Tanzania bila ufisadi inawezekana? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania bila ufisadi inawezekana?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by ggg, Dec 21, 2010.

 1. ggg

  ggg Member

  #1
  Dec 21, 2010
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 60
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Dk Hoseah adaiwa kufichua siri za JK Send to a friend Monday, 20 December 2010 23:53

  MKURUGENZI Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Dk Edward Hoseah, anadaiwa kufichua siri za Rais Jakaya Kikwete kwamba kiongozi huyo wa nchi asingependa vigogo serikalini kufikishwa mahakamani kwa tuhuma za rushwa.
  [​IMG] Dk Hoseah

  Kadhalika, mkuu huyo wa Takukuru anadaiwa kushindwa kuwafikisha mahakamani vigogo waliohusika na kashfa ya rada kwa sababu anahofia usalama wake, gazeti la The Guardian la Uingereza liliripoti juzi.

  Mbali na hofu hiyo, gazeti hilo pia lilieleza juzi kuwa Dk Hoseah alipewa maelekezo maalumu na Rais Kikwete kutoshughulikia kesi za rushwa zinazowahusu vigogo katika serikali yake na hasa marais waliomtangulia. The Guardian lilitoa taarifa hiyo likiunukuu mtandao wa habari wa WikiLeaks uliojizolea umaarufu duniani kwa kutoa habari za kiuchunguzi hasa baada ya mwasisi wake, Julian Paul Assange, kutiwa matatani.

  Kwa mujibu wa habari hiyo, Dk Hoseah, alisema hayo Julai 14 mwaka 2007, alipokuwa akizungumza na mwanadiplomasia wa Marekani, Purnell Delly jijini Dar es Salaam. Alisema uchunguzi wa kashfa ya rada ni hatari kwake kwa kuwa vigogo nchini, hawaguswi kwa tuhuma na kwamba "tayari alikuwa ameanza kupata vitisho".

  Akizungumza kwa huzuni na kusononeka, Dk Hoseah alidai kuwa kwa ari na utashi alionao katika vita dhidi ya ufisadi, angeweza kuwafungulia mashtaka watuhumiwa wa ufisadi, lakini ameshindwa kwa kuwa kesi hiyo inawagusa vigogo kadhaa, wakiwamo marais na waziri mkuu mstaafu na ndani ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ). "Biashara hiyo chafu iliwahusisha maafisa kuanzia ngazi ya Wizara ya Ulinzi na afisa mmoja au wawili wa ngazi za juu ndani ya jeshi, The Guardian lilieleza likinukuu vinasa sauti vya ubalozi huo.

  Dk Hoseah alitumia mkutano huo kueleza mafanikio ya Tanzania katika mapambano dhidi ya rushwa na kueleza kuwa matumaini yake ya awali kusimamia mkakati huo, yamevunjwa moyo. "Alituambia waziwazi (rais) kwamba tuhakikishe kesi inayomhusu rais au waziri mkuu na viongozi waliomtangulia, tusiziguse na ziwekwe chini ya meza," lilieleza gazeti hilo katika taarifa yake.
  Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na sheria zake ndogondogo, mtu yeyote aliyewahi kuwa rais wa nchi hawezi kufikishwa mahakamani kwa tuhuma zozote zinazomkabili.

  Lakini, wadau kadhaa wa masuala ya siasa, sheria, haki za binadamu na utawala bora wamekuwa wakiendesha harakati za kudai katiba mpya ambayo pamoja na mambo mingine, wametaka iondoe kinga ya rais ya kutoshitakiwa mahakamani hata mara baada ya kustaafu kwenye nafasi hiyo.
  "Kuna taarifa za ufisadi ndani ya Beki Kuu ya Tanzania (BoT). Pia Visiwani Zanzibar kuna mambo mengi yanayohusiana na rushwa na ufisadi,"alinukuliwa Dk Hoseah ambaye alieleza kuwa anaamini "maisha yake yatakuwa hatarini" iwapo atathubutu kuendesha uchunguzi huo.

  Taarifa hizo kutoka kumbukumbu za vinasa sauti vya ubalozi wa Marekani nchini, zimeeleza kuwa katika mazungumzo hayo, Dk Hoseah alikuwa anarudia na kusisitiza kuhusu usalama wake, akisema anaamini maisha yake yapo hatarini kwa sababu alishapokea ujumbe wa vitisho kupitia simu yake ya mkononi na barua. "Amesema (Dk Hoseah) amekuwa akikumbushwa mara kwa mara kwamba katika vita hiyo ya ufisadi, anapigana na matajiri na wenye nguvu katika vita dhidi ya ufisadi,"gazeti The Guardian lilimnukuu Delly, afisa huyo wa Marekani aliyekuwa akizungumza na Dk Hoseah.
  Imeelezwa katika taarifa hiyo kuwa sababu kubwa ya Dk Hoseah kujaribu kutia mguu kwenye sakata la rada ni taarifa ya uchunguzi wa Taasisi ya Kuchunguza Ufisadi ya Uingereza (SFO), ambayo ilieleza kinagaubaga kuhusu kesi hiyo. Delly alisema, Hoseah amekuwa akionywa katika vitisho hivyo kwamba anaweza akaiona chungu nchi yake ikiwa ataendelea na mapambano hayo.

  "Alisema (Dk Hoseah), ukihudhuria mikutano ya ndani na vigogo wa serikali, wanataka wakuone ukijihisi kwamba wao ndio wamekuweka katika cheo chako, lakini ukiwa mbishi wa kushikilia misimamo yako tu, basi uko katika hatari," gazeti hili lilimnukuu Delly. Awali akizungumza na gazeti hili, Dk Hoseah alikiri kupata vitisho vinavyohatarisha maisha yake kutokana na mapambano yake dhidi ya rushwa, lakini akasema hajaiona habari hiyo iliyonukuu mazungumzo yake na mwanadiplomasia huyo wa Marekani.  TAHARIFA IKO WAZI, UKIISOMA KWA MAKINI WAWEZA TAMBUA NI NANI WAHUSIKA.DR HOSEA ANAKATAA NINI? AU NDIO KILE ALICHO KISEMA KULINDA MAISHA YAKE, SWALI LANGU NI KWAMBA, Tanzania bila ufisadi inawezekana KAMA MAMBO YANYEWE NDIO HAYA?
   
 2. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #2
  Dec 21, 2010
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Haiwezikaniiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii!
   
 3. semango

  semango JF-Expert Member

  #3
  Dec 21, 2010
  Joined: Aug 24, 2010
  Messages: 532
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  kwa sasa TZ bila ufisadi ni ndoto isiyowezekana kutimia maana serikali imefunga ndoa na mafisadi "papa"
   
 4. STEIN

  STEIN JF-Expert Member

  #4
  Dec 21, 2010
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 1,764
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  kwani umesahau kwamba walikuja na ari mpya. nguvu mpya na kasi mpya na this time wamekuja na Zaidi ya hiyo.

  itabidi tuwe makini. Huyu hoseh naye ni mnafiki tu utaona jinsi watakavyo mlipua sasa.
   
 5. mkibunga

  mkibunga Senior Member

  #5
  Dec 21, 2010
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 196
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  sasa nchi imekaa tenge rais wetu yuko mtupu kwa hili atasema upinzani wanapiga kelele sasa mmeona dr slaa aliposema mkuu ni fisadi wakadhani anaganga njaa kweli watanzania bado na hili litapita jamaa ataendelea na safari zake kama kawida.TUMEKWISHA NCHI INALIWA WINGU JEUSI LIMETANDA RAIS WETU ANAPINGA MAFISADI WASICHUKULIWE HATUA NA KILA WAKATI ANASISITIZA KUWA WAKO SERIOUS NA WATAWACHUKULIA HATUA SIAMINI ni heri yule jamaa anayetaka kuleta wawekezaji wanunue mikoa ya tanga.kilimanjaro na arusha aje atuchukue tu tuwaachie pwani,singida,dodoma,songea,ambao wao ccm ni wazazi wao
   
 6. mkibunga

  mkibunga Senior Member

  #6
  Dec 21, 2010
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 196
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ebu kwanza mwone hosea kwenye picha ya thread hii ameonyesha ofisi tatu mashuri hapa nchini kwa rushwa 1 ya rais 2. waziri mkuu 3. jwtz hizi hazifai kwa rusha zinamerermeta kisha zinaturichmonduli mwisho zina epa mungu wangu tumekwisha ila cha moto mtakiona wikleaks wamesema bado kashifa za mapenzi za ofisi tatu zinakuja anikwa jinsi wanavyofanya huko majuu
   
 7. N

  Nonda JF-Expert Member

  #7
  Dec 21, 2010
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  Kama ni kweli Hosea anazuiwa kufanya kazi yake,ilimpasa ajiuzulu na baadae awashe moto kwa kuelezea sababu ya yeye kuacha kazi kwa umma.

  Kuendelea kwa TAKUKURU kushughulikia vidagaa na kuwaacha mapapa,vigogo bila kuguswa si ujasiri,wala si sababu ya msingi ya kujitetea kuwa amepata maelekezo kutoka juu.

  Kinachojionesha hapa ni kuwa Hosea ni mwoga! Hafanyi maamuzi magumu,hathubutu.

  Angejitoa muhanga kama hali hiyo ingeliokoa taifa. Kuna mnara wa mashujaa,kuna makaburi ya mashujaa.Angepata nafasi yake hapo. At least, katika nyoyo za Wananchi.Angekuwa ni mfano wa kuigwa katika harakati za kuirekebisha jamii yetu.
  Ameshindwa kazi yake basi aendelee na kazi aliyojipangia kuwasafisha,kuwakosha mafisadi.
   
Loading...