Wickama
Platinum Member
- Mar 8, 2009
- 1,568
- 1,350
Wakuu, muda mrefu tumeelezwa kuwa Mkoani Singida, Wilayani Manyoni, kijiji cha Sukamahela ndipo katikati ya Tanganyika. Tumeelezwa pia kwamba ma-surveyor wa mkoloni (niliambiwa wakijerumani) walichimbia alama (beacon) juu ya jabali kupatambua. Hii point na jabali ipo jirani na highway ya Dodoma-Singida. Kwa bahati mbaya haijageuzwa kuwa kivutio cha kitalii wala cha kiburudani kwa wasafiri. Yaani hata kijiji husika hakifaidi chochote. Kiufupi kwa sasa ni "chokambaya".
Mimi nawashauri Tanroads na mamlaka zingine hii sehemu ijengwe Round About kubwa itakayobeba sehemu za wasafiri kupumzika, kula, kupiga picha, stori, mikutano, harusi na mengineyo ili kupaenzi na kuieleza jamii yetu na hata wageni jiografia yetu. Kiasi hata wakazi wa hapo Sukamahela wafaidi jiografia yao.
Zipo nchi zimetengeneza roundabout kubwa kama hizo na zinavutia sana na kuingiza vipato (hii hapa chini ni Western Australia)
Picha: Nimezitoa Mitandaoni. Nawashukuru walioziweka