ukiendelea kufanyika.

Kwa upande wake Naibu Kiongozi wa Mabalozi na wakuu wa mashirika ya kimataifa hapa nchini ambaye ni Balozi wa Saharawi Mhe. Brahim Salehe El-Mami Buseif amempongeza Mhe. Rais Magufuli na Serikali yake kwa juhudi kubwa zilizofanyika kuimarisha huduma za afya, elimu, maji na kuongeza ukusanyaji wa mapato na ameahidi kuwa Mabalozi na wakuu wa mashirika ya kimataifa wataendelea kushirikiana na Serikali katika kufanikisha miradi mbalimbali.

Gerson Msigwa

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

Dar es Salaam

09 Februari, 2018
IMG_20180210_004221.jpg

IMG_20180210_004227.jpg


======

The Head of State said yesterday that the government has allocated 64 plots for embassies that are ready to move to Dodoma. Dr Magufuli was speaking during the New Year Sherry Party, hosted for Heads of Diplomatic Mission at the State House.

He said that each plot has 5.5 acres and that the government avails the land free of charge for each embassy that is ready to move its operations to the central region. “The Dodoma Municipal Council Director is here with title deeds, we will distribute them for free to embassies that are ready to move to Dodoma,” he said. He added, “I am inviting you to Dodoma, personally, I will be moving from Dar es Salaam this year.”

The Head of State expressed appreciation to the United Nations for opening an office in the capital city in December, 2017. Commenting on the past year achievements, President Magufuli said his government is proud of the attainments it hasregistered in many spheres of endeavours during the past year. He said the government has successfully managed to focus on industrial development policy aiming at building up an industry- based economy.

He added that the government has been working closely with the private sector in the country and that it stands to invite both local and foreign investors to venture for investment opportunities in the country.

“I would like to assure you that Tanzania invites investors: We have been working closely with the private sector in the country. Some people, for their own intentions, have been accusing the government of not supporting or siding with the private sector, please ignore such rumours,” he said. On power generation, Dr Magufuli said the government is continuing to set strategies that will ensure implementation of power generation projects in the country.

He said the state’s goal is to generate 5000MW by 2020. “We are focusing at generating power from natural gas, hydro power project on which the Rufiji Hydropower Project is set to be implemented soon. He said upon completion, the project will be able to generate 2100MW. The Head of State assured the diplomats that the government conducted research to ensure there would be no environmental impact.

“I would like to assure you that there will be no environmental impact in the implementation of the ‘Rufiji Hydropower project,” he said. On supporting refugees, the Head of State said the government has decided to stop the Comprehensive Refugee Response Framework (CRRF) for security reasons and poor support from the United Nations.

He said few years ago, Tanzania wrote history by providing citizenship to 150,000 refugees at once and the International Community had promised to support the country with funds. However, President Magufuli said the International Community did not fulfil its promises and instead the government has been advised and encouraged to seek loans to take care of refugees.

He noted that for decades, the country has acted as home to hundreds of thousands of asylum seekers and refugees fleeing persecution from their countries. On ship registration, Dr Magufuli said the government has suspended the registration of new ships and has launched investigation on 470 ships.

“Tanzania flagged-ships have been seized several times for carrying illegal goods. We are making a close follow up on the matter, we are investigating all the ships that were registered in the country to establish the truth,” he said.

On peace missions, President Magufuli said Tanzania has been in the frontline to ensure peace and security by participating in various peace missions across the world.

He asked the UN to speed up the ongoing investigation on the brutal killing of 15 Tanzania peacekeepers and injuring more than 40 in the Democratic Republic of Congo (DRC) on December 8, last year
 
MABALOZI NI CHADEMA HAO,,,,,,,,,,,, SIO WAZALENDO HAHAHAAAAA

MANENO GANI WANAMWAMBIA MKUU
 
Mkuu wengine bado tupo kwenye majukumu
Tudadavulie yanayoendelea uko
 
Back
Top Bottom