illegal migrant
JF-Expert Member
- Oct 18, 2013
- 1,277
- 1,121
Salaam,
Naandika kwa uchungu mkubwa kuliko ule wa mjamzito, binafsi elimu niliyopata ni ya kuunga unga siku hizi tunasema ya kimagumashi, nashukuru Mungu niliweza kujiendeleza nikafanikiwa kuajiriwa na haya mashirika ya kimataifa ingawa kazi yangu ni ya kutumwa tumwa lakini si haba.
Katika kutumwa tumwa huku nimebahatika kuingia maofisi meeengi mno ya umma na hata ya binafsi katika kufanya shughuli mbali mbali,
Huwa nachukia sana ninapotumwa banki kwa maana najua siku yangu ndo itaishia huko mbaya zaidi ni pale napomkuta teller mmoja wakati kuna counter zaidi ya saba, mfano lile li benki lililopo kule posta ya zamani, unakaa kwenye foleni zaidi ya saa nzima ikifika zamu yako yule muhudumu anaweka kibao kimeandikwa closed akirudi anakwambia subiri kwanza maudhi mengi jamani,
Huu msamiati unaoitwa huduma kwa wateja kwetu hatuuelewi kabisa, kwenye ofisi za umma ni kawaida sana kuambiwa "mhasibu kafiwa na hawezi kumuachia mtu kwani idara ya fedha ni nyeti", leo hii ukitaka siku yako ivurugike piga simu huduma kwa wateja kwenye hii mitandao ya simu utaambiwa mfano "umia ikili wewe kila saa unakosea namba ya siri",
Mabosi wameajiri vimada wao mapokezi au ma secretary anakujibu vyovyote akiamini la kumfanya huna kwa kweli hatuko tayari na mabadiliko chanya yoyote kwa mfano hiyo jumuiya tuwaachie walio tayari sisi bado tupo saaaaana,