Tangzo hili linanikwaza!!

Chiwa

JF-Expert Member
Apr 17, 2008
3,982
4,750
hivi hapa wadau inakuaje? anyway sijui mimi ni mshamba au wa kale! hili tangazo la mama mjamzito halinifulahishi hata kidogo na mbaya zaidi linatoka saa mbilimbili umepiga pozi na familia mnaangalia habari mara hao na uingizaji wao!
hivi tumeshindwa kutumia njia nyingine kueleza ni kwa jinsi gani huduma katika vituo vya afya zimeboreshwa mpaka kuwadharililisha wanawake? hivi kweli ?
mbaya zaidi wadada wa mjini wanaanza kuamini kuwa tendo la kuzaa ni tendo hatari sana kiasi kuwa wanafikiria ni bora ukipata mimba uitoe! linawajengea uoga wa ndoa watoto wetu na hasa ukichukulia kizazi tulichokilea hakina uwezo mkubwa wa kufikiri lakini kinajua vizuri kingereza na techinologia (wako digital zaidi)
nini hikina tamaduni na ustaharabu wetu unaruhusi hiki kitu kiwe hivi?
sijui nisaidie kwa kunielimisha nielewe vizuri nisikeleke tena.
 
You are absolutely right. Lina ukakasi
Eti nyuuuuuu nani asiyejua uchungu una mlio wake. Halina msg yo yote ya maana. Waliorekodi hawana ubunifu na wanaolirusha ni hovyo kabisa
 
likianza tu kujitokeza muwe mnazima tv mkuu, hiyo itasaidia sana ninahakika
teh...teh..teh....tatizo sio kuzima tv hasaidii kitu kichwani bado litakuwepo na inawezekana nikaumia zaidi nitajaribu
 
You are absolutely right. Lina ukakasi
Eti nyuuuuuu nani asiyejua uchungu una mlio wake. Halina msg yo yote ya maana. Waliorekodi hawana ubunifu na wanaolirusha ni hovyo kabisa

kweli bwana
tabu wanafikiri kila mtu anaweza kufanya kila kitu ni upuuzi tu kazi za kubebana matokeo yake wanafanya bila hata utafiti mdogo
 
Sana sana pale yule mama anapolia....Kama mtu uko mbali na TV na ni mara yako ya kwanza kulisikia utasema labda watu wananaliuiuuuu....Khaaa
 
sometimes watu wetu wa wizara wanakua bize zaidi kutafuta kamishen ya kurusha matangazo hadi wansahau content na context

na kuna kampuni moja ya matangazo nadhani wana mtu asiye creative wala sensitiv to culture... ila wanalamba sana mikataba ya jingles
 
Ukiona wanaume mnapinga kitu hapo ni dhana ya mfumo dume hakuna chochote.
Nani kakueleza wanawake/ wasichana wa kitanzania hawapendi kuzaa tatizo watazaje wakati wanaume wa kuoa hampo bali ni hit and run!

hivi hapa wadau inakuaje? anyway sijui mimi ni mshamba au wa kale! hili tangazo la mama mjamzito halinifulahishi hata kidogo na mbaya zaidi linatoka saa mbilimbili umepiga pozi na familia mnaangalia habari mara hao na uingizaji wao!
hivi tumeshindwa kutumia njia nyingine kueleza ni kwa jinsi gani huduma katika vituo vya afya zimeboreshwa mpaka kuwadharililisha wanawake? hivi kweli ?
mbaya zaidi wadada wa mjini wanaanza kuamini kuwa tendo la kuzaa ni tendo hatari sana kiasi kuwa wanafikiria ni bora ukipata mimba uitoe! linawajengea uoga wa ndoa watoto wetu na hasa ukichukulia kizazi tulichokilea hakina uwezo mkubwa wa kufikiri lakini kinajua vizuri kingereza na techinologia (wako digital zaidi)
nini hikina tamaduni na ustaharabu wetu unaruhusi hiki kitu kiwe hivi?
sijui nisaidie kwa kunielimisha nielewe vizuri nisikeleke tena.
 
huwa najiuliza mama mjamzito aliyewahi kujifungua hukon nyuma na akapata matatizo ya hapa na pale wakati wa kujifungua aonapo tangazo hilo litamsaidia kuongeza tahadhari yeye na mumewe au litamtia hofu zaidi ya kujifungua?huwa nahisi hofu itachukua nafasi zaidi....na hofu hiyo ni sababu tosha ya kuleta matatizo tena!
 
Kwa kweli tangazo hilo ni baya sana kwanza mi la udhalilishaji, mambo mengine ni mambo ya faragha. Tatizo ni waongozaji kutokuwa na ubunifu, Mimi mwaka fulani tangazo moja la kujihifadhi kina mama lilikuwa baya niliandika gazetini nalilipigwa marufuku kwani hata walioigiza wakadai kila wakilisikia wanafadhaika ( maana halisi) wakasema kilichowaponza ni kulipwa pesa baas. Ujumbeunaweza ukafikakwania ya staha zaidi.
 
Lile tangazo kusema kweli halina maana mm huwa nikiliona tu nabadili channel
 
kuna kitu wanaita kuzip zapping. kwa maana kuwa ukiona tangazo haliendani na mila na desturi za mahali ulipo una zip kwenye channel nyingine.
Pia nafikiri wamekosa ushauri.Ila mamlaka husika inabidi wachukue hatua.
 
Back
Top Bottom