TANROADS na Halmashauri ya jiji la Arusha wekeni Zebra

Ulongupanjala

JF-Expert Member
Apr 9, 2013
8,259
13,549
Habari zenu wote,

Naomba niliseme hili tatizo la kufutika kwa alama ya pundamilia (Zebra) kwenye barabara nyingi hapa Arusha mjini,imechukua miezi mingi kama sio miaka bila wahusika kulifanyia kazi,nakumbuka miaka michache nyuma niliona Rotary/Lions International wakipaka rangi hiyo mistari kwenye barabara ya jirani na TANESCO na TFA,lakini naona hawakumaliza kwa barabara zote.(Labda fungu liliisha)

Nimejiuliza ina maana TANROADS na halmashauri ya jiji,hawaoni kama hili ni tatizo,au hizo alama mwanzo zilichorwa kimakosa au wanataka watu wagongwe na magari/toyo wakivuka kwenye sehemu hizo ambazo madereva wengi wahasimami maana hakuna alaza ya Zebra tena?

Leo nitataja barabara mbili tu ambazo zilikuwa na Zebra na imefutika kwa muda mrefu sasa.
1.Barabara ya Namanga/Nairobi jirani na Triple A Night club
2.Barabara ya inayopita jirani na chuo cha ufundi Arusha(ATC) jirani na ghorofa za NHC (Kambi ya fisi)
Kama wao hawajui wapi palikuwa na alama hizo na zimefutika,nipo tayari kuwatembeza ili wajue na watuondolee kero hii inayotia aibu kwa mji kama wa Arusha tunaoita wa kitalii,lakini pia askari wa usalama barabarani nao hawaoni hili tatizo au wao wapu busy kuangalia over speed na kutofunga mkanda nk?

Tuna safari ndefu sana kuiona Tz tuitakayo!
 
Hilo ni kweli Emili yani mji mzima hakuna zebra hata sehemu mmoja trafic wamekazana na faini kila mahali huku wananchi wakishindwa kuvuka. Vituo vya toyo vimegeuka kuwavusha wananchi barabara .
 
Hilo ni kweli Emili yani mji mzima hakuna zebra hata sehemu mmoja trafic wamekazana na faini kila mahali huku wananchi wakishindwa kuvuka. Vituo vya toyo vimegeuka kuwavusha wananchi barabara .
Target yao kubwa ni kukusanya mapato kupitia makosa ya madereva bila kujali usalama wa wananchi.
Sijui wanasubiri tena wahisani waje kupaka rangi hizo zebra???
 
Naunga mkono hoja, ila napinga kurudishwa mistari ya parking iliyofutika pale Uhuru road, maana ilikuwa ni mtaji kwa wale jamaa wa wrong parking yaani ukikosea ukakanyaga kiduchu tu, gari yako inapigwa cheni na faini yake ni sh 50,000, yaani wale jamaa ni jipu na wezi waliokubuhu
 
Back
Top Bottom