TANROADS wekeni taa za barabarani Morogoro

TANROADS wekeni taa za barabarani Morogoro

Tuko

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2010
Posts
11,180
Reaction score
7,354
TANROADS kwa kushirikiana na Manispaa ya Morogoro tunaomba muweke taa za kuongozea magari maeneo kadhaa mjini Morogoro kupunguza ajali na adha zingine.

Imekuwa ni karibia kila siku kushuhudiwa ajali zinazopelekea vifo kwenye makutano kadhaa mjini Morogoro, matukio ambayo yanaweza kupunguzwa kwa 100% kama maeneo hayo yatawekwa taa za kuongozea magari.

Maeneo hatarishi zaidi ni pamoja na

1. Barabara ya Modeko inapoingia kwenye barabara kuu ya kwenda Iringa
2. Makutano ya barabara eneo la Fire
3. makutano ya barabara eneo la Masika
4. Barabara ya Mazimbu inapoingia barabara kuu ya Dodoma
5. Barabara ya kuingia stendi kuu Msamvu

Na maeneo mengine ambayo naamini wanayajua...

Nawasilisha
 
Nadhani hata round-abouts ni suluhiso na ziko effective sana tu ... Tanga, kwa mfano, kuna round abouts tu/hakuna hata traffic lights na ni nadra sana kutokea ajali.
 
Umesahau kona ya prokula na old dar es salaam roads kila wk lazima ajali.
 
huo mji jua likizama tu na movement zote hupotea ni mji usio kuwa na harakati kabisa sijui kwa nini, maduka mengi sa kun na moja yashafungwa mapema, msamvu giza sana mpka ujenzi uishe sijui lini
 
Hili ndio eneo baya zaidi hasa nyakati za usiku
1. Barabara ya Modeko inapoingia kwenye barabara kuu ya kwenda Iringa

Hii barabara mimi ndio huwa sielewi nani anatakiwa amsubiri mwenzake apite kwanza.

2. Makutano ya barabara eneo la Fire

Sehemu nyingine ambayo haihitaji kuwekwa taa ila ni eneo hatari dereva anatakiwa awe makini, hasa wenye pikipiki ni pale mizani Kihonda sehemu ya kuingilia na kutokea. Wanye magari makubwa wakishatoka kupima huwa wanaingia kwa fujo sana barabara kuu.
 
Nadhani hata round-abouts ni suluhiso na ziko effective sana tu ... Tanga, kwa mfano, kuna round abouts tu/hakuna hata traffic lights na ni nadra sana kutokea ajali.

Ni kweli

Ila gharama ya kuchomekea round about hasa kwenye hizi barabara kuu za mikoani inaweza kuwa kubwa kiaina
 
Back
Top Bottom