TANROAD zibeni shimo barabara ya Mwaikibaki karibu na Clouds FM, linasababisha foleni kali

Nyikanavome

JF-Expert Member
Mar 3, 2008
482
176
Barabara ya Mwaikibaki inakuwa na foleni sana kuanzia Juzi kwa mida ya asubuhi na jioni na chanzo kikubwa ni shimo lililo pembezoni ya bara bara hiyo karibu na ofisi za clouds fm.

Pia eneo hilo lina mfereji wa maji machafu ambao umeziba kutakana na shimo hilo na kusababisha maji kusambaa barabarani na kuongeza adha ya foleni. Mie jana na leo asubuhi ilibidi nigeuze gari kabla ya njiapanda ya Kawe na kurudi Bagamoyo road ili kukwepa foleni.

Wahusika hasa TANROAD na Manispaa ya kinondoni, inabidi hili suala walishughukie kwa haraka ili kupunguza adha kwa wananchi.

Huo ni uzoefu wangu wa jana na leo, nafikiri na wengine waliopita njia hiyo hivi karibuni wanaweza kuchangia.
 
Back
Top Bottom