Hawa watu walipaswa kulipa fine kwa kutofuata mkataba wa mwanzo,baada ya kushikilia makinikia tuligundua ni watu wasiokuwa waaminifu,ndo ikapelekea kuwatoza fine. Hawahawa ambao si waaminifu sasa tunaingia nao mkataba mwingine,kwa kubadilisha jina la kampuni,je ile fine sasa anapaswa kuilipa nani? Hapo kuna Jambo la kuwekwa sawa sisi watanzania,tumefanya Jambo kwa maslahi ya nchi basi tujue maslahi yetu mapema, ili tusije kutwa na mambo yaliyotukuta mwanzo. Je hawa watu hawataweza kufanya waliyoweza kufanya kabla?
Sehemu pekee itakayoipatia faida nchi ni katika mrabaha na hisa zetu 16%, lakin tunafahamu kwenye hisa, hapa faida inapatikana kwenye gawio(devidents) au kwa kuuza hisa za mwanahisa.Tuangalie suala la hiyo 16%,hii ni hisa yetu Kama taifa,faida inayopatikana hapa ni kupitia gawio (devidents) ,kuhusu kuuza hisa ni Jambo ambalo halitaweza tokea,hatuwezi kuuza hizo hisa zetu hata kama thamani ya hisa itaongezeka,labda tuuze ili anunue fulani kwa maslahi yake binafsi.
Kuhusu devidents hapa kuna tegemea na sera ya kampuni. 16% ipo kwenye divident wakati makampuni mengi makubwa ya uchimbaji madini hayatoi dividents. Faida kubwa kwa wanahisa wa makampuni ya madini ni kutokana na mauzo ya hisa wakati zinapokuwa zimepanda. Kwa mfano tangazo hili tu la kusema Barrick imefikia maafikiano mazuri na serikali ya Tanzania, hisa za Barrick zitapanda, na baadhi ya wanahisa watauza hisa zao na kutengeneza faida. Kwa bahati mbaya serikali haitaziuza hisa zake kipindi chote, na hivyo kutokufaidi faida itokanayo ya kuongezeka thamani kwa hisa zake.
Jambo la pili, hata kama watatoa gawio, itakuwa ni baada ya muda mrefu maana kwenye migodi uwekezaji huwa ni mkubwa na haukomi. Bahati mbaya gawio ni mpaka baada ya Barrick kurudisha pesa yake aliyowekeza. Atarudisha lini wakati uwekezaji unaendelea? Ndiyo swali la msingi.
Kwa upande mwingine wa barick sasa tuangalie inafaidika vipi
Barrick katika hili wamefanikiwa sana kuliko hata mazingira ya mwanzo. Sasa wataweza kuipata hata miradi ambayo zamani wasingeipata. Maana ndani ya Barrick, sasa ipo serikali.
Kule kusakamwa kuwa mara Barrick wametiririsha maji ya sumu, mara Barrick wanawaonea wafanyakazi wazalendo, mara Barrick ni majizi na mabeberu - yote hayo sasa wameyashinda. Yamefikia mwisho. Hii sasa ni kampuni yetu. Kampuni ya Taifa letu inayobeba nembo ya Taifa, TWIGA. Mwenye kutaka kuihujumu kampuni hii kwa namna yoyote ile, anaihujumu kampuni ya serikali, atakuwa analihujumu Taifa. Na anayelihujumu Taifa amekosa uzalendo.
Sent using
Jamii Forums mobile app