crome20
JF-Expert Member
- Feb 5, 2010
- 1,168
- 779
Kwa muda mrefu nimekuwa najiuliza, inawezekanaje barabara kuu za jiji kama Daresalam zitelekezwe namna ile. Najiuliza hivi viongozi wetu huwa hawaoni wivu wanapotembelea nchi za nje na kuona unadhifu na mpangilio wa hali ya juu ya majiji au miji yao tena kwa yale mambo ambayo si ya gharama kubwa bali utashi na ufuatiliaji tu.
Hebu tuwaulize TANROAD au Jiji la DSM inawezekanaje ukawa na kituo cha basi kama kile cha Buguruni sokoni au kama kile cha Malapa? Vituo vimejaa matope, mashimo, uchafu wa kila namna wakati bado hiyo ni perimeter ya city centre!!
Nilibahatika kwenda nje ya nchi, nilishangaa kuona city center za wenzetu unaweza kutembea zaidi ya masaa mawili ukiwa kwenye highways huku bustani zikianikisha mpangilo wa miji. Wakati hapa DAR baada ya kilomita 3-5 kutoka city center tayari uko kama kwenye kitongoji cha mji mdogo hivi. Eti City center ya DSM inaishia mnazi mmoja, kilometre 2 tu kutoka Posta Mpya ambapo ni reference ya city center yetu.
Yanayoikabili Barabara ya Uhuru pia yako kwenye barabara zingine na mengine wala hayahitaji gharama kubwa.
Nawashauri Tanroad kuondoa aibu hii ambayo ni maamuzi tu wala si mradi mkubwa. Pale Malapa hadi Daladala haziwezi kutumia kituo hicho kwa jinsi palivyochimbika, mashimo na maji machafu yakiwepo hapo kwa miaka mingi sasa.